PreGE2025 Rais Samia azindua Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania Tambukareli-Dodoma, leo tarehe 05 April, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Majaji wanapaswa kutenda haki tu maana kila kitu wamepewa., wamepewa Majengo mazuri, nyumba safi, mishahara minono, usafiri, ulinzi na marupurupu kibao.
 
Kwahiyo hamtaki jengo pia

Ila nyie jamaa mbumbumbu sana

Mna kipi mnakikubali nyie?

Hapo mahakamani si kila siku mnaenda kufungua mashauri kibao?
Usiwe mjinga ww, jaji anajengewa nyumba ya 1b, wakati utendaji wa mahakama sio wa kuridhisha. Watu wanaenda kufungua mashitaka hapo mahakamani sio kwakuwa wana imani na hizo mahakama, ila ni kwakuwa hawana pa kwenda.

Hebu waruhusu wasio na imani na hizi mahakama wakafungue mashitaka kwenye mahakama za nje, uone kama kuna mtu utamuona kwenye mahakama zetu.
 
Wewe ni pimbi sana unadhani hizo mahakama anaendesha raia wa urusi au?

Si nyie nyie watanzania mnaendesha?

Kasomee sasa Sheria uje usimamie haki dogo
 
Rais Samia Suluhu Hassan ataongoza hafla ya uzinduzi wa majengo ya Mahakama ya Tanzania leo Aprili 5, 2025, katika Mtaa wa Tambukareli, jijini Dodoma.

Majengo hayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha miundombinu ya utoaji haki, kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuimarisha upatikanaji wa huduma za kimahakama kwa wananchi.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa juu wa serikali, Mahakama na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria.

Miradi hiyo ni pamoja jengo la makao makuu ya Tume ya Utumishi wa Mahakama, ambalo lipo mkabala na jengo la makao makuu ya Mahakama ya Tanzania.

Mradi wa pili utakaozinduliwa ni makazi za majaji ambayo yapo karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma na mradi wa tatu ni jengo la makao makuu ya Mahakama ya Tanzania lenye jumla ya ghorofa tisa na ambalo helikopta inaweza kutua juu yake.

Fuatilia matangazo ya moja kwa moja hapa

Majaji wa Mahakama ya Rufani walivyowasili katika eneo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania panapofanyika hafla ya uzinduzi rasmi wa majengo ya Mahakama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Willium Lukuvi akisalimiana na baadhi ya viongozi waliowasili katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania panapofanyika Halfa ya Uzinduzi wa Majengo ya Mahakama ya Tanzania.

Rais Samia alivyopanda mti na kukata utepe uzinduzi wa majengo ya Mahakama ya Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule; "Jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania si tu kwa ajili ya huduma za kimahakama, bali ni urithi wa kipekee unaoleta hadhi, fursa za kiuchumi, na kuvutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi."

"Muundo huo wa kipekee umebeba maono, heshima, na urembo unaoitangaza Tanzania kimataifa."

"Tunamshukuru Rais kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kupitia muundo huu wa kipekee wa Mahakama. Ni fahari kwa Dodoma, ni fahari kwa nchi."

Rais Samia Suluhu akizindua Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Dodoma

"Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ni la sita kwa ukubwa kati ya majengo ya Makao Makuu ya Mahakama duniani. Tanzania tuko pazuri sana na tuna haki ya kutembea kifua mbele, na ni la kwanza barani Afrika."

"Serikali imefanya makusudi kujenga mazingira mazuri kwa majaji wetu. Lakini mazingira haya yaendane na huduma bora zinazotolewa ndani ya majengo haya."

"Jengo jipya la Mahakama Kuu litafanya kazi na kutoa huduma bila kutumia karatasi, hatua inayolenga kuboresha utoaji wa haki kwa kutumia teknolojia za kisasa. Jengo hilo jipya litatumika kuendesha shughuli za kimahakama kwa mfumo wa kidijitali, hatua itakayosaidia kuongeza ufanisi na uwazi katika shughuli za utoaji haki."

"Tumearifiwa kuwa mahakama hii tunayoizindua leo inakwenda kutoa huduma bila karatasi, yaani paperless, ni mambo ya mtandao na teknolojia ndiyo yatatawala humu ndani,"

maendeleo makubwa sana
 
Nimegundua viongozi wa Africa hawana kazi. Rais anapaya wapi muda wa kuzindua majengo na matatizo yote tuliyonayo?
Matatizo mnayo chadema tu ndo maana mnawapiga wajinga tone tone, wengine hawana shida za kuzidi au wanaweza kusema nazo shida zao ndo maana hawana makasiriko yasiyo na msingi.
 
Hii kitu niliwaambia watu wakawa wanabisha viongoz wetu hawana plan na mipango ya kuzikomboa nchi zao top za nchi zinazunguka kuzindua hospital mara shule vitu pet sana badala ya kukaa chin wawe wanabrainstorm jinsi ya kututoa tulipo na mamipango makubwa
 
Matatizo mnayo chadema tu ndo maana mnawapiga wajinga tone tone, wengine hawana shida za kuzidi au wanaweza kusema nazo shida zao ndo maana hawana makasiriko yasiyo na msingi.
Ile michango ya mwenge wa uhuru huwa mnawapiga wajinga ama wajanja?
 
Rais Samia Suluhu Hassan ataongoza hafla ya uzinduzi wa majengo ya Mahakama ya Tanzania leo Aprili 5, 2025, katika Mtaa wa Tambukareli, jijini Dodoma.

Majengo hayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha miundombinu ya utoaji haki, kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuimarisha upatikanaji wa huduma za kimahakama kwa wananchi.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa juu wa serikali, Mahakama na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria.

Miradi hiyo ni pamoja jengo la makao makuu ya Tume ya Utumishi wa Mahakama, ambalo lipo mkabala na jengo la makao makuu ya Mahakama ya Tanzania.

Mradi wa pili utakaozinduliwa ni makazi za majaji ambayo yapo karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma na mradi wa tatu ni jengo la makao makuu ya Mahakama ya Tanzania lenye jumla ya ghorofa tisa na ambalo helikopta inaweza kutua juu yake.

Fuatilia matangazo ya moja kwa moja hapa

Majaji wa Mahakama ya Rufani walivyowasili katika eneo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania panapofanyika hafla ya uzinduzi rasmi wa majengo ya Mahakama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Willium Lukuvi akisalimiana na baadhi ya viongozi waliowasili katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania panapofanyika Halfa ya Uzinduzi wa Majengo ya Mahakama ya Tanzania.

Rais Samia alivyopanda mti na kukata utepe uzinduzi wa majengo ya Mahakama ya Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule; "Jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania si tu kwa ajili ya huduma za kimahakama, bali ni urithi wa kipekee unaoleta hadhi, fursa za kiuchumi, na kuvutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi."

"Muundo huo wa kipekee umebeba maono, heshima, na urembo unaoitangaza Tanzania kimataifa."

"Tunamshukuru Rais kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kupitia muundo huu wa kipekee wa Mahakama. Ni fahari kwa Dodoma, ni fahari kwa nchi."

Rais Samia Suluhu akizindua Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Dodoma

"Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ni la sita kwa ukubwa kati ya majengo ya Makao Makuu ya Mahakama duniani. Tanzania tuko pazuri sana na tuna haki ya kutembea kifua mbele, na ni la kwanza barani Afrika."

"Serikali imefanya makusudi kujenga mazingira mazuri kwa majaji wetu. Lakini mazingira haya yaendane na huduma bora zinazotolewa ndani ya majengo haya."

"Jengo jipya la Mahakama Kuu litafanya kazi na kutoa huduma bila kutumia karatasi, hatua inayolenga kuboresha utoaji wa haki kwa kutumia teknolojia za kisasa. Jengo hilo jipya litatumika kuendesha shughuli za kimahakama kwa mfumo wa kidijitali, hatua itakayosaidia kuongeza ufanisi na uwazi katika shughuli za utoaji haki."

"Tumearifiwa kuwa mahakama hii tunayoizindua leo inakwenda kutoa huduma bila karatasi, yaani paperless, ni mambo ya mtandao na teknolojia ndiyo yatatawala humu ndani,"
 
Na Askofu Kalikawe Bagonza:

UJINGA WANGU SASA UMEKOMAA

Niliamini UHAINI ni kosa kubwa. Neno lenyewe tu, linaogopesha kulisoma, kuliandika na kulitamka. Ni kitendo cha kutaka au kupindua serikali yoyote (halali au haramu).

Sasa kuna mtu mmoja katuhumiwa kutaka kutufanyia hayo. Huyu atakuwa ni mtu mbaya sana. Kwa nini atuhumiwe yeye kwa kosa hili baya? Nikawaza;

1. Kesi yake ingesikilizwa wazi (uwanja wa Taifa maana Kisutu hapatoshi).

2. Pale uwanjani wangeweka vipaza sauti na televisheni zote zirushe mubashara ili watu wote waone.

3. Makarandinga ya polisi yangesomba wote wasio na nauli kwenda kusikiliza kesi.

4. Asasi za kiraia na kianaharakati wangetoa maji ya kunywa bure kwa waliofika kusikiliza.

5. Posho za watumishi wa mahakama zingeongezwa ili kuwatia moyo wakati wa usikilizaji.

6. Siku ya hukumu ingekuwa siku ya mapumziko ili nchi itulie na kusikiliza hukumu hiyo.

Kwa nini nafikiri hivi?

a) Ingetoa fundisho la wazi kwa watu wote wanaopenda kuchezea amani ya nchi yetu.

b) Elimu ya uraia na utii wa sheria bila shuruti ingetolewa kwa vitendo kupitia kesi hii.

c) Hatua hii ingehamasisha watu wengi zaidi kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu bila kuhofia Polisi kuvuruga uchaguzi huo.

d) Wale wenye “mdomomdomo” kama mimi, wanaopenda kutumia neno HAKI kuliko amani, wangekuwa wamefungwa goli la kisigino na timu AMANI isiyopenda kutamka neno haki.

e) Hatua hii, ingeua kabisa kampeini za za NO REFORMS, NO ELECTION kwa sababu utawala wa sheria ungeonekana wazi.

f) Chama kingepata fursa nzuri ya kuonyesha ushahidi jinsi mabeberu wanapandikiza wahaini katika siasa zetu.

SASA, nimegundua ujinga wangu umekomaa. Kumbe kesi hii ni muhimu na nyeti. Haiwezi kuwa wazi. Ni kwa ajili ya wanasheria na wateule wachache wenye vifurushi kwenye simu.

Nilidhani nchi hii ni yetu wote kumbe ya wana sheria tu na polisi. Hata serikali iliyotaka “kupinduliwa” ni yetu au ya wana sheria na polisi?

Kama ni yetu wananchi, kwa nini hairuhusiwi watu kwenda mahakamani kusikiliza?

Aisee ujinga wangu una gharama. Akili zimeisha kichwani. Nimebakiza za kunipeleka msalani.

Wajinga wengine kama mimi wameenda wakaishia kuvunjwa viuno, mikono, na migongo.

Hili giza la kuona haki ikitendeka haliwezi kutuacha salama.

Nawaombea uponyaji walioumizwa.
Nawaombea waliowaumiza ili wao wasiumizwe maishani maana inauma.

Vitendo hivi vimelaaniwa vya kutosha. Nafasi za kulaani zimejaa. Nitalaani kesho.
 
Back
Top Bottom