Rais Samia Hakuhitaji Kiapo cha Urais

Kisanduku

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
284
482
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Makala hii ilitoka July 13, 2021 kwenye RAIA MWEMA ukurasa wa 13

Rais John Magufuli alifariki saa 12:00 jioni ya tarehe 17/03/2021, Rais Samia Suluhu Hassan aliapishwa masaa 40:15 baadaye, yaani tarehe 19/03/2021 saa 04:15 asubuhi.

Kiapo hiki kilifanya Chama cha Wanasheria nchini (TLS) kishauri ateuliwe waziri mkuu kwa kuwa ndivyo inavyoelekeza ibara ya 51(2) ya katiba yetu Tanzania.

Makundi yaliibuka ya kuipinga na kuiunga mkono TLS, lakini yote hayakuonyesha historia ya viapo. Makala hii inaonyesha historia hiyo ilivyo msingi usioepukika wa jambo hili.

Kuanzia mwaka 325 ukatoliki ulikuwa dini rasmi Ulaya na serikalini kulikuwa na maaskofu, mapadri na watawa.

Kuanzia mwaka 793 Ulaya ilikumbwa na vita za kila mara. Hivyo mtawala wa jamii alilazimika kuwa jasiri anayeweza kupigana vita. Jasiri huyo aliitwa "amiri jeshi mkuu", yaani mfalme au malkia.

Kwa kuwa dini ilitawala maisha, mtu aliaminika alipotoa tamko la kidini linaloitwa "oath" yaani "kiapo". Hivyo kila ajira ilianza kwa kuapa kumtii mfalme, yaani "oath of allegiance".

Kiapo cha watawala Ulaya kilianza mfalme Phocas wa Roma alipopishwa mwaka 602 kikaitwa "oath of coronation". Hata hivyo siku ya kuapishwa haikuwahi kuhesabika kama tarehe ya kuanza utawala wake.

Karne ya 16 ukatoliki ukaanza kutokuwa dini rasmi, maisha hayakuhitaji kuapisha kila mtu. Kiapo cha utii ("oath of allegiance") kikabaki tu kwa wanaoomba uraia na wasaidizi wa mfalme kama askari na wabunge.

Katika kiingereza neno "office" asili yake ni kilatini “opus” na “facere” yaani "kazi inayotendwa". Hata hapa limetafsiriwa mara 302 kwenye katiba kuwa ni "kazi" au "shughuli" au "majukumu" au "madaraka" au "kiti".

Hivyo ubunge, uwaziri, ujaji, urais zote ni "ofisi" ambazo Marekani zina kiapo kinachoitwa "oath of office", si kama Uingereza ambako serikali inaanza kazi pale waziri mkuu anapobusu mkono wa mfalme au malkia.

Hivyo mtawala alikosekana ofisini iwapo tu amefariki au kajiuzulu na mrithi alirithi ofisi sekunde ileile "kiti hakikubaki wazi". Mrithi wa mfalme aliitwa "prince" au "princess".

Je nini hutokea rais wa Tanzania akikosekana ofisini? Rais akikosekana ofisini ibara ya 47(1)(c) ya katiba inasema makamu atafanya "kazi zote za urais".

Bado watu duniani huuliza je, mrithi huanza kazi siku anapoapishwa au siku alipofariki mtangulizi? Hadi hapa unaweza kujibu swali hili ila tuone wataalam wanavyolijibu.

Mwaka 1984 "Tume ya Kurekebisha Sheria" ya Australia ilitoa ripoti iitwayo "Relating to the Demise of the Crown" ikieleza kwamba mrithi huitawala Australia kuanzia sekunde anapofariki mtawala na si lazima aapishwe.

Hata wasomi wa Uingereza wanaeleza hivyohivyo katika kitabu chao "Swearing in the new King, (ISBN: 9781903903810)". Sasa tuone mifano ya waliotawala Uingereza tangu sekunde waliyofariki baba zao.

Edgar aliyeitawala Uingereza tangu mwaka 959 aliapishwa mwaka 973. Elizabeth II ameitawala tangu Februari 1952 aliapishwa Juni 1953. Mfalme Edward VIII ameitawala mwaka 1936 na hakuapishwa kabisa.

Hata Marekani, makamu wa rais ndiye mrithi wa urais, hahitaji kuapishwa anaporithi urais. Mwaka 1841 William Harrison alifia madarakani wakati katiba ikisema, rais akifariki au kujiuzulu makamu "atafanya kazi zote za urais".

Mawaziri waliona makamu wa Rais John Tyler hajageuka kuwa rais ingawa anafanya kazi za urais. John Tyler akaona haiwezekani afanye "kazi zote" za urais halafu asiitwe rais, hivyo akajitangaza kuwa rais wa Marekani.

Japokuwa John Tyler aliapa kiapo cha urais yeye alikiita "superfluous" yaani hakikuhitajika, aliapa tu kupunguza ubishi uliokuwepo, kama kinavyoeleza kitabu "John Tyler, Champion of the Old South", ukurasa wa 202-203.

Mwaka 1967 Marekani iliingiza hoja za John Tayler kwenye katiba. Marekebisho hayo ya 25 yanasema rais akifariki au kujiuzulu, makamu anageuka kuwa rais, hayasemi aapishwe, ninayanukuu, "In case of the removal of the President from office or of his death or resignation, the Vice President shall become President".

Hivyo, hakuhitajiki kumuapisha mrithi anayerithi utawala, kote Uingereza na Marekani tulikorithi miundo yao.

Sasa tuirejee ibara ya 51(2) inayosema rais "akishashika madaraka" atateua waziri mkuu. Je, Rais Samia alishika lini madaraka ya urais? Mfumo wa urithi tuliouona na pia katiba yetu vinajibu swali hili kama ifuatavyo.

Moja, makamu wa rais ni mrithi kama "prince" na "princess", hivyo, si tu madaraka aliyarithi sekunde ya kifo cha Rais Magufuli, bali pia hakulazimika kuapishwa.

Mbili, kwa kuwa anapofanya "kazi zote" za rais ibara ya 47(1)(c) ya katiba haimuhitaji aapishwe, ndivyo pia haikumuhitaji aapishwe sekunde Rais Magufuli alipokosekana kazini kwa kufariki.

Kiapo alichoapa Rais Samia hakikuongeza jukumu jipya nje ya aliyoyapata sekunde ile aliyofariki Rais Magufuli. Hivyo Samia Suluhu ameanza urais tangu sekunde aliyofariki Rais Magufuli.

Hata inapotokea anapishwa, japo si lazima, ile mifano ya Uingereza imetuonyesha kwamba haapishwi wakati wa maombolezo kwani ni rahisi kusahau protokali kama ilivyotokea Tanzania na Marekani.

Mwaka 1963 Rais John Kennedy wa Marekani alipofariki waandaaji walisahau Biblia hadi Rais Lyndon Johnson akaapishwa kwa kutumia kitabu cha "Misale ya Waumini" wakati hakuwa mkatoliki.

Hata alipoapishwa Rais Samia ule mkuki na ngao ya taifa vilisahauliwa hivyo hatuna picha ya Rais Samia akiwa ameshika mkuki na ngao kama marais waliomtangulia.

Hata siku ya mazishi ya Rais Magufuli, Generali Venance Mabeyo, kwa maneno yake, alitaabika kumpongeza Rais Samia kwa kuwa haikuwa siku ya kupongeza.

Hitimisho ni kwamba hatujawahi kukosa amiri jeshi mkuu hata kwa robo sekunde. Hivyo tuache kuamini kwamba Samia alianza urais siku aliyoapishwa kwani aliuanza sekunde ileile aliyofariki Rais Magufuli, tarehe 17/03/2021.

Kinachotakiwa ni kuiondoa ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ili hata asiyetafiti atambue kirahisi kwamba rais anapofariki basi sekunde hiyohiyo makamu anakuwa rais ("automatically") kama Marekani walivyojirekebisha mwaka 1967.

Pia, maneno kiti cha "kuwa wazi" yaondolewe kwenye katiba kwani muundo wenye mrithi hauachi kiti wazi. Kitakachotusaidia ni katiba ya Marekaniambamo hayajawahi kuwemo maneno hayo.
 
ibara ya 37(5) imeweka sharti kuwa ikitokea Rais akifariki akiwa madarakani lazima makamu wa rais aapishwe, kumbuka Rais kikatiba ndio kiongozi wa nchi,serikali na amiri jeshi mkuu, hivyo ili aweze kuwa amiri jeshi mkuu na hayo majukumu mengine ni lazima aape, na lile gwaride la kijeshi lina umuhimu mkubwa sana,kiitifaki maana amirijeshi lazima awe mmoja tu ambaye ni Rais.na siyo mtu mwingine yoyote ama kwa kurithi ama kukasimishwa ni lazima ale kiapo
 
Tunahitaji katiba mpyaaa
 
umelala nayo naona unaota!
Uvccm woote mmelaanika
659443965.jpg
 
Wewe ambaye ni muumini wa ibara ya 37(5) isome pamoja na 37 (10) inayosema hivi

Bila ya kujali masharti yaliyoelezwa hapo awali katika ibara hii, mtu atakayetekeleza kazi na shughuli za Rais, kwa mujibu wa ibara hii hatakuwa na madaraka ya kulivunja Bunge, kumwondoa yeyote kati ya Mawaziri katika madaraka yake au kufuta uteuzi wowote uliofanywa na Rais.

ibara ya 37(5) imeweka sharti kuwa ikitokea Rais akifariki akiwa madarakani lazima makamu wa rais aapishwe, kumbuka Rais kikatiba ndio kiongozi wa nchi,serikali na amiri jeshi mkuu, hivyo ili aweze kuwa amiri jeshi mkuu na hayo majukumu mengine ni lazima aape, na lile gwaride la kijeshi lina umuhimu mkubwa sana,kiitifaki maana amirijeshi lazima awe mmoja tu ambaye ni Rais.na siyo mtu mwingine yoyote ama kwa kurithi ama kukasimishwa ni lazima ale kiapo
 
Wewe ambaye ni muumini wa ibara ya 37(5) isome pamoja na 37 (10) inayosema hivi

Bila ya kujali masharti yaliyoelezwa hapo awali katika ibara hii, mtu atakayetekeleza kazi na shughuli za Rais, kwa mujibu wa ibara hii hatakuwa na madaraka ya kulivunja Bunge, kumwondoa yeyote kati ya Mawaziri katika madaraka yake au kufuta uteuzi wowote uliofanywa na Rais.
kumbuka kwa mujibu wa ibara hii 37(5) haihusiani na kukaimu tena hii anaapa kuwa Rais kamili ma anakuwa na madaraka yote. ibara hiyo inaeleza kwa atakayekaimu.
 
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Makala hii ilitoka July 13, 2021 kwenye RAIA MWEMA ukurasa wa 13
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Rais John Magufuli alifariki saa 12:00 jioni ya tarehe 17/03/2021, Rais Samia Suluhu Hassan aliapishwa masaa 40:15 baadaye, yaani tarehe 19/03/2021 saa 04:15 asubuhi.

Kiapo hiki kilifanya Chama cha Wanasheria nchini (TLS) kishauri ateuliwe waziri mkuu kwa kuwa ndivyo inavyoelekeza ibara ya 51(2) ya katiba yetu Tanzania.

Makundi yaliibuka ya kuipinga na kuiunga mkono TLS, lakini yote hayakuonyesha historia ya viapo. Makala hii inaonyesha historia hiyo ilivyo msingi usioepukika wa jambo hili.

Kuanzia mwaka 325 ukatoliki ulikuwa dini rasmi Ulaya na serikalini kulikuwa na maaskofu, mapadri na watawa.

Kuanzia mwaka 793 Ulaya ilikumbwa na vita za kila mara. Hivyo mtawala wa jamii alilazimika kuwa jasiri anayeweza kupigana vita. Jasiri huyo aliitwa "amiri jeshi mkuu", yaani mfalme au malkia.

Kwa kuwa dini ilitawala maisha, mtu aliaminika alipotoa tamko la kidini linaloitwa "oath" yaani "kiapo". Hivyo kila ajira ilianza kwa kuapa kumtii mfalme, yaani "oath of allegiance".

Kiapo cha watawala Ulaya kilianza mfalme Phocas wa Roma alipopishwa mwaka 602 kikaitwa "oath of coronation". Hata hivyo siku ya kuapishwa haikuwahi kuhesabika kama tarehe ya kuanza utawala wake.

Karne ya 16 ukatoliki ukaanza kutokuwa dini rasmi, maisha hayakuhitaji kuapisha kila mtu. Kiapo cha utii ("oath of allegiance") kikabaki tu kwa wanaoomba uraia na wasaidizi wa mfalme kama askari na wabunge.

Katika kiingereza neno "office" asili yake ni kilatini “opus” na “facere” yaani "kazi inayotendwa". Hata hapa limetafsiriwa mara 302 kwenye katiba kuwa ni "kazi" au "shughuli" au "majukumu" au "madaraka" au "kiti".

Hivyo ubunge, uwaziri, ujaji, urais zote ni "ofisi" ambazo Marekani zina kiapo kinachoitwa "oath of office", si kama Uingereza ambako serikali inaanza kazi pale waziri mkuu anapobusu mkono wa mfalme au malkia.

Hivyo mtawala alikosekana ofisini iwapo tu amefariki au kajiuzulu na mrithi alirithi ofisi sekunde ileile "kiti hakikubaki wazi". Mrithi wa mfalme aliitwa "prince" au "princess".

Je nini hutokea rais wa Tanzania akikosekana ofisini? Rais akikosekana ofisini ibara ya 47(1)(c) ya katiba inasema makamu atafanya "kazi zote za urais".

Bado watu duniani huuliza je, mrithi huanza kazi siku anapoapishwa au siku alipofariki mtangulizi? Hadi hapa unaweza kujibu swali hili ila tuone wataalam wanavyolijibu.

Mwaka 1984 "Tume ya Kurekebisha Sheria" ya Australia ilitoa ripoti iitwayo "Relating to the Demise of the Crown" ikieleza kwamba mrithi huitawala Australia kuanzia sekunde anapofariki mtawala na si lazima aapishwe.

Hata wasomi wa Uingereza wanaeleza hivyohivyo katika kitabu chao "Swearing in the new King, (ISBN: 9781903903810)". Sasa tuone mifano ya waliotawala Uingereza tangu sekunde waliyofariki baba zao.

Edgar aliyeitawala Uingereza tangu mwaka 959 aliapishwa mwaka 973. Elizabeth II ameitawala tangu Februari 1952 aliapishwa Juni 1953. Mfalme Edward VIII ameitawala mwaka 1936 na hakuapishwa kabisa.

Hata Marekani, makamu wa rais ndiye mrithi wa urais, hahitaji kuapishwa anaporithi urais. Mwaka 1841 William Harrison alifia madarakani wakati katiba ikisema, rais akifariki au kujiuzulu makamu "atafanya kazi zote za urais".

Mawaziri waliona makamu wa Rais John Tyler hajageuka kuwa rais ingawa anafanya kazi za urais. John Tyler akaona haiwezekani afanye "kazi zote" za urais halafu asiitwe rais, hivyo akajitangaza kuwa rais wa Marekani.

Japokuwa John Tyler aliapa kiapo cha urais yeye alikiita "superfluous" yaani hakikuhitajika, aliapa tu kupunguza ubishi uliokuwepo, kama kinavyoeleza kitabu "John Tyler, Champion of the Old South", ukurasa wa 202-203.

Mwaka 1967 Marekani iliingiza hoja za John Tayler kwenye katiba. Marekebisho hayo ya 25 yanasema rais akifariki au kujiuzulu, makamu anageuka kuwa rais, hayasemi aapishwe, ninayanukuu, "In case of the removal of the President from office or of his death or resignation, the Vice President shall become President".

Hivyo, hakuhitajiki kumuapisha mrithi anayerithi utawala, kote Uingereza na Marekani tulikorithi miundo yao.

Sasa tuirejee ibara ya 51(2) inayosema rais "akishashika madaraka" atateua waziri mkuu. Je, Rais Samia alishika lini madaraka ya urais? Mfumo wa urithi tuliouona na pia katiba yetu vinajibu swali hili kama ifuatavyo.

Moja, makamu wa rais ni mrithi kama "prince" na "princess", hivyo, si tu madaraka aliyarithi sekunde ya kifo cha Rais Magufuli, bali pia hakulazimika kuapishwa.

Mbili, kwa kuwa anapofanya "kazi zote" za rais ibara ya 47(1)(c) ya katiba haimuhitaji aapishwe, ndivyo pia haikumuhitaji aapishwe sekunde Rais Magufuli alipokosekana kazini kwa kufariki.

Kiapo alichoapa Rais Samia hakikuongeza jukumu jipya nje ya aliyoyapata sekunde ile aliyofariki Rais Magufuli. Hivyo Samia Suluhu ameanza urais tangu sekunde aliyofariki Rais Magufuli.

Hata inapotokea anapishwa, japo si lazima, ile mifano ya Uingereza imetuonyesha kwamba haapishwi wakati wa maombolezo kwani ni rahisi kusahau protokali kama ilivyotokea Tanzania na Marekani.

Mwaka 1963 Rais John Kennedy wa Marekani alipofariki waandaaji walisahau Biblia hadi Rais Lyndon Johnson akaapishwa kwa kutumia kitabu cha "Misale ya Waumini" wakati hakuwa mkatoliki.

Hata alipoapishwa Rais Samia ule mkuki na ngao ya taifa vilisahauliwa hivyo hatuna picha ya Rais Samia akiwa ameshika mkuki na ngao kama marais waliomtangulia.

Hata siku ya mazishi ya Rais Magufuli, Generali Venance Mabeyo, kwa maneno yake, alitaabika kumpongeza Rais Samia kwa kuwa haikuwa siku ya kupongeza.

Hitimisho ni kwamba hatujawahi kukosa amiri jeshi mkuu hata kwa robo sekunde. Hivyo tuache kuamini kwamba Samia alianza urais siku aliyoapishwa kwani aliuanza sekunde ileile aliyofariki Rais Magufuli, tarehe 17/03/2021.

Kinachotakiwa ni kuiondoa ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ili hata asiyetafiti atambue kirahisi kwamba rais anapofariki basi sekunde hiyohiyo makamu anakuwa rais ("automatically") kama Marekani walivyojirekebisha mwaka 1967.

Pia, maneno kiti cha "kuwa wazi" yaondolewe kwenye katiba kwani muundo wenye mrithi hauachi kiti wazi. Kitakachotusaidia ni katiba ya Marekaniambamo hayajawahi kuwemo maneno hayo.
Wambie Marekari waje waige kwetu.

Kitu kuwa wazi ni sahihi na dhahiri. Haina haj aya kutumia akili kujua kiti kiko wazi.
 
Yaani wewe! Ulikuwepo nchini kipindi Cha kifo cha JPM? Mtanange kugombania kubaki Ikulu uliuona au uliusikia tu?
Sasa nikuulize; huyo #SSH si alikula kiapo? Sasa mbona bado mnamdharau ndani ya ccm?
Kwa hulka zenu hizo mnadhani asingekula kiapo cha urais mngeendelea kumsikiliza?

NB: Nilichogundua ccm ni genge baya zaidi ya lile la fisi. Wazandiki!
 
Makala yako ni nzuri kwa sababu za kihistoria ila kuhusu Samia kuwa alianza kazi mara moja Magufuli alipokufa ninakupinga.

Magufuli alifariki tarehe 9/ 03/ 2021 au kabla ya hapo. Na Samia alitangaza msiba tarehe 17/ 03/ wa na aliapishwa tarehe19/ 03/ 21.

Kwa kipindi cha siku 8 Serikali ilikuwa imetekwa nyara na kikundi cha wasiri wa Magufuli ( Bashiru, Chamuriho, Prof Mchembe, Dotto James) ambao walikuwa ndiyo watendaji wakuu wa Serikali.

Bila hisani ya Mabeyo CDF, Tanzania ingekuwa ni mahali tofauti kabisa na tulivyo sasa.

Kwa mazingira hayo ilikuwa lazima Samia aapishwe ili Sukuma Gang watengwe
 
Back
Top Bottom