'Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mgonjwa'

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
'Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mgonjwa'

Na Mashirika ya Habari

ZIMEIBUKA taarifa za kutatanisha juu ya hali tete ya afya ya Rais wa Zimbabwe, Bw. Robert Mugabe (87) huku zingine zikieleza kuwa hali yake si nzuri na amelazimika kulazwa hospitalini nchini Malaysia baada ya kufanyiwa
upasuaji kutibu kansa ya kibofu.

Tangu Jumatatu kumekuwepo na taarifa mbalimbali za vyombo vya habari vya kimataifa na mitandao mbalimbali kama vile Sauti ya Amerika, Daily Telegraph, zikinukuu vyanzo mbalimbali vya ndani, serikalini na kwenye chama zikisema kuwa kiongozi huyo wa Zimbabwe ana hali mbaya tangu afanyiwe operesheni hiyo hivi karibuni.

Lakini kwa haraka, maafisa wa Serikali ya Zimbabwe hata wale wa chama chake cha ZANU-PF wamekanusha taarifa hizo, wakisema Rais Mugabe yuko katika mapumziko ya mwaka, ambayo huyafanya Desemba hadi Januari, kila mwaka.

Habari juu ya hali tete ya Rais Mugabe kwa mara hii, zilianza kuripotiwa na Gazeti la Daily Telegraph (Uingereza) la Jumatatu, likisema kuwa kiongozi huyo matata, alikuwa hopsiotali baada ya kufanyiwa operesheni. Ingawa pia haikusemwa kama ilikuwa ni uchunguzi wa afya wa kawaida ama la.

Msemaji wa Rais Mugabe, Bw. George Charamba, alitupilia mbali taarifa hizo, huku mbali ya kusema kuwa kiongozi huyo yuko likizo ya mwaka, amenukuliwa akisema “unaonekana kujua mambo mengi kuhusu rais kuliko mimi mwenyewe ninavyojua…kadri ninavyojua, rais yuko likizo yake ya mwaka na suala hili tuliutaarifu umma, atarudi muda si mrefu,” amenukuliwa Bw. Charamba.

Kwa mujibu wa mtandao wa NewsDay, kwa sasa Makamu wa Rais, John Nkomo ndiye anayekaimu nafasi ya Komredi Mugabe.
Kwa upande wake msemaji wa ZANU-PF, Bw. Rugare Gumbo naye hakutoa kauli tofauti na Charamba, akisema kiuwa hata chama kinajua kuwa rais yuko likizo na si vinginevyo.

Jumatatu iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Malysia Bw. Datuk Seri Hishammuddin Hussein, alipoulizwa na waandishi wa habari, juu ya taarifa za Daily Telegraph kuwa Rais Mugabe alikuwa nchini humo, alikataa kukubali wala kukanusha habari hizo.

“Siwezi kukubali wala kukanusha juu ya taarifa hizo,” amenukuliwa waziri huyo katika gazeti la The Malaysian Insider.
Kwa mujibu wa taarifa kadhaa, Rais Mugabe ambaye amekuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1980, huku akitimiza miaka 87 ifikapo February, 2011, alifanyiwa uchunguzi wa afya yake akiwa likizoni mapema mwezi huu wa Januari.

Kwa miaka kadhaa sasa, kumekuwepo na uvumi wa mara kwa mara juu ya hali tete ya kiafya ya rais huyo, lakini haijawahi kuthibitika hata mara moja, hali iliyomlazimu kulizungumzia suala wakati fulani na kubeza.

Mwezi Septemba mwaka jana, mbele ya wahariri wa vyombo vya habari nchini humo, akiwa ikulu, kwa mara ya kwanza alizungumzia juu ya uvumi huo wa mara kwa mara juu ya hali tete ya afya yake na kusema “ sijui huwa ninakufa mara ngapi, lakini hakuna hata mmoja amewahi kusema nimefufuka lini.

“Nafikiri hawataki kuzungumzia, maana watalazimika kuzungumzia kufufuka kwangu mara kwa mara na hiyo maana yake ni utakatifu kitu ambacho kitakuwa ni mafanikio kwa mtu ambaye si mtakatifu…Yesu alikufa mara moja na akafufuka mara moja tu, muda wangu utafika, lakini si sasa,” aliwahi kusema Rais Mugabe.
 
This is poetic justice for Africa and Zimbwabwe in particular............................I will go to Harare to bury Mugabe but not to mourn his eventual demise....................
 
I think age wise mwili umeishaanza kuchoka between he has stayed in power for to long, for the time that he has left he needs to rest
 
Good observation.....lakini la kushangaza hayupo tayari kuachia ngazi.......................................Viongozi wa Afrika wanapougua hawako tayari kutibiwa nchini kwao na kwa hali hiyo huduma za afya kamwe Afrika hazitakaa zitengemae hata kidogo.........................
 
Pole sana the true son of africa. Usife upesi, bado tunakuhitaji sana kwenye ukombozi wa Zimbabwe na Afrika kwa ujumla.
 
Mugabe may be has forgot the fact that the World is still ruled by WAZUNGU in terms of economy and power. So my his decision to DENY wazungu from ruling Zimbabwe, its pipo of Zimbabwe who are hurted.
Also most African leaders are RULERS instead of LEADERS.
While wazungu rules the World, they are simply LEADERS in their own countries
 
Bob Mugabe yuko fiti,hizo ni rumours zilizoenezwa na vyombo vya magharibi..kwani ni mara ya kwanza kuzushiwa hivi??mtu yupo zake anakula pepo nyie mnapiga longolongo hapa
 
Long live Mugabe! get well soon son of the soil but this time allow someone else to lead coz its too late!
I hope there will be someone to build on your strengths..................and that there will be someone to learn from your mistakes and give Zimbabweans and Africa the best that you wanted to realise in ways that were not pleasing to Americans and Europeans.:crying:
 
Kama kweli Mugabe angekua mpiganaji wa maslahi ya wa Zim wote nasio yeye binafsi angechagua succesor mda mrefu awe amemtrain halaf anamwachia madaraka na kumguide kwa remote control. Lakin kwasbab ni jitu la tamaa akifa ndio mwisho!
 
Kama Mugabe asingewanyang'anya Walowezi wa Kizungu mashamba yao tena bila ya kuwalipa fidia kitendo ambacho kimsingi kilitokana na Serikali ya Uingereza kushindwa kutekeleza makubaliano ya Lancaster, mpaka leo angeendelea kuheshimiwa na mataifa ya magharibi
na hivyo maslahi yake binafsi yangekuwa bora zaidi lakini kwa kuwa aliamua kinyume na matakwa yao kwa ajili ya Wazimbabwe weusi makini leo hii amekuwa dikteta na mtawala muovu.

To me, Mugabe is an icon of African emancipation from western domination, african leaders should stop bowing to western threats and corrupting influences, longlive comrade Bob Mugabe.
 
Butola hapakuwa na njia ingine ya akili zaidi ambayo Mugabe angeweza kutumia? Wale veterans walikua wanavamia ranches vunja nyumba na kuchoma moto matractor,irrigation systems and other facilities. Ilikua ni ushujaa wa kijinga,sasa wamemkomoa nani? Njia sahihi ingekua kutumia hypocrasy hio hio ya wazungu kuwaumiza bila kuharibu maslahi ya taifa directly. E.g. Ongeza kodi yao ya kulima na weka askari kanzu wa kulinda rasilimali. In a few years angeweza lipa deni la lancaster bila ushujaa bila akili.
 
Nakubaliana na wewe hasa ukizingatia madhara yaliyoletwa na kitendo hicho lakini sioni sababu ya yeye kutafuta pesa za kuwalipa Walowezi wa Kizungu fidia ya ardhi walioinyang'anya awali kwa nguvu kutoka kwa wazawa wa Zimbabwe, hili lilikuwa ni jukumu la Serikali ya Uingereza kufanya hivyo.

Lakini yatupasa pia tuzingatie ugumu aliokuwa nao kutokana na Wazimbabwe kuchoka kusubiri zaidi, Umri kumtupa mkono huku akiwa hajakamilisha lengo la msingi la ukombozi wa watu wa Zimbabwe na wakati huohuo Waingereza kutoonyesha dalili za kutimiza makubaliano.

Naamini ulikuwa ni uamuzi mgumu na wenye risk kubwa lakini naiunga mkono nia na dhamira yake katika hilo.
 
'Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mgonjwa'

Na Mashirika ya Habari

ZIMEIBUKA taarifa za kutatanisha juu ya hali tete ya afya ya Rais wa Zimbabwe, Bw. Robert Mugabe (87) huku zingine zikieleza kuwa hali yake si nzuri na amelazimika kulazwa hospitalini nchini Malaysia baada ya kufanyiwa
upasuaji kutibu kansa ya kibofu.

Tangu Jumatatu kumekuwepo na taarifa mbalimbali za vyombo vya habari vya kimataifa na mitandao mbalimbali kama vile Sauti ya Amerika, Daily Telegraph, zikinukuu vyanzo mbalimbali vya ndani, serikalini na kwenye chama zikisema kuwa kiongozi huyo wa Zimbabwe ana hali mbaya tangu afanyiwe operesheni hiyo hivi karibuni.

Lakini kwa haraka, maafisa wa Serikali ya Zimbabwe hata wale wa chama chake cha ZANU-PF wamekanusha taarifa hizo, wakisema Rais Mugabe yuko katika mapumziko ya mwaka, ambayo huyafanya Desemba hadi Januari, kila mwaka.

Habari juu ya hali tete ya Rais Mugabe kwa mara hii, zilianza kuripotiwa na Gazeti la Daily Telegraph (Uingereza) la Jumatatu, likisema kuwa kiongozi huyo matata, alikuwa hopsiotali baada ya kufanyiwa operesheni. Ingawa pia haikusemwa kama ilikuwa ni uchunguzi wa afya wa kawaida ama la.

Msemaji wa Rais Mugabe, Bw. George Charamba, alitupilia mbali taarifa hizo, huku mbali ya kusema kuwa kiongozi huyo yuko likizo ya mwaka, amenukuliwa akisema “unaonekana kujua mambo mengi kuhusu rais kuliko mimi mwenyewe ninavyojua…kadri ninavyojua, rais yuko likizo yake ya mwaka na suala hili tuliutaarifu umma, atarudi muda si mrefu,” amenukuliwa Bw. Charamba.

Kwa mujibu wa mtandao wa NewsDay, kwa sasa Makamu wa Rais, John Nkomo ndiye anayekaimu nafasi ya Komredi Mugabe.
Kwa upande wake msemaji wa ZANU-PF, Bw. Rugare Gumbo naye hakutoa kauli tofauti na Charamba, akisema kiuwa hata chama kinajua kuwa rais yuko likizo na si vinginevyo.

Jumatatu iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Malysia Bw. Datuk Seri Hishammuddin Hussein, alipoulizwa na waandishi wa habari, juu ya taarifa za Daily Telegraph kuwa Rais Mugabe alikuwa nchini humo, alikataa kukubali wala kukanusha habari hizo.

“Siwezi kukubali wala kukanusha juu ya taarifa hizo,” amenukuliwa waziri huyo katika gazeti la The Malaysian Insider.
Kwa mujibu wa taarifa kadhaa, Rais Mugabe ambaye amekuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1980, huku akitimiza miaka 87 ifikapo February, 2011, alifanyiwa uchunguzi wa afya yake akiwa likizoni mapema mwezi huu wa Januari.

Kwa miaka kadhaa sasa, kumekuwepo na uvumi wa mara kwa mara juu ya hali tete ya kiafya ya rais huyo, lakini haijawahi kuthibitika hata mara moja, hali iliyomlazimu kulizungumzia suala wakati fulani na kubeza.

Mwezi Septemba mwaka jana, mbele ya wahariri wa vyombo vya habari nchini humo, akiwa ikulu, kwa mara ya kwanza alizungumzia juu ya uvumi huo wa mara kwa mara juu ya hali tete ya afya yake na kusema “ sijui huwa ninakufa mara ngapi, lakini hakuna hata mmoja amewahi kusema nimefufuka lini.

“Nafikiri hawataki kuzungumzia, maana watalazimika kuzungumzia kufufuka kwangu mara kwa mara na hiyo maana yake ni utakatifu kitu ambacho kitakuwa ni mafanikio kwa mtu ambaye si mtakatifu…Yesu alikufa mara moja na akafufuka mara moja tu, muda wangu utafika, lakini si sasa,” aliwahi kusema Rais Mugabe.
Namuombea babu apone haraka,kwani bado tunamhitaji kuendeleza heshima ya MWAFIRIKA ambayo siku hizi inachezewa kama mboga ya PITIKU
 
Ila miaka 87 ni mingi sana kuwa fit kiakili na kimwili. Namkubali Mgabe ila ni wakati akaandaa mrithi manake life span yake imefikia kikomo.
Africa will loose a solder... Get well soon grang pa Mgabe.
 
Back
Top Bottom