Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,519
- 41,030
Matatizo mengi ya Tanzania, kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na uongozi mbaya unaolindwa na sheria mbaya na Katiba mbovu.
Rais Samia, kwa dhamira yake, anaonekana ni mtu anayependa haki - hili amelitamka mara kadhaa.
Rais Samia anapenda demokrasia ya vyama vingi - hili alilitamka hata kule Nairobi aliposema, 'Nawapongeza Wakenya kwa demokrasia na namna bunge linavyojadili mambo mbalimbali kwa uhutu. Huwa napenda kuangalia Bunge la Kenya".
Rais Samia anaamini katika uchumi wa kisasa - ameliongea sana hili alipokemei TRA kwa primitivity katika ukasanyaji kodi.
Kwenye katiba mpya, alisema, hili lisubiri kwanza lakini hakusema moja kwa moja kuwa hatashughulikia.
Agenda kubwa za siasa za upinzani ni:
Katiba nzuri na bora
Haki za wananchi
Uhuru wa kujieleza na maoni
Uhuru wa vyombo vya habari
Sera rafiki za kodi
Sera rafiki za uwekezaji, biashara na uchumi kwa ujumla.
Kama Rais Samia akayatekeleza hayo yote, kama anavyoonekana kufanya, wapinzani watakuwa na wakati mgumu wa kupata agenda ya uchaguzi 2025.
Mapungufu makubwa ya utawala wa Rais Samia, mpaka sasa, ni kwamba yale mambo yote ambayo Rais ameonekana kuyachukia, ametoa tu kauli lakini hajafanya chochote kwenye sheria zinaruhusu hayo maovu kutendeka. Akilifanya hilo, itakuwa ni furaha na faida kwa Watanzania wote wanaolipenda Taifa lao.
Rais Samia, ni Mama, akiyafanya hayo yote niliyoyataja kwa kuyawekea sheria, wagombea kutoka vyama pinzani, ambao uwezekano mkubwa watakuwa wanaume, itakuwa ni ngumu sana hata kutoa zile kauli kali kali dhidi ya huyu Mama, wapiga kura wanaweza wasikuelewe, hasa kama watatoa kauli za kumdhalilisha Mama ambaye atakuwa amefanya mema mengi.
Uchaguzi ujao, Mungu akitujalia uhai, tutarajie siasa za kistaarabu kwa kiwango ambacho hakijawahi kuwepo.