Rais Samia awabadili Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman na Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Kattanga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya nafasi za viongozi Serikalini Ikulu jijini Dares Salaam, leo tarehe 03 Januari, 2023.

Amesema “Mtakumbuka kuwa Novemba 2022, Bunge la Tanzania lilikuwa na mjadala mzito kidogo kuhusu matumizi ya fedha na madaraka katika ofisi zetu za Kibalozi zilizopo Nchi mbalimbali, Serikali inafanyia kazi kasoro zilizoelezwa ili kurudisha hadhi ya balozi zetu.

“Nimefanya mabadili katika ofisi ya Ubalozi iliyopo New York, ambayo inakuwa na Mwakilishi wetu wa kudumu katika Umoja wa Mataifa.

“Ofisi hii ni muhimu kwa Nchi yetu kwa kuwa ndio inatuwakilisha katika mambo yanayojadiliwa na mataifa na taasisi za kimataifa zilizo chini ya Umoja wa Mataifa Mjini New York.

“Ofisi yetu hiyo inahitaji mwanadiplomasia mahiri anayejua siasa za kimataifa, mzalendo kwa nchi yake na mtulivu wa hekima na busara.

“Hivyo nimeamua kumrudisha nyumbani Prof. Kennedy Gaston aliyeko Ofisi ya New York na kumpeleka Hussein Othman Kattanga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

“Kattanga anaenda kuiwakilisha Tanzania kama Balozi wa Kudumu huko New York.

“Nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi itajazwa na DKT. Moses Mpogole Kusiluka aliyekuwa Katibu Mkuu Ikulu.

“Nafasi ya Katibu Mkuu Ikulu itajazwa na Diwani Athuman Msuya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS)

“Nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa itajazwa na Said Hussein Massoro aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Shughuli za ndani za TISS.”


 
Back
Top Bottom