Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa serikali atakayoiunda endapo atachaguliwa itaendelea kwa kasi zaidi katika kutekeleza mpango wa kuboresha maisha ya watu na ustawi wa jamii, kama ambavyo Ilani ya CCM inavyoelekeza.
Akizungumza leo Jumamosi Oktoba 4, 2025 katika mkutano wa mwisho wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika kwenye viwanja vya CCM Sabasaba mjini Babati, mkoani Manyara, Dkt. Samia amesema dhamira ya CCM ni kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma muhimu za maji, umeme, afya na elimu.
Ameongeza kuwa serikali yake itashughulikia kwa dhati maombi yote yaliyowasilishwa kwake na wagombea ubunge wa majimbo ya mkoa wa Manyara pamoja na wabunge wa viti maalum, huku ikihakikisha miradi yote ya maendeleo mkoani humo inatekelezwa kikamilifu.
Aidha, akitaja utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020, Dkt. Samia amesema serikali ya awamu ya sita tayari imetoa zaidi ya shilingi bilioni 700 kwa ajili ya miradi mbalimbali mkoani Manyara, nje ya miradi ya kitaifa, jambo linalothibitisha nia ya chama hicho katika kuwaletea wananchi maendeleo.