Rais Samia awasili nchini Msumbiji

Rais Samia awasili nchini Msumbiji

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili Jamhuri ya Msumbiji 24 Juni 2025 ambapo anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Jamhuri ya Msumbiji, kufuatia mwaliko maalum wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Daniel Francisco Chapo. Sherehe hizo zinafanyika leo katika Uwanja wa Machava, Mjini Maputo.

Mwaliko huo Kidiplomasia na ushawishi wa nchi nje ya mipaka ya Tanzania, unaonyesha kukubalika kwa Rais Samia na pia kukua kwa diplomasia ya Tanzania mpaka kupewa mwaliko maalum wa kuwa mgeni rasmi wakati nchi nyingine inapoadhimisha sherehe zake za Uhuru. Msumbiji ni taifa kubwa ambalo lina historia kubwa sana Afrika na Duniani, katika ma-rais wote na wageni wote walioalikwa Msumbiji kuchaguliwa Rais Samia kuwa mgeni rasmi kunaonyesha kukubalika kwake katika nchi nyingine lakini pia mchango wake unatambulika hata nje ya mipaka ya Tanzania.

Katika historia ya Tanzania, akiwa Rais mwanamke wa Kwanza, anakuwa pia Rais ambaye amepata mwaliko maalum wa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya uhuru ya nchi nyingine. Imezoeleka kwenda kuhudhuria na sio kuwa mgeni rasmi, lakini mara hii ni heshima kubwa sana kwa nchi, kupitia Rais Samia kupata mwaliko rasmi wa kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Uhuru wa nchi nyingine.

View: https://www.youtube.com/watch?v=H9qBbUi1b5k

1750834314119.png

1750834484965.png

1750834522754.png

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka taji la maua kwenye mnara wa kumbukumbu wa Mashujaa Mjini Maputo ikiwa sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Jamhuri ya Msumbiji, tarehe 25 Juni 2025.​
1750854329834.png
 
25 June 2025
Machava Stadium
Maputo, Mozambique

Rais Samia Hassan na viongozi wengine wa kitaifa wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa taifa.​

Paulino Kicheki 2025-06-20

Mais de 40 mil pessoas esperadas nas celebrações dos 50 anos da independência nacional (de Mozambique)​

View: https://m.youtube.com/watch?v=SinbSdz5sW4
Zaidi ya watu 40,000 wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Msumbiji.
Maputo, Juni 20 (AIM) – Uwanja wa Machava wa hadithi unajiandaa kuwakaribisha, Jumatano ijayo, karibu watu elfu 40 kwa ajili ya sherehe za tarehe 25 Juni, ambazo zinaadhimisha miaka 50 ya uhuru wa kitaifa, uliotangazwa tarehe 25 Juni 1975.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu sherehe hizo, Waziri wa Nchi Tawala na Utumishi wa Umma, Inocêncio Impissa, amewahakikishia kuwa maazimisho ya leo ni makubwa zaidi kwa mwaka huu iliyoandaliwa na Serikali.

"Tunatarajia kukaribisha karibu watu 40,000 hapa na tayari tumewaalika wakuu wa nchi 36 na marais wa zamani.

Katika suala la uhamasishaji, tunafanya kazi ili kuhakikisha kwamba wananchi wengi wa Msumbiji wanashiriki," alisema Impissa, ambaye pia ni msemaji wa serikali.

Impissa alikumbusha matukio mengine sambamba na kuhusishwa na sherehe za miaka 50, ambayo ni sherehe iliyofanyika siku chache zilizopita katika wilaya ya Mueda, jimbo la Cabo Delgado, ikiongozwa na Mkuu wa Nchi, Daniel Chapo kwa ajili ya kumbukumbu ya wanaume, wanawake na watoto waliouawa katika Mauaji ya Mueda, kitendo cha kinyama kilichofanywa na utawala wa kikoloni wa Ureno.

Pia alikumbushia sherehe za kuzindua mwenge wa umoja wa kitaifa katika wilaya ya Nangade, katika jimbo hilo hilo, uliopita katika majimbo tisa ya nchi hiyo na leo umewasili katika jimbo la Maputo kupitia lango la kuingilia katika mji wa Incoluane wilayani Macia
 
Historia inaonesha Tanzania imetoa mchango mkubwa kwa uhuru wa Mozambique na mataifa mengine ya Kusini mwa Afrika kama Zimbabwe, Angola, South Africa na Namibia

Miaka 50 ya Uhuru wa Frelimo kumekuwepo na changamoto nyingi.

Mwaka jana kulikuwepo, mgawanyiko mkubwa kufuatia uchaguzi mkuu wa Oktoba 2024 ambapo Wapinzani hawakufurahia mchakato mzima kuelekea uchaguzi na pia uchaguzi wenyewe ulivyosimamiwa na Tume ya Uchaguzi na matokeo yaliyotangazwa.

Ikabidi matokeo hayo ya uchaguzi mkuu wa nchi na wa majimbo kupitiwa upya na Mahakama Maalum ya Uchaguzi ndipo rais Daniel Chapo alipotangazwa kuwa mshindi kwa tiketi ya chama kongwe dola cha FRELIMO chama rafiki cha chama kongwe CCM cha nchini Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili Jamhuri ya Msumbiji 24 Juni 2025 ambapo anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Jamhuri ya Msumbiji, kufuatia mwaliko maalum wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Daniel Francisco Chapo. Sherehe hizo zinafanyika leo katika Uwanja wa Machava, Mjini Maputo.

Mwaliko huo Kidiplomasia na ushawishi wa nchi nje ya mipaka ya Tanzania, unaonyesha kukubalika kwa Rais Samia na pia kukua kwa diplomasia ya Tanzania mpaka kupewa mwaliko maalum wa kuwa mgeni rasmi wakati nchi nyingine inapoadhimisha sherehe zake za Uhuru. Msumbiji ni taifa kubwa ambalo lina historia kubwa sana Afrika na Duniani, katika ma-rais wote na wageni wote walioalikwa Msumbiji kuchaguliwa Rais Samia kuwa mgeni rasmi kunaonyesha kukubalika kwake katika nchi nyingine lakini pia mchango wake unatambulika hata nje ya mipaka ya Tanzania.

Katika historia ya Tanzania, akiwa Rais mwanamke wa Kwanza, anakuwa pia Rais ambaye amepata mwaliko maalum wa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya uhuru ya nchi nyingine. Imezoeleka kwenda kuhudhuria na sio kuwa mgeni rasmi, lakini mara hii ni heshima kubwa sana kwa nchi, kupitia Rais Samia kupata mwaliko rasmi wa kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Uhuru wa nchi nyingine.

View: https://www.youtube.com/watch?v=H9qBbUi1b5k

Unaingilia majukumu ya Lucas Mwashambwa
 
Ukoloni ni unyama. (voice of Samora Machel)

MAPAMBANO YANAENDELEA (STRUGGLE) ALUTA CONTINUA DHIDI YA WALIOHODHI MADARAKA BAADA YA 'UHURU'

Samora Machel : Ukoloni wa kiFikra, Ukoloni Hauna Rangi

View: https://m.youtube.com/watch?v=Omh25kcA1Lw

Katika hotuba yake motomoto kuhusu kutawaliwa, alihoji vipi mwafrika aliyetawaliwa na mfaransa akajiona m-bora kuliko mwingine kwa kuwa Ufaransa wana tamaduni bora zaidi ya uandishi wa mistari ya mashairi ya mapendo kwa umahiri wa kisomi.

Samora Machel anazidi kuwaza hata wale waliotawaliwa na muingereza wajiona wao ni bora kwa vile Uingereza ilitawala nchi nyingi zaidi na inasemekana ni wazungu 'wastaarabu' zaidi.

Samora Machel anatuasa ingawa Portugal ni nchi masikini zaidi ktk ulaya lakini ni nchi iliyoendekeza ukoloni kama Ufaransa, Uingereza na Ureno / Portugal na sifa za nchi zote hizo za ulaya ni kuwa ziliendekeza ukoloni.

Samora Machel anapigia mstari neno ukoloni na kuwa ukoloni ni unyama hauna utu hivyo kujisifia wewe ni zao la ukoloni huu au ule wenye hadhi ya juu ni kukosa fikra sahihi.

Hivyo maneno ya Samora Machel anasisitiza tuamke na kuwa mapambano lazima yaendelee (2022) dhidi ya ukabila, ujinga, maradhi, njaa, ushirikina na mawazo potofu ya kukumbatia ukoloni wa aina yoyote.

Samora Machel anakumbushia kuwa Mozambique walipambana na ukoloni mkongwe wa miaka 500 wa Mreno uliokuwapo Mozambique, na kama kawaida pamoja na umasikini wa taifa la Portugal barani ulaya,lakini walikuwa wakoloni kama wakoloni wengine.

Anamalizia kuwa ukoloni wowote hauna usafi wa kujivunia kwani ni Ukoloni unaogandamiza jamii zingine na kuzigawanisha.

N.B
Kiongozi wa kwanza wa Mozambique alikuwa rais Samora Moises Machel aliyekuwa kiongozi wa chama kilichoongoza mapambano cha FRELIMO dhidi ya utawala mkongwe wa Ureno uliodumu miaka 500.

FRELIMO ilikuwa na makao yake makuu jijini Dar es Salaam na kambi za wapiganaji huko Kongwa Dodoma na pia FARM 17 mkoani Mtwara nchini Tanzania ambapo wapiganaji wa FRELIMO walijipenyeza kuanza mapambano ya kuungoa utawala mkongwe wa Mreno kwa kuanzia mkoa wa Capo Delgado kaskazini ya Msumbiji

Samora Moises Machel kiongozi mcheshi (charismatic), hotuba zake za hasama hadi leo kizazi hiki zinasilizwa kwa kuwa zililenga kuwa na mtu huru kifikra. Moja ya hotuba yake motomoto hapo juu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili Jamhuri ya Msumbiji 24 Juni 2025 ambapo anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Jamhuri ya Msumbiji, kufuatia mwaliko maalum wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Daniel Francisco Chapo. Sherehe hizo zinafanyika leo katika Uwanja wa Machava, Mjini Maputo.

Mwaliko huo Kidiplomasia na ushawishi wa nchi nje ya mipaka ya Tanzania, unaonyesha kukubalika kwa Rais Samia na pia kukua kwa diplomasia ya Tanzania mpaka kupewa mwaliko maalum wa kuwa mgeni rasmi wakati nchi nyingine inapoadhimisha sherehe zake za Uhuru. Msumbiji ni taifa kubwa ambalo lina historia kubwa sana Afrika na Duniani, katika ma-rais wote na wageni wote walioalikwa Msumbiji kuchaguliwa Rais Samia kuwa mgeni rasmi kunaonyesha kukubalika kwake katika nchi nyingine lakini pia mchango wake unatambulika hata nje ya mipaka ya Tanzania.

Katika historia ya Tanzania, akiwa Rais mwanamke wa Kwanza, anakuwa pia Rais ambaye amepata mwaliko maalum wa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya uhuru ya nchi nyingine. Imezoeleka kwenda kuhudhuria na sio kuwa mgeni rasmi, lakini mara hii ni heshima kubwa sana kwa nchi, kupitia Rais Samia kupata mwaliko rasmi wa kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Uhuru wa nchi nyingine.

View: https://www.youtube.com/watch?v=H9qBbUi1b5k

Tunashukuru kaenda karibu nadhani sio mbaya tuende
 
Back
Top Bottom