Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Leo Machi 27, 2025 majira ya saa 5:00 asubuhi Rais Samia Suluhu Hassan atapokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ya mwaka 2023/2024 Ikulu Dar es Salam.
TUJIKUMBUSHE ALICHOSEMA RAIS SAMIA BAADA YA KUPOKEA REPOTI YA 2022/2023
Taasisi zilizopata hati zenye shaka na hati mbaya ni pamoja na Kiwanda cha Dawa Keko, Bodi ya Chai Tanzania, Chuo cha Sukari cha Taifa na Shirika la Posta Tanzania haya ni mashirika ya umma, amesema Kichere.
Katika upande wa miradi ya maendeleo, ameitaja Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru, Mfuko wa Afya pia zilipata hati mbaya
Mwaka 2007 mfuko wa taifa hifadhi ya jamii, wa sekta binafsi, ulitoa mkopo wa Bilioni 15.91 kwa Halmashauri la Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Machinga Complex, hadi kufikia Juni 2024 mkopo na riba imefikia bilioni 27.61 lakini halmashauri ilikuwa imerejesha Milioni 80 tu tangu mwaka 2009
Mashirika ya Umma yanayojiendesha kibiashara yaliyopata faida. Mwaka 2023/24, TPDC imepata faida ya Tsh. Bilioni 248.75, NHC imepata faida ya Tsh. Bilioni 242.9 na TPA imepata faida ya Tsh. Bilioni 140.8
Katika kipindi hicho hicho cha mwaka wa fedha 2023/24, mashirika kadhaa yaliendelea kupata hasara jambo linaloashiria uwepo wa changamoto za kiutendaji wa kiuongozi.
TUJIKUMBUSHE ALICHOSEMA RAIS SAMIA BAADA YA KUPOKEA REPOTI YA 2022/2023
Machi 28, 2024 Ikulu Chamwino jijini Dodoma, wakati akipokea Ripoti ya Rais Samia, alisema Serikali itafanyia kazi mambo yaliyoibuliwa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Alisema, ripoti hizo zinazosomwa kila mwaka zinachangia kuimarika kwa utendaji ndani ya serikali na mashirika ya umma. “Kuna dosari zilizotolewa hapa tutaenda kuzifanyia kazi kisawasawa turekebishe na mwakani pengine hizi hazitajirudia tutakuwa tumesogea,” amesema
Moja ya tukio kubwa katika ripoti zilizosomwa mwaka jana ni pamoja na CAG kuwasilisha ripoti ya ukaguzi iliyoonesha mashirika 8 ya umma yalikusanya mapato ya shilingi bilioni 23.27 kinyume na utaratibu.
Pia soma: CAG Kichere: Licha ya kupewa Ruzuku ya Tsh. Bilioni 31.55, ATCL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 56.64, ongezeko la 61% kutoka hasara ya Mwaka 2021/22
Fuatilia kwa Updates zaidi......

MDHIBITI NA MKAGUZI MKUUU WA HESABU ZA SERIKALI, CHARLES KICHERE
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameeleza kuwa hadi kufikia tarehe 30 Juni 2024, deni la serikali lilifikia shilingi trilioni 97.35. Hii ni ongezeko kutoka trilioni 82.25 lililoripotiwa katika mwaka wa fedha wa 2022/23, ikiwa ni tofauti ya trilioni 15.1 sawa na ongezeko la asilimia 18.36.
Taasisi zilizopata hati zenye shaka na hati mbaya ni pamoja na Kiwanda cha Dawa Keko, Bodi ya Chai Tanzania, Chuo cha Sukari cha Taifa na Shirika la Posta Tanzania haya ni mashirika ya umma, amesema Kichere.
Katika upande wa miradi ya maendeleo, ameitaja Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru, Mfuko wa Afya pia zilipata hati mbaya
Mwaka 2007 mfuko wa taifa hifadhi ya jamii, wa sekta binafsi, ulitoa mkopo wa Bilioni 15.91 kwa Halmashauri la Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Machinga Complex, hadi kufikia Juni 2024 mkopo na riba imefikia bilioni 27.61 lakini halmashauri ilikuwa imerejesha Milioni 80 tu tangu mwaka 2009
Mashirika ya Umma yanayojiendesha kibiashara yaliyopata faida. Mwaka 2023/24, TPDC imepata faida ya Tsh. Bilioni 248.75, NHC imepata faida ya Tsh. Bilioni 242.9 na TPA imepata faida ya Tsh. Bilioni 140.8
Katika kipindi hicho hicho cha mwaka wa fedha 2023/24, mashirika kadhaa yaliendelea kupata hasara jambo linaloashiria uwepo wa changamoto za kiutendaji wa kiuongozi.
- Shirika la Reli Tanzania lilipata hasara ya Tsh. Bilioni 224 ikilinganishwa na Tsh. Bilioni 102.
- Kampuni ya Ndege Tanzania ilipata hasara ya Tsh. Bilioni 91.8 ikiwa ni ongezeko la asilimia 62% kutoka kutoka Tsh. Bilioni 56.6 mwaka uliopita.
- Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ilipata hasara ya Tsh. Bilioni 27.78 mwaka wa fedha 2023/24 ongezeko hili ni kutoka Tsh. Bilioni 4.32 ya hasara kwa mwaka uliopita.
- Shirika la Posta Tanzania (TPC) lilipata hasara ya Tsh. Bilioni 23.63 ikilinganishwa na Tsh. Bilioni 1.34 mwaka uliopita.
- Kampuni ya Kutengeneza Nguzo za Zege Tanzania (Kampuni Tanzu ya TANESCO) iliyoanzishwa kwa lengo la lengo la kutengeneza Nguzo za Zege imebainika kuwa kampuni hiyo haijatekeleza jukumu hilo la msingi ipasavyo ambapo hadi kufikia mwaka wa fedha 2023/24 kampuni ilipokea Tsh. Bilioni 6 kutoka TANESCO ambapo Tsh. Bilioni 4 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda na Maabara ya kupima ubora wa Nguzo na Tsh. Bilioni 2 kwa ajili ya gharama za uendeshaji. Licha ya mipango hiyo fedha nyingi zilitumika kulipa gharama za kawaida na kulipa wazabuni wa nje wanaotengeneza Nguo badala ya Kampuni yenyewe kufanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake kampuni bado haijaanzisha uzalishaji wa Nguzo wala kuwa na Maabara yake ya ndani.
- Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linadaiwa jumla ya shilingi bilioni 238 na kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL). Kati ya kiasi hicho, bilioni 111 ni deni la msingi, huku bilioni 127 zikiwa ni riba.