Rais Samia, chukua tahadhari kuwa "Ukicheka na nyani utavuna mabua"

MEXICANA

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
1,772
2,032
Usipende sana mama kufanya jambo ili kuwafurahisha hawa jamaa utaambulia failure.

Tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu ndani yao hakuna nia njema. Baba yao ni baba wa uongo kama inavyojulikana.
Lengo ni kuangusha state kwa gharama yoyote.

Alitokea nabii mmoja katika roho ya Elia, huyo alikuwa haangalii sura za akina Ahabu, sina mda wa kutosha kukuelezea namna huyo nabii alivyowanyoosha hao jamaa ili mioyo yao igeuke na kurejea katika uzalendo wa nchi yao.

Take care mama, hawa watu watakupoteza soon, historia inasema, Lucifer na malaika zake ni wapinzani wa Mungu na haitatokea wawe kitu kimoja na Jehova, na ikitokea hivyo haikosi kutokea kwa anguko kubwa la wafalme juu ya uso wa nchi.

Lucifer ni mshitaki wa ndgu zetu,hilo linajulikana, hakosi kuibua mashitaka ya uongo na ya kweli maana ndio kazi yake.

Kwa kipindi hiki tarajia mengi. Yatakuja kwa sura ya uzuri kumbe original intent ni ile ile iliyokuwako tangu kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu.

“Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

— 2 Wakorintho 11:14 (Biblia Takatifu)
 
Mtoa maada kula tano

Watu hawajui ukweli wa mambo na Siri zilizopo ulimwenguni Hapa unaokaa chini ya yule joka kuu

Namuomba mama Kama akipungukiwa hekima na aombe kwa mwenyeziMungu anayetoa. Kuna dalili sio nzuri nchini tangu kukamatwa kwa Tani ya ngada baharini mpk kuachiwa kwa mafisadi mpk matukio ya wizi kuongezeka na corona kuogopwa tena Ni wazi TAMAA imewaka na zao la tamaa linafahamika.
 
Unawezaje kuyajua yalo ndani ya moyo wa mtu? Kama una taarifa za uhakika peleka kwa mama alisharihusu hilo. Acha kuteseka na Uongozi wa HAKI
 
Ataiweka ccm hatarini huyu mama kwa kucheka na nyani. Hawa wanafadhiliwa na mabeberu. Aweke akilini uongo wa lissu na mbowe na kejeli zao dhidi ya magufuli. Asidhani anaweza kujenga nchi kushirikiana na chadema.
 
Ukuandika jambo bila kuhusisha katika jamii ya watanzania ni kundi gani watamuangusha mama, ambao ni wawakilishi wa lucifer, ambao watamuangusha mama hujaongea kitu hapo. Ni zero work done. Uwe muwazi ueleweke.

Kwani kununa na kufoka ndipo rais anafanikiwa uongozi .tusitishane nchi iko salama kama mikononi mwa JPM, hata leo tuko salama. Unless uwe mitume wa kutabiri majanga na hayaji sasa.
 
Utawala wa kiimla ndio maana mwengine kapotezwa, wewe unatakiwa ulielewe hilo na hata sasa hivi mkileta tena ujinga kazi itarudiwa tu.

Madharau mwiba guu huota tende, msiwachukulie wapinzani ki-mchezo mchezo au mtakuwa mnafanya hivyo at your own peril.
 
Back
Top Bottom