kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 122
- 241
Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Wizara ya Kilimo wameamua kubadilisha sekta ya kilimo kutoka kilimo cha kwenye karatasi kwenda kwenye utekelezaji. Katika hotuba zake za hivi karibuni Rais Samia alisema kilimo kina hela vijana wakajiajiri kwenye kilimo.
Ili kuhakikisha vijana wanajiajiri kwenye kilimo, Serikali imeanzisha programu ya mashamba ya pamoja ya umwagiliaji. Shamba la kwanza limezinduliwa katika vijiji vya Mlanzo na Ndogoe Wilayani Chamwino, Shamba hilo lina ukubwa wa ekari 11,453.
Shamba la pili liko Bahi lina ukubwa wa ekari 3,560 maalum kwa kilimo cha ngano na shamba la tatu lina ekari 8,000 lipo katika Wilaya ya Chamwino. Katika mashamba hayo kutakua na eneo maalum la makazi ya vijana watakaoshiriki kwenye shughuli za kilimo pamoja na ufugaji.
Wataalam wa udongo tayari wameanza kazi ya kupima udongo ili kujua aina ya mazao yatakayolimwa lakini pia Wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) wakishirikiana na Mamlaka ya Maji safi na Majitaka wako site kutekeleza uchimbaji wa visima na mabwawa ya umwagiliaji.