Rais Samia achangia mamillioni ya pesa taasisi ya profesa Jay Foundation, atoa maagizo mazito kwa Wizara ya Afya na Muhimbili

Rais Samia achangia mamillioni ya pesa taasisi ya profesa Jay Foundation, atoa maagizo mazito kwa Wizara ya Afya na Muhimbili

Rais Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,nuru ya wanyonge,nyota ya matumaini,simba wa nyika, komandoo wa vita,mama wa upendo, mzalendo wa kweli,mwamba wa siasa ameendelea kuonyesha moyo wake mkubwa wa upendo na ukarimu kwa watanzania anao waongoza.
Umeandika kishabiki na kishamba saana

Kwani ametoa kwenye mshahara wake?
 
Lamsingi ni Serikali kuboresha huduma za Afya kila mahala Tanzania ziwe world class na si kusubiri mtu aumwe ndio tuanze kuchanga na kutafuta mileage za uchaguzi.

Hospitali ziwe na vifaa vya kisasa, madaktari wabobezi wakutosha nk.

Serikali isomeshe madaktari bingwa wengi sana kukidhi kada hii hasa haya magonjwa ambayo tiba zake hapa ni ngumu, kikubwa ni watalaam na vifaa.

Haiwezekani toka awamu ya kwanza mpaka leo awamu ta sita zaidi ya miaka 30 ya uhuru hatuna madaktari bingwa wa figo, moyo nk na vifaa vyake kiasi cha watu kwenda India na SA..
 
wengine ambao sio akina Prop Jay ambao ni mamilioni ya watu tunafanyeje, maana umezungumzia Rais kutoa maagizo mazito dhidi ya huduma kwa Prop Jay, maana yake Rais anakubali pale Muhimbili kuna tatizo, sasa hawa watanzania wengine mamilioni ambao kila siku wamejaa pale Muhimbili.
Hii ni kwa ajili ya wenye majina tu.

Mbona mie Nina ndugu mwenye tatizo hilo hilo na ameomba kwenda kutibiwa India lakini Mujimbili wamekataa kutoa barua japo na yeye bado yuko kwenye ajira. Hapa naona ni maigizo kwa wasio na usemeo.
 
Wewe huwezi kuwa Rais wetu maana Taifa letu haliwezi kuongozwa na vichaa na wendawazimu kama wewe
Kichaa akiwa uchi barabarani watu wakimshangaa naye huwashangaa na kuwaona waliojisitiri ni vichaa wamejibebesha mizigo.

Kila mmoja anakushangaa, nawe unamshangaa kila mmoja!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lamsingi ni Serikali kuboresha huduma za Afya kila mahala Tanzania ziwe world class na si kusubiri mtu aumwe ndio tuanze kuchanga na kutafuta mileage za uchaguzi...
Hayo uliyoyaeleza yanafanywa na serikali yetu na hata haya matibabu ya figo yanafanywa hapa hapa nchini,lakini pia serikali yetu imeendelea kusomesha madaktari bingwa nje ya nchi.
 
Kwani million hamsini ni kitu gani kwa kiongozi kama Rais? Yaani wabunge tu wanazo hizo million hamsini ndio Rais asiwe nazo? Hata hivyo kutoa ni moyo na siyo utajili. Kuna wengine wana fedha nyingi lakini huwezi kuwaona wala kuwasikia wakitoa misaada kwa watu wenye uhitaji.
Utajili ndio kitu gani wewe chawa?

Halafu anza kujipanga kurudi shule.

Huyu bibi wa kizimkazi 2025 hatokuwepo nimekuibia siri hiyo.

Umenielewa chawa mwenye utapiamlo wa akili ?
 
Utajili ndio kitu gani wewe chawa?

Halafu anza kujipanga kurudi shule.

Huyu bibi wa kizimkazi 2025 hatokuwepo nimekuibia siri hiyo.

Umenielewa chawa mwenye utapiamlo wa akili ?
Asante kwa masahihisho .lakini pia napenda kukwambia kuwa Rais samia tu tunaye mpaka 2030 ,Rais samia ameinuliwa na Mungu kwa makusudi maalumu kuliongoza Taifa letu .huwezi ukashindana na aliye pewa kibali na Mungu.
 
Back
Top Bottom