Rais Samia aidhinisha pesa kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara ya Lami kutoka Manyovu hadi Kakonko, kilometa 260+

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
Ni kama ndoto kwa wakazi wa Kigoma kilio cha muda mrefu kinaenda kuwa historia baada ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuidhinisha pesa kwa ajili wa Ujenzi wa Barabara ya Lami kutoka Manyovu hadi Kakonko zaidi ya kilometa 260. Ni kama Rais samia anasema sifa ya watu wa kigoma ibakie kuwa ubishi si Barabara za vumbi

Ulikuwa ni utaratibu wa kawaida kwa wakazi wa Kakonko kuogopa kusafiri na nguo safi wakihofia vumbi la njiani na Ubovu wa Barabara. Sasa hali hii inakwenda kuwa historia

Kama hiyo haitoshi Serikali ya Rais Samia imetoa Pesa kugharamia Ujenzi wa barabara kutoka Malagarasi-Ilunde-Uvinza kwa kiwango cha lami urefu wa takribani KM 51.1 utakaogarimu shilingi bilioni 62.5

Huu ni mwendelezo wa Serikali ya Rais Samia kuendelea kuufungua mkoa wa kigoma wenye fursa mbalimbali na kurahisha kuinua maisha ya wakazi wa Mkoa huu..
 
Labda anamaanisha ile ya Kasulu-Kibondo- Kakonko ambayo ndio inatengenezwa sasa hivi
Mbona hiii barabara ipoo, umetokaa nyakanazi, Hadi kibondo to kasulu, ukifika kasulu kabla hujafika mjini huku mwanzoni mwa Kijiji Cha kidyama, imechepukia hapoo, kuacha inayoendelea kasulu mjini kwenda kigoma, yenyewe inapandisha kuelekea mashamba ya Kijiji Cha kabangaa Hadi mlima uitwao lusunwe adi huko manyovu. Hii barabara itakapoisha haitakua na mfano wowotee hapa balani Africa Kwa viwango inavyojengwa.

Nani kama Samia?
 
Ni kama ndoto kwa wakazi wa Kigoma kilio cha muda mrefu kinaenda kuwa historia baada ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuidhinisha pesa kwa ajili wa Ujenzi wa Barabara ya Lami kutoka Manyovu hadi Kakonko zaidi ya kilometa 260. Ni kama Rais samia anasema sifa ya watu wa kigoma ibakie kuwa ubishi si Barabara za vumbi

Ulikuwa ni utaratibu wa kawaida kwa wakazi wa Kakonko kuogopa kusafiri na nguo safi wakihofia vumbi la njiani na Ubovu wa Barabara. Sasa hali hii inakwenda kuwa historia

Kama hiyo haitoshi Serikali ya Rais Samia imetoa Pesa kugharamia Ujenzi wa barabara kutoka Malagarasi-Ilunde-Uvinza kwa kiwango cha lami urefu wa takribani KM 51.1 utakaogarimu shilingi bilioni 62.5

Huu ni mwendelezo wa Serikali ya Rais Samia kuendelea kuufungua mkoa wa kigoma wenye fursa mbalimbali na kurahisha kuinua maisha ya wakazi wa Mkoa huu..
Manyovu to kakonko unaijua au unataka kumdanganya Rais?
 
Manka Musha/musa acha uongo hizo road zimeanza kujengwa kitambo, nilipita mwaka jana nilikuta greda zinachapa kazi, pia ile ya kutokea Kaliua kwenda uvinza nayo inakaribia kumalizika
 
Mnawatengenezea lami watu wa Kigoma alafu sisi tutacheka wapi? Tumeshazoea kama tuna huzuni tunaenda stand kuangalia abiria wa kigoma wanavyoshuka kwenye bus wameoga vumbi kama wanatoka kuzikwa
 
Siku ambayo ujenzi wa bara bara ya Kigoma - Tabora utakamilika, ndio utakuwa mwisho wa Dunia 😀😀😀
Ujenzi wa bara bara hii umechukua miaka 60 tangu nchi ipate uhuru.
Pengine huu ni ujenzi uliochukua muda mrefu kuliko ujenzi wowote hapa nchini...
 
Back
Top Bottom