Rais Samia ahani msiba wa Marehemu SACP, Zelothe Stephen

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,035
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima za mwisho kwenye Jeneza la Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Kamishna Mstaafu Marehemu Zelothe Stephen Zelothe wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2023




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia Kifo cha Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Kamishna Mstaafu Zelothe Stephen Zelothe Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Bi. Flora Zelothe Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Kamishna Mstaafu Marehemu Zelothe Stephen Zelothe wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2023
 
Hongo ya uongozi ndiyo inawafanya polisi wailinde CCM na kuwaonea wananchi wema.
 
Uteuzi wa Zelothe kuwa kiongozi wa CCM ulileta utata mkubwa sana maana watu walijiuliza kumbe akiwa RPC lakini kwapani alikuwa ni kada wa CCM? Ni kwa vipi angetenda haki Kwa vyama vya upinzani? Mungu ameamua ugomvi, ngoja na mimi nijaribu kuziba nafasi yake Arusha.
 
Pole Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa kuondokewa na Best yako wa muda mrefu

Zelothe Stephen ndie akiwa tayari amestaafu kuwa RPC akiwa pale Dodoma ndie akapokea maelekezo ya kuendelea kutumikia Nchi katika capacity ya Kamanda wa Mkoa akapelekwa Mtwara kuwa RPC wakati wa vurugu za Gas na mwana Mama aliekuwa pale kama RPC na kazi akaisimamia Zelothe chumba kwa chumba shuka kwa shuka hadi akarejesha amani kule Kusini

Kwaheri Mwamba sie Wakwere hatuna tunachokudai
 
RPC wa Mara Kamanda Mustafa Wandwi baada ya kustaafu mbona alijiunga na CUF na akagombea Ubunge Musoma mjini kupitia CUF mwaka 2000?

Mabere Nyaucho Marando Kachero na Jasusi Bobezi mbona ameshawahi kuwa Mbunge wa Rorya ?

Mbona Lyatonga Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa Shinyanga baadae alihamia Upinzani na kuwa Mbunge wa majimbo tofauti?

Mbona Robert Mboma Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama alishawahi kugombea Ubunge Mbeya vjijini ?

Kamanda Alfred Tibaigana alijitosa kwny kiny'anganyiro cha Ubunge kule Muleba kwa Prof Tibaijuka katika uchaguzi wa 2010


Adadi Rajabu alikuwa Mbunge kabisa kule kwa Mwana FA japo aliwahi kuwa Kachero Mkuu wa Nchi wakati wa Mzee Benjamin Mkapa


Mwacheni Swahiba wa amani ya Nchi apumzike
 
Sawa Sawa
Viongozi Kukumbatia Vyeo Vya Ccm Huku Wakiwa Bado Ni Watumishi Wa Umma Inatia Kinyaa
 
Unaposema kurejesha amani huku mtwara unamaanisha nini?Kikwete ni zaidi ya shetani
 
Kurejesha amani namaanisha kuitoa Gas Mtwara kuileta Dar es salaam,


Unaposema kurejesha amani huku mtwara unamaanisha nini?Kikwete ni zaidi ya shetani
' Kama huwezi kustahamili chuki za watu, matusi, kejeli na hasira zao basi usijaribu kuwa Mwanasiasa na kama utajaribu basi huwezi kuwa Mwanasiasa Mwandamizi '- Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete Mizega- Amiri Jeshi Mstaafu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Ni pumba gani unaziandika mpuuzi wewe mimi ninaekusimulia ni muhanga wa hizo vurugu za gas sasa unaniletea drama za kipuuzi hapa halafu nikuchekee
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…