Rais Samia ahitimisha ziara yake ya kiserikali nchini Angola

Rais Samia ahitimisha ziara yake ya kiserikali nchini Angola

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
RAIS SAMIA AHITIMISHA ZIARA YAKE YA KISERIKALI NCHINI ANGOLA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amehitimisha Ziara yake ya Kiserikali ya siku 3 nchini Angola.

Mapema leo asubuhi, Rais Dkt. Samia alitembelea kiwanda cha kusafisha mafuta cha Luanda Oil Refinery nchini humo.

Mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho, Rais Dkt. Samia amepokelewa na Waziri wa Madini, Mafuta na Gesi wa Jamhuri ya Angola, Mhe.Diamantino Pedro Azevedo ambae alimueleza Rais Dkt. Samia shughuli mbalimbali za kiwandani hapo ikiwemo uzalishaji na teknolojia inayotumika katika uzalishaji kiwandani hapo. Kiwanda cha Oil Refinery kina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Angola ambayo ni nchi ya pili kwa kuwa na hifadhi ya mafuta barani Afrika baada ya Nigeria.

Soma Pia: Rais Samia Suluhu Hassan, awasili jijini Luanda Angola kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu

Rais Dkt. Samia amehitimisha ziara yake kwa kuagana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Angola Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço katika Ikulu ya nchi hiyo na kurejea nyumbani Tanzania mapema jioni ya leo.

 
Raisi Samia kachuja sana😳 yaani hata machawa sasa topic zao ni kumchafua
lissu 😳😳🤦🏾‍♂️
 
NO REFORMS NO ELECTION
 
Wacha azurure, wachini yake wanapiga hela kufa!
Bure kabisa kabisa huyu rais..
 
Back
Top Bottom