Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,530
- 34,358
Kuna dhana imekomazwa kwenye akili za Watanzania na kugeuka kuwa ni utamaduni wetu kwamba Rais tunaemchagua akishaapishwa anageuka kuwa Bosi wa kila mtanzania jambo ambalo si sahihi.
Kwa mujibu wa Katiba yetu Rais anakuwa ni mtumishi namba moja wa nchi hii anayechaguliwa ili kuisimamia serikali (Siyo wananchi) kwa lengo la kuleta maendeleo kwa taifa kwa ujumla!
Rais anaweza kuogopwa na wale walioajiriwa kwenye serikali na taasisi zake pamoja na taasisi zingine za Umma, lakini haiyumkini Rais akaogopwa na Raia waliomchagua ambao kimsingi ndiyo mabosi wake. Na ndiyo maana wananchi wa kawaida hawahitajiki kusema hela wanazozipata wamezitumiaje wakati serikali inapaswa kutoa taarifa fedha wanazozipata kwa njia mbali mbali wanazitumiaje kwa kuwa wao pamoja na Rais ni watumishi wa Umma na wala siyo Umma ni watumishi wa waliio serikalini Rais akiwemo!