mambo ya kijinga huwa yanapenda kushikilia vichwa zaidi kuliko yenye tija.
Tugusie bajeti,
mie najikita katika faini za waendesha pikipiki na bajaji, kiufupi naona hizo faini ka hazijasaidia kitu na pili waendesha bodaboda wanajua sheria za barabarani na vyombo vya moto kiujumla ila wengi wanakiuka makusudi, mfano kuambiwa wasipakize mishikaki na wao wanapakiza, yani hilo la mishkaki hata mtoto wa miaka 12 anajua kuwa haitakiwi
Pili swala la kofia ngumu, kila dereva wa pikipiki anajua kuwa inampasa yeye na abiria wake kuvaa hiyo kufia ngumu ila hawavai kwasababu mbalimbali ila zaidi ya 90% ya hizo sababu zao hazina mashiko.
Swala la usalama kwa mtu mmoja mmoja na jamii nzima halihitaji mbwembwe ama siasa flani maana yale ni maisha ya mtu, kitendo cha kushusha hizo adhabu mie sioni kama itawasaidia ila itawafanya waone adhabu hiyo ni ndogo ambako kutawafanya wawe wazembe zaidi ambako kutakuwa na madhara zaidi.
Kitendo cha dereva wa pikipiki kuona adhabu ka ni ndogo na anaimudu kunaweza fanya wale wenye uelewa mdogo kuona ka ndo muda wa kufanya vile waonavyo inafaa kwao