Abuu Ibraahiym Sibomana
Senior Member
- Jun 1, 2025
- 130
- 114
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa rais wa Kenya ,familia ya Odinga na wananchi wa Kenya kufuatia kifo cha waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga.
Kupitia taarifa ambayo rais Samia ameiweka kwenye mitandao ya kijamii ameeleza kuwa kapokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Odinga.
" Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Raila Amolo Odinga. Tumempoteza kiongozi mahiri, Mwanamajumui wa Afrika, mpenda amani na mtafuta suluhu, ambaye ushawishi na upendo wake haukuwa tu ndani ya Kenya, bali Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Msiba huu si wa Kenya pekee, bali wetu sote."
" Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt. William Samoei Ruto, Mama Ida Odinga, watoto, familia, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Kenya kwa msiba huu".
Mheshimiwa Dkt.Samia katika salamu hizo za pole amewaombea familia ya Odinga na wakenya wote wapate subra,faraja na imani katika kipindi hiki.