Rubawa
JF-Expert Member
- Dec 25, 2015
- 2,055
- 3,267
NA MOHAMMED ABDURAHMAN
Miongoni mwa wanasiasa maarufu sana nchini Cote d´Ivoire ni
Guillaume (GIYOM) Sorro. Alikuwa kijana wakati jina lake lililopoanza
kuvuma, wakati akiwaongoza waasi waliokuwa wakipigana dhidi ya
majeshi ya serikali ya Rais aliyekuwa madarakani Laurenrt Gbagbo.
Hiyo ilikuwa ni wakati ilipozuka vita ya wenyewe kwa wenyewe 2002,
muda mfupi baada ya Gbagbo kuingia madarakani pamoja na
machafuko yaliofuatia 2010-2011.
Cote d´Ivoire, taifa la Afrika magharibi na ambalo linasisitiza lijulikane
kwa jina hilo na sio tafsiri ya Kiingereza ya Ivory Coast lilitumbukia
katika mgogoro wa kisiasa na mapigano baada ya Gbagbo kuyakataa
matokeo ya uchaguzi wa Rais Novemba 2010 na Mwenyekiti wa tume
aliyemdhibiti kumtangaza yeye kuwa mshindi, pamoja na kwamba kura
zikionesha ni Ouattara aliyeshinda uchaguzi.
Koloni hilo la zamani la Ufaransa liligawika kati ya Kaskazini na Kusini.
Sorro ni mkristo kutoka Kaskazini eneo lenye wakaazi wengi wa
Kiislamu na Gbagbo ni kutoka Kusini.
Sorro ni mshirika wa zamani wa chanda na pete wa Rais aliyeko
madarakani Alassane Ouattara ambaye ni Muislamu kutoka pia
Kaskazini, lakini watu hao wawili walianza taratibu kutafautiana
baadaye baada ya Sorro kutangaza nia yake ya kutaka kugombea
katika uchaguzi wa Rais Oktoba mwaka huu unaoanza leo Jumatano
wa 2020.
Tayari alishakuwa Waziri mkuu kuanzia 2007 na baadaye 2011 hadi
mwaka jana 2019 akawa Spika wa Bunge la taifa hilo. Mvutano wa
watu hao wawili ulizidi kupamba moto Desemba 23, pale ndege
ya Sorro ilipobadili njia na kuelekea Ghana badala ya
kutuwa nyumbani.
Alikuwa akirejea nyumbani kutoka nje alikokuweko kwa miezi kadhaa.
Hakuweza kufahamika kilichosababisha tukio hilo, lakini maafisa wa
Cote d´Ivoire wanasisitiza ulikuwa uamuzi wa Sorro mwenyewe
kwamba ndege yake ikatuwe nchi hiyo jirani.
Huko nyuma nyumbani yakaibuka mengine zaidi. Serikali imetoa
waranti wa Sorro kukamatwa, ikimshutumu kwa kula njama dhidi yadola na kwamba vyombo vya usalama vilikuwa na ushahidi kuwa
kiongozi huyo wa zamani wa waasi akipanga kutekeleza hivi
karibuni aliyoyakusudia.
Mwendesha mashitaka wa serikali alisema Sorro anachunguzwa pia
kwa ubadhirifu wa fedha za serikali. Majeshi ya serikali yakayavamia
makao makuu ya chama chake mjini Abdijan Génération et Peuple
Solidaire ( Kizazi na Umma katika Mshikamano ) GPS. Hatua ya serikali
dhidi ya Sorro imeibuwa maswali mengi, kubwa na zito likiwa kama
Rais Alassane Dramane Ouattara maarufu kwa jina la “ADO“ ataachia
madaraka wakati muda wake utakapomalizika au atagombea tena
muhula wa tatu?
Ni kweli siasa haina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu. Wadadisi
wanasema huenda matukio ya karibuni ni njama ya kumzuwia Sorro
asiwe mgombea, ambaye umaarufu wake ni mkubwa na hasa miongoni
mwa vijana. Lakini si mshirika huyo wa zamani pekee anayeandamwa.
Ouattara pia ameamua kuwageukia Gbagbo na Bedié, akisema
atajimwga uwanjani ikiwa Gbagbo na Bedié wataamua kuwemo
kwenye kinyang’anyiro cha kugombea Urais. Wote wawili bado
hawajatangaza kama watagombea.
Katika mkutano mmoja na maafisa wa chama chake, alisema
hatouunga mkono mpango wowote wa kutaka kubadili kifungu cha
katiba kurejesha umri wa miaka 75 kuwa ndio kikomo kwa mwenye
kugombea Urais. Hata hivyo ingawa Ouattara mwenye umri wa miaka
78 ameshasema anaamini katiba ya 2016 inamruhusu kugombea tena,
jambo ambalo linapingwa na vingi miongoni mwa vyama vya kisiasa
yungali akiwachezesha raia kindumbwe ndumbwe, akisita kutamka wazi
anachokusudia, zaidi ya kuendelea na vijembe na mafumbo. Katika
mkutano mwingine na waandishi habari Ouattara alisema : “Kile mtu
anachoweza kufanya katika umri wa miaka 68 hawezi kukifanya
tena anapokuwa 78, achilia mbali unapokuwa miaka 85 au
86.“ Matamshi yake yalielekea kumgonga hasimu yake Bedié
ambaye ana umri wa miaka 85. Gbagbo ana umri wa miaka 75 na
tangu alipoachiwa huru kwa masharti na Mahakama ya Jinai ya
Kimataifa -ICC mjini The Hague, kufuatia mashitaka yaliohusiana na
machafuko ya baada ya uchaguzi 2011, anaishi bado nchin Ubeligiji.
Kurudishwa kifungu hicho ndani ya katiba, kutamzuwia pia Henri
Konan Bedié aliyeshika hatamu na kuliongoza taifa hilo kwa mujibu
wa katiba alipokuwa Spika wa bunge baada ya kifo cha Rais wa
kwanza Felix Houphouet-Boigyn 1993, . Bedié alikuwa pia mshirika wa
ADO alipomshinda Gbagbo. Uhasama wao umetokana na kile
mwanasiasa huyo mkongwe alichodai kuwa ni kuvunjwa makubaliano
ya awali kwamba uchaguzi unaofuata mgombea Urais atatoka katikachama chake Parti Démocratique de Côte d’Ivoire (Chama cha
Demokrasia cha Cote d´Ivoire)-PDCI na sio Rassemblement des
Houphouétistes pour la démocratie et la paix ( Mkusanyiko wa wafuasi
wa Houphouet kwa ajili ya Demokrasia na Amani)-RHDP.
Sakata la Sorro linaloendelea kugonga vichwa vya habari, lilitokea saa
24 tu baada ya ziara ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
kumtembelea Rais Ouattara, kwa kile kilichoelezwa ni mazungumzo
kuhusu usalama katika eneo la Sahel na kuwazuru wanajeshi wa
Ufaransa mjini Abidjan ambako dola hilo lina kambi ya kijeshi.
Kiongozi wa Cote d´Ivoire ni mshirika mkubwa wa Ufaransa na majeshi
ya nchi hiyo yaliwasaidia waasi kumn´goa Rais wa zamani Gbagbo.
Gazeti la Le Figaro, lilikuwa na kichwa cha maneno “Ushindi kwa
Ufaransa”, na kuyaeleza yaliotokea kuwa mabadiliko katika
sera ya Sarkozy ambaye alipoingia madarakani alikuwa na matatizo
ya kufafanua siasa yake kuelekea bara hilo.
Alipoitetea hatua yake ya kuamuru wanajeshi wa Ufaransa wajiingize
kati kumuangusha Gbagbo, Sarkozy alidai Umoja wa Afrika
na Jumuiya za Kikanda barani humo zilishindwa kuchukua hatua
kumuondoa madarakani gbagbo.
Alichosahau ni kuwa Ufaransa ina historia ndefu ya kutetea
madikteta katika makoloni yake ya zamani na kusaidia kukandamiza
vuguvugu la Umma kudai Demokrasia ambayo taifa hilo linadai ni
msingi wake mkubwa. Mwandalizi mkubwa wa mipango yote ya
hujuma barani humo yakiwemo mapinduzi katika mataifa kadhaa
makoloni yake ya zamani, Jacques Foccart aliyeitwa “Monsieur Afrique
du Charles De Gaulle”, (Bwana wa Afrika wa Charles De Gaulle) na
muasisi wa sera ya ukoloni mambo leo ya Ufaransa barani Afrika kwa
miaka mingi alikuwa na ofisi yake Ikulu ya Elysée alikoandaa mikakati
kuwadhibiti viongozi wakiafrika waliokuwa vibaraka. Ufaransa ina
masilahi makubwa ya kiuchumi Cote d´Ivoire ambako hadi katikati ya
1990 jiji lake Abidjan likijulikana kama ‘Paris ya Afrika.”
Kwa mara nyengine tena tatizo la muhula wa tatu linazidi kuibua
mijadala na migogoro wa kisiasa katika nchi nyingi za Afrika. Nchi jirani
na Cote d`Ivoire ya Guinea nako kumeibuka maandamano na
mvutano kati ya wapinzani na raia upande mmoja dhidi ya mpango
wa Rais Alpha Conde kutaka kuirekebisha katiba ili aweze kugombea
tena muhula wa tatu.
Alipokuwa akiishi uhamishoni kwa miaka mingi nchini Ufaransa, Conde
alikuwa msitari wa mbele kuwakosoa viongozi waliomtangulia nchini
Guinea kwa kubakia madarakani muda mrefu akisema tabia yaoinadumaza demokrasia na maendeleo. Kwa mshangao wa wengi na
yeye sasa anafuata mkondo ule ule . Ana umri wa miaka 81 na muhula
wake wa pili wa miaka mitano na wa mwisho kwa mujibu wa katiba
unamalizika mwaka huu wa 2020.
Kwa mtazamo huo, unapoyafuatilia yanayotokea Cote d´Ivoire, Guinea
na kwengineko ambako kuliibuka suala la viongozi kurefusha vipindi
vyao vya utawala, huenda waliosema madaraka matamu,
hawakukosea. Kuna hatari mgogoro huu mpya Cote d´Ivoire unaweza
kuirejesha tena kule ilikotoka miaka takriban 18 iliyopita.
Sent using Jamii Forums mobile app