#COVID19 Rais Ramaphosa akutwa na maambukizi ya COVID-19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
1639383455461.png

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amepimwa na kukutwa na Covid-19 na anatibiwa kwa dalili zisizo kali.

Bw Ramaphosa alianza kujisikia vibaya siku ya Jumapili baada ya kuondoka katika ibada ya kumbukumbu ya Rais wa mwisho wa enzi za ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini FW De Klerk mjini Cape Town, kulingana na taarifa kutoka kwa ofisi ya rais.

Watu ambao walitangamana na rais siku hiyo wameshauriwa kutazama dalili au kupimwa.

Rais amepewa chanjo kamili na amekabidhi majukumu yake yote kwa Naibu Rais David Mabuza.

Rais Ramaphosa alirejea Jumatano iliyopita kutoka katika ziara ya nchi za Afrika Magharibi za Nigeria, Ivory Coast, Ghana na Senegal.

Rais alisema yeye na ujumbe wake walipimwa Covid katika nchi zote walizotembelea. Taarifa hiyo ilisema rais alikuwa amepatikana bila virusi hivyo aliporejea.

Kirusi cha Omicron kinachoambukiza sana, ambacho kimezua wasiwasi wa kimataifa, kilitambuliwa kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini mwezi uliopita.

BBC Swahili
 
Sasa umuhimu wa hiyo chanjo nnn kama.bado unaambukizwa hali inakuwa tete mpaka kulazwa kabisa?

Duh, afadhali ni uamuzi wa mtu kuchanja au kutochanja!
 
Kuugua kwa President CR sio siri na dunia nzima tunajua ILA kuna nchi President wake yupo in ICU fighting for his life wananchi wake wakaambiwa wachape kazi Rais yupo salama anapiga kazi!na hii yote kwa sababu ya ukilaza wa raia wa nchi hiyo!
 
Mhe. Rais wa Afrika Kusini Kamaradi Cyril Ramaphosa yuko kitandani kwa shambulizi la Omicron Variant. Tumuombee huyu Superpower wetu wa Afrika.







Cyril Ramaphosa Flag of South Africa

@CyrilRamaphosa


Thank you, fellow South Africans, for your good wishes following my COVID-19 positive result. As I recover, my message of the week is: don’t let your guard down. Do everything you can and need to, to stay safe, beginning with vaccination.

11:46 AM · Dec 13, 2021·Twitter for iPhone
 
Nimemsikiliza vizuri kumbe mzee hapendi ujinga wa kikoloni. Anadai mabeberu watuonyeshe namana ya kutengeneza chajo na siyo kuleta ready made chanjo eti sisi tufanye kazi ya kujaza na kuweka lebo.
 
Nimemsikiliza vizuri kumbe mzee hapendi ujinga wa kikoloni. Anadai mabeberu watuonyeshe namana ya kutengeneza chajo na siyo kuleta ready made chanjo eti sisi tufanye kazi ya kujaza na kuweka lebo.
Huyu watamchomoa.... Bado yule anayevaa kofia ya mviringo pale ziwa Victoria
 
Back
Top Bottom