Rais Samia awapa Coaster mpya shule ya wasichana Lindi, atoa onyo kali kwa watakao litumia kwa sendoff na kitchen party

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Rais samia mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,nuru ya wanyonge, komandoo wa vita, simba wa nyika, nyota ya matumaini,mama wa upendo na ukarimu,mwamba wa siasa ,mzalendo wa kweli Anaendelea kuleta Tabasamu, furaha na matumaini katika mioyo ya wengi.

Leo Rais wetu amekabidhi gari mpya aina ya Coaster kwa shule ya wasichana lindi,ambapo gari hilo limekabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Lindi ili alipeleke shuleni hapo kutimiza ahadi ambayo aliwaahidi wakati alipotembelea shuleni hapo.

Lakini pia katika maelekezo yake jemedari wetu Rais mama Samia Suluhu Hasssan ameelekeza gari hilo litumiwe na wanafunzi pamoja na walimu wao lakini pia akatoa onyo kali kutokuona gari hilo likigeuzwa na kuanza kutumiwa katika sherehe za sendoff pamoja na kitchen party jambo ambalo siyo malengo wala makusudio ya kutoa na kuwapelekea gari hilo.

Kwa hakika hakuna mahali ambapo utakwenda katika Taifa hili usikute alama za Rais Samia.kateka kila eneo na kuweka mikono yake kila sehemu, ni mama wa huruma ni mama wa upendo, ni mama mwenye ukarimu,ni mama msikivu na ni mama wa Taifa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu,.

0742-676627.
 
Hongera mama kwakutambua watoto wanahitaji coaster ili wafaulu
Ni kwa ajili ya kurahisisha usafiri na kuwasaidia wakitaka kwenda sehemu kwa ajili ya shughuli za masomo na kujifunza nje ya shule yao.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais samia mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,nuru ya wanyonge, komandoo wa vita, simba wa nyika, nyota ya matumaini,mama wa upendo na ukarimu,mwamba wa siasa ,mzalendo wa kweli Anaendelea kuleta Tabasamu, furaha na matumaini katika mioyo ya wengi.

Leo Rais wetu amekabidhi gari mpya aina ya Coaster kwa shule ya wasichana lindi,ambapo gari hilo limekabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Lindi ili alipeleke shuleni hapo kutimiza ahadi ambayo aliwaahidi wakati alipotembelea shuleni hapo.

Lakini pia katika maelekezo yake jemedari wetu Rais mama Samia Suluhu Hasssan ameelekeza gari hilo litumiwe na wanafunzi pamoja na walimu wao lakini pia akatoa onyo kali kutokuona gari hilo likigeuzwa na kuanza kutumiwa katika sherehe za sendoff pamoja na kitchen party jambo ambalo siyo malengo wala makusudio ya kutoa na kuwapelekea gari hilo.

Kwa hakika hakuna mahali ambapo utakwenda katika Taifa hili usikute alama za Rais Samia.kateka kila eneo na kuweka mikono yake kila sehemu, ni mama wa huruma ni mama wa upendo, ni mama mwenye ukarimu,ni mama msikivu na ni mama wa Taifa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu,.

0742-676627.
Kutoa ni moyo!
 
ni wajibu wake Tena Kwa pesa zetu... sema kaza kuna mkeka unatoka siku sio nyiingi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom