Megalodon
JF-Expert Member
- Apr 9, 2021
- 2,199
- 3,871
Kwa mara ya kwanza najaribu kumuelewa Mama Rais Samia, Sikubaliani nae kwa mambo mengi ikiwemo hilo la kumnanga JPM, lakini hili la kuchungulia wataalam kutoka private sector hasa USAID, ameonesha usikivu na Intelligence kama kiongozi.
Sio kazi ndogo kuwa Country Director chini ya wazungu, Huyu Bw. Mfamasia, na amesomea mambo ya Famasi kwenye Masters yake pamoja na mambo ya Purchasing.
Haiwezekani Bohari ya Dawa ambayo ndiyo key player wa dawa Tanzania kwa wananchi iongozwe na mtu tofauti na Mtaalam wa dawa ambao kazi yao ni kusomea dawa tu kuanzia production mpaka inaingia kwenye mwili wa binadamu, ni mambo ya hovyo na haya mambo ni Tanzania tu.
Matokeo yake CAG akihoji kwanini dawa zinakufa za Bil 20, majibu huwa ni ya kisiasa na ujinga ujinga.
Sasa huyu Bw. Mfamasia akafanye kazi na atupe majibu kwanini serikali inatumia hela nyingi na dawa nyingi zinakufa, yeye si ndio mfamasia , na ndio CEO , ang’amue na aje na majibu ili kama anahitaji msaada kutoka Serikali kuu asaidiwe.
Kumbe tunawataalam waliobobea kwenye Dawa na Corporate Management ... halafu tunawaacha watumike na wazungu kwenye NGOs, kwenye taasisi zetu tunaweka wanajeshi wasio kuwa na skills. Taasisi inaendeshwa kitapeli na kibabe bila ya kuheshimu sheria za Umma huku tunawataalam wa kutosha: aliyeiroga Tanzania nae alishakufa.
Kwa Uteuzi huu Mama unatakiwa kuangalia Hata Wakurugenzi wa Tanesco wawe ni watu waliosomea na kuspecialize kwenye mambo ya Energy na wawe pia na
Corporate skills.
Lakini Ali Tukai alone hatoweza, atahitaji kushirikiana na wataalam wa logistic MSD , watu wa mifumo na data base, Corporate services, wataalam wa fedha ili wamshauri matumizi ya Fedha za taasisi.
Naanza kumuelewa Mama taratibu, huyu Mama ana dira, ana patience and the most important ana exposure and she is a good listener. tumpe support ili 2025 awe Rais wetu tena.
Ukiwa kama Mtanzania chanya, nini Ushauri wako ? kwa Ali Tukai kama CEO mpya wa MSD.
Maendeleo Hayana Uchama, Nasema Uongo Ndugu Zangu ?