Rais Samia apeleka Bilioni 300 Tume ya umwagiliaji

Rais Samia apeleka Bilioni 300 Tume ya umwagiliaji

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,282
Reaction score
3,955
Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mwaka wa fedha 2025|2026, Tume ya Umwagiliaji iliidhinishiwa jumla ya Shilingi 382,138,408,000.

Fedha hizi zimetengwa kama ifuatavyo:

Shilingi 308,721,961,000 ni fedha za Maendeleo, huku Shilingi 73,416,447,000 zikielekezwa kwa matumizi ya kawaida.

Soma pia: GE2025 - Rais Samia: Tumeweka fedha nyingi katika Umwagiliaji kukabili Mabadiliko ya Tabianchi

Fedha za Maendeleo zinatokana na Shilingi 259,617,801,000 kutoka vyanzo vya ndani na Shilingi 49,104,160,000 kutoka vyanzo vya nje

Hii itawawezesha kutekeleza miradi ya umwagiliaji inayolenga kuongeza tija na maendeleo ya sekta ya kilimo nchini katika mwaka 2025|2026

Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itachimba visima 500 vya umwagiliaji vitakavyomwagilia eneo lenye ukubwa wa hekta 30,393.39 katika Halmashauri 178 nchini na kunufaisha wakulima 58,903

1755088256999.png

Chanzo: ITV DIGITAL
 
Back
Top Bottom