Rais Samia anaonekana si mtu wa kujisifu; shida kuna walakini kwenye usimamizi wa fedha za umma

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Jambo la kuweza kumsifia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan inaonesha dhahiri ni mpole sana na ni rais asiyependa makuu kwa viongozi wa chini yake anaowaongoza hili kwa kifupi yeye linampa heshima kubwa kwa kusifu na kuabudiwa kuwa anaupiga mwingi huku wahuni wakila kulingana na urefu wa kamaba yao.

Juzi ametoa kauli yenye utata mkubwa akisema kwamba kiongozi yeyote atakayeharibu katika serikali yake hatamfukuza bali atasubiri aone anaharibu zaidi ya mara tatu ndiyo amfukuze. Hii kauli imeleta mashaka makubwa kwani viongozi hao huenda wakafuja fedha za umma na adhabu zao zikawa kufukuzwa kazi huku huko waendapo wakienda kutafuna mamilioni waliyoyakwapua.

Kitu kingine dhana ya kusubiri kiongozi aharibu mara tatu naona si dhana njema katika uongozi ingawa rais wetu ana huruma kupita kiasi kuna kila sababu za kubadilika kifikra na kimtazamo wa kuongoza watu wake wa chini, huku choni watu wanalia sana bei ya bidhaa kupanda na vifaa vya ujenzi yeye amejikalia kimya.

Na anaambiwa anaupiga mwingi na siyo mtu wa ma kamera na television kama mtangulizi, kwa maoni yangu umma kujua kodi zao zinatumikaje siyo dhambi. Tunataka tujue nini anafanya kila siku tujue pesa zinaenda wapi maana tunaona kama miundo mbinu ya barabara imepigwa kapuni zaidi ya kuona hizi za changarawe ambazo na zenyewe zinajengwa chini ya kiwango.

Kama ujenzi wa madarasa walitangaza basi na miradi mingine tangazeni tupate ukweli yanayoendelea kama mmelipa fedha kwa wakandarasi kwa miradi mnayoendeleza basi umma ujue, hii ya kimya kimya inaleta sintofahamu kwenye matumizi ya fedha za umma.
 
Back
Top Bottom