Mkuu heshima kwako, Ila nakushauri ongeza bidii kwa kile unafanya. Serikali haitakuletea ugali mezani(ukweli mchungu)
Fanya kazi kwa bidii sana, kila siku buni vitu vipya punguza masaa ya kulala. Hizi kelele za humu kuwa pesa hakuna Wala usizitilie Sana maanani
Mkuu mimi naangalia mzunguko wa hela ulivyo wakati wa JK na MEKO ndio nafanya comparison!
1.Wakati wa JK ukitangaza kuuza kiwanja haipiti wiki mbili ushakiuza ila kwa NGOSHA unaweza ukagonga hadi miezi 6 hakuna hata mtu wa kuuliza.
2. Waati wa JK ukijenga fremu hata kabla ya kumaliza upo kwenye foundation wafanyabiashara washakuja kuzibook zote na kulipia kodi ya mwaka mzima.
3. Enzi za JK nyumba sinza,mikocheni,mbezi beach ulikuwa hauwezi kupata maana zilikuwa full ila kwasasa mabango ya nyumba inapangishwa yapo kibao.
4.Enzi za JK ulikuwa hauwezi kukuta office for rent kwenye prime areas,ila sasa Majengo kibao yameandikwa office for rent,ina maana wafanyabisahra wengi wamekimbia na kuhamisha bizness zao sehemu nyingine na wengine wamefunga.
5.Enzi za JK Bar zilikuwa zinajaa watu wa kutosha ,supermarket ukienda watu kama wote unapanga foleni kibao kupata huduma,ukienda bank foleni ya mufa mtu ila sasa aibu.
Kwakifupi pesa imepungua kwenye mzunguko ,wewe shukuru kwamba upo kwenye chain ya wapigaji wa MEKO ambao walikuwa wanatumia fedha zao kukuunga mkono kwenye Hardware yako hiyo.