Rais Samia aendelea kuiteka mioyo ya wana CHADEMA kwa uchapa kazi wake, wasafiria nyota yake kupata uungwaji mkono Kanda ya Ziwa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,243
9,700
Ndugu zangu Watanzania,

Hakika Rais Samia Haepukiki Wala Hazuiliiki katika mioyo ya watanzania,Huwezi ukafanikiwa kulitawala jukwaa la kisiasa na kupata wasikilizaji ikiwa utajifanya kumshambulia na kutokutambua juhudi za mh Rais wetu mpendwa mama Samia, kwa kuwa Ni Rais Samia ndiye aliyerejesha mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ili kutoa nafasi kwa watu wote kusikika sauti zao na mawazo yao juu ya ujenzi wa Taifa letu.

Ni Rais Samia ndiye aliye rejesha amani katika mioyo ya waliokuwa na chuki na serikali kwa sababu mbalimbali,Ni Rais Samia ndiye aliyejenga umoja wa kitaifa ulio imara na madhubuti Kama sakafu ya zege,Ni Rais Samia aliyestawisha demokrasia na masikilizano hapa nchini,Ni Rais Samia ndiye aliye kata kamba za hasira chuki jazba visasi na maombi mabaya katika mioyo ya baadhi ya watanzania na Ni Rais Samia aliyejenga Imani na kuaminiani kwa watanzania wa makundi yote.

Kwa hali hii kila mtu ,kila mpinzani,kila mwanachadema anamuona Rais Samia Kama mkombozi wao,kila mpinzani anamuona Rais Samia Kama kiongozi wake,ndio sababu ya kupongezwa Sana na kutajwa Mara nyingi Sana na Kuuteka mkutano wa chadema na viongozi wao kutokana na kutambua juhudi kubwa zilizofanywa na Rais huyu shupavu Jasiri na shujaa wa Afrika katika kuimarisha uchumi, Demokrasia na kuongoza nchi kwa kufuata na kuzingatia misingi ya utawala Bora na utawala wa kisheria.

Utasema Nini na kumshambulia vipi Rais Samia mpaka ueleweke na kuungwa mkono na watanzania? Nani atakusikiliza ukimtukana Rais Samia? Nani atavumilia kuona ukimsimanga Rais wao mpendwa mama Samia ? Watanzania Ni mashuhuda wa kazi kubwa na za kutukuka zilizofanywa na Rais Samia kila Kona ya nchi hii, watanzania Ni mashuhuda na wanaona jitihada za mh Rais kuwakwamua kiuchumi.

Vijana ambao wamekuwa mtaji wa vyama vya upinzani hawawezi wakakuelewa ukiwaambia wasimuunge mkono Rais Samia maana wanaona namna Mama Yao alivyo fanya kazi kubwa ya kuwawekea mazingira wezeshi ya kupata fursa za ajira na kujiajiri, kutoa ajira za moja kwa moja kwa vijana kupitia serikali yao,kuwapatia mikopo kupitia halmashauri zao na kuwekeza mabillioni ya pesa katika shughuli na miradi inayo gusa maisha yao vijana na kutoa ajira kwao.

Utawaambia Nini na kuwashawishi vipi watumishi wa umma wakati wanaona namna mh Rais Samia alivyo ibua furaha na Tabasamu mioyoni mwao kwa kuwaongezea mishahara hasa wa kima Cha chini kwa 23%,kuwapandisha madaraja kazini,kuwalipa malimbikizo ya madeni Yao, kuwaboreshea mazingira Yao ya kazi na kuwathamini kwa kazi zao kwa kuwasikiliza na kutoa majibu kwa wakati.

Utawaambia Nini na kuwashawishi vipi wakulima wanaonufaika na mbolea za Ruzuku,Bei nzuri ya mazao yao,hakuna mkulima atakayekusikiliza akiona unamshambulia Rais wao,lazima apambane na wewe na kukuzomea,utawaambia Nini vijana wanaopata Elimu bure Hadi kidato Cha sita na kupata mikopo ya Elimu ya juu bila shida yoyote na hivyo kutimiza Ndoto zao za kielimu.

Hii ndio sababu ya kuona vyama vya upinzani hasa chadema vikitambua juhudi kubwa zilizofanywa na mh Rais na kumpongeza hadharani na kuahidi Kuendelea kumuunga mkono katika ujenzi wa Taifa letu,maana wote wanatambua namna mh Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania alivyo msikivu kwa watu wote.

Rai yangu kwa Rais wangu mama Samia Ni Kuendelea kuchapa kazi,kusonga mbele katika kuwatumikia watanzania kwa kuwa amepewa baraka zote na watanzania na kuungwa mkono na watanzania wote wa makundi yote,Ni Tanzania iliyo moja chini yake ambayo yote inamtizama yeye kwa jicho la matumaini makubwa na matarajio makubwa ambayo mpaka Sasa anaendelea kuyatimiza kwa watanzania.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa , kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hakika Rais Samia Haepukiki Wala Hazuiliiki katika mioyo ya watanzania,Huwezi ukafanikiwa kulitawala jukwaa la kisiasa na kupata wasikilizaji ikiwa utajifanya kumshambulia na kutokutambua juhudi za mh Rais wetu mpendwa mama Samia, kwa kuwa Ni Rais Samia ndiye aliyerejesha mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ili kutoa nafasi kwa watu wote kusikika sauti zao na mawazo yao juu ya ujenzi wa Taifa letu.

Ni Rais Samia ndiye aliye rejesha amani katika mioyo ya waliokuwa na chuki na serikali kwa sababu mbalimbali,Ni Rais Samia ndiye aliyejenga umoja wa kitaifa ulio imara na madhubuti Kama sakafu ya zege,Ni Rais Samia aliyestawisha demokrasia na masikilizano hapa nchini,Ni Rais Samia ndiye aliye kata kamba za hasira chuki jazba visasi na maombi mabaya katika mioyo ya baadhi ya watanzania na Ni Rais Samia aliyejenga Imani na kuaminiani kwa watanzania wa makundi yote.
Aya ya pili, tueleze humu ninani alipoka mshikamano wa nchi mpaka leo uone, Rais aliyepo amerejesha? Niwambie ndugu zangu shida sio mtu aliyeharibu misingi ya Taifa hili ,bali ni chama ama mfumo, na mfumo huo upo, na utakuepo ila sasa ni kuwahaadaa tu..Lucas wewe unapenda mtu au chama ? Je unapenda nchi yako au chama chako au mtu wako ?.
 
Wewe jama ni chawa wa ukweli
Mimi Ni msema kweli kwa hoja za ukweli kwa uthibitisho wa ukweli

Nalipenda Taifa langu ambalo siku zote limekuwa salama na Tulivu kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na serikali ya CCM
 
Mara nyingi kisha weka namba kwenye KUJIPENDEKEZA huku, lakini haijamsaidia! Namba tu haitoshi, awe anaweka na. Picha yake, labda ATAONWA!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Kazi yangu siyo kuonwa Wala siandiki hapa kwa ajili ya kuonwa Bali Ni kuwasilisha mawazo yangu juu ya mwenendo mzuri wa kiuongozi wa Rais wetu mpendwa mama Samia na serikali yake aliyoiunda kututumikia watanzania
 
Mimi Ni msema kweli kwa hoja za ukweli kwa uthibitisho wa ukweli

Nalipenda Taifa langu ambalo siku zote limekuwa salama na Tulivu kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na serikali ya CCM
Kule kwenu, Chama kimefanya yepi ambayo wewe na nduguzo wanasherekea?
 
Kule kwenu, Chama kimefanya yepi ambayo wewe na nduguzo wanasherekea?
Sisi Kama wakulima tumefaidika na serikali hii ya CCM kwa kupatiwa mbolea za Ruzuku baada ya juhudi za makusudi za mh Rais wetu mpendwa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu.

Lakini pia Bei ya mazao yetu Ni nzuri na ilikuwa hivyo tangia wakati wa mavuno,ukienda katika huduma za kijamii Kama Elimu ,Afya,maji na huduma za umeme vyote Ni vya uhakika na vimesogezwa karibu yetu,
 
Hela za mbolea Serikali yako imezitoa wapi?mpaka wewe uone hisani??
 
Hela za mbolea Serikali yako imezitoa wapi?mpaka wewe uone hisani??
Imetoa katika mfuko wetu tunaochanga kwa pamoja amba nchi zingine waliokosa fursa hiyo kutoka kwa viongozi wao kutokana na kukosa maono na utambuzi na hivyo kuacha wananchi wao wakiumia na kuteseka,Na Ikumbukwe kuwa Bei ya mbolea haikupandishwa na serikali yetu Bali uliotokana na mfumuko wa Bei katika soko la Dunia
 
Mfuko mnaochanga kwa pamoja unapata pesa kutoka wapi? Mpaka wewe uone ni hisani?
 
Back
Top Bottom