MoureenAbel
Member
- Sep 24, 2021
- 29
- 43
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 14 Januari, 2022 amepokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Évariste Ndayishimiye uliowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum ambaye ni Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni wa Burundi Mhe. Ezechiel Nibigira, Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.
Mhe. Nibigira amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kukubali kupokea Ujumbe huo Maalum na kufikisha salamu kutoka kwa Mhe. Rais Ndayishimiye na kumjulisha kuwa hali ya Burundi ni salama na tulivu, hivyo kupelekea wananchi wake kuendelea na shuguli mbalimbali za kujiletea maendeleo.
Amesema Mhe. Rais Ndayishimiye amemtuma kufikisha ujumbe huo wenye lengo la kukuza zaidi uhusiano kati ya Tanzania na Burundi katika masuala ya kiuchumi.