GE2025 Rais Samia azindua Maabara Kuu ya Kilimo Dodoma

GE2025 Rais Samia azindua Maabara Kuu ya Kilimo Dodoma

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua Maabara Kuu ya Kilimo ya Taifa (National Laboratory Centre) mkoani Dodoma, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha tija, ubunifu na utafiti katika sekta ya kilimo

Mradi huo wa kimkakati uliozinduliwa siku ya Ijumaa Agosti 08, 2025 kama sehemu ya maadhimisho ya Nanenane umebuniwa kwa lengo la kusaidia wakulima kupata suluhisho la kitaalamu kwa changamoto mbalimbali zinazokabili uzalishaji. Kupitia maabara hiyo ya kisasa, kutakuwa na vitengo maalum vya uchunguzi wa mimea, magonjwa, wadudu, udongo na sumu kuvu, pamoja na maabara ya tishu kacha kwa ajili ya kuzalisha miche isiyo na magonjwa

Vilevile, kituo hicho kitahusisha maabara za kuchunguza ubora wa mbegu na kufanyia uchambuzi wa kemikali kwenye udongo, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao kwa njia salama, endelevu na yenye ufanisi

Kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akizungumza na Rais Samia, mradi huu ulipata ufadhili kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na ndio utakaokuwa kituo cha kurejelewa na maabara zote nchini.

Uwepo wa kituo hicho nchini unatarajiwa kuchochea mageuzi ya kilimo, kuhakikisha wakulima wanapata huduma za kitaalamu ndani ya nchi, na kupunguza gharama za uchunguzi zinazotegemea maabara za nje

1754649368814.png


1754649446441.png


Chanzo: JAMBO TV & ITV DIGITAL
 
Back
Top Bottom