Rais ni mtumishi wetu na wala siyo Bosi wetu

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,493
34,247
Kuna dhana imekomazwa kwenye akili za Watanzania na kugeuka kuwa ni utamaduni wetu kwamba Rais tunaemchagua akishaapishwa anageuka kuwa Bosi wa kila mtanzania jambo ambalo si sahihi.

Kwa mujibu wa Katiba yetu Rais anakuwa ni mtumishi namba moja wa nchi hii anayechaguliwa ili kuisimamia serikali (Siyo wananchi) kwa lengo la kuleta maendeleo kwa taifa kwa ujumla!

Rais anaweza kuogopwa na wale walioajiriwa kwenye serikali na taasisi zake pamoja na taasisi zingine za Umma, lakini haiyumkini Rais akaogopwa na Raia waliomchagua ambao kimsingi ndiyo mabosi wake. Na ndiyo maana wananchi wa kawaida hawahitajiki kusema hela wanazozipata wamezitumiaje wakati serikali inapaswa kutoa taarifa fedha wanazozipata kwa njia mbali mbali wanazitumiaje kwa kuwa wao pamoja na Rais ni watumishi wa Umma na wala siyo Umma ni watumishi wa waliio serikalini Rais akiwemo!
 
Don't hit around the bush ...go straight and articulate what exactly you want to tell us.
 
Akili yako ndo imeishia hapo, "mteja mfalme" kale usilipe uone kichapo utakachopokea. Kuna mtumishi anapata mshahara mkubwa kuliko boss wake? Kuna mtumishi anatembea na walinzi boss hana hata mgambo, kuna mtumishi anatembea na msafara boss anachapa lapa, kuna mtumishi anamwamlisha boss wake cha kufanya hata asichopenda?

Sasa we endelea ujenge dhana yako
 
Hili jinga kubwa vipi? Eti likimuona shamba boy wake linakuwa kama limemuona JPM

PUUMBAVU
 
Hii inawezekana tu, katika nchi zile ambazo kuna Demokrasia ya kweli.

"A government afraid of its citizens is a Democracy. Citizens afraid of government is tyranny!" Thomas Jefferson

Hii inawezekana tu, pale kwenye uwajibikaji wa kweli upo. Nchi nyingi za kiafrika zinafanya kinyume kidogo na ulichokiosema katika uzi wako, kuna tofauti kubwa kati wa msimami na mtawala!
 
Kuna dhana imekomazwa kwenye akili za Watanzania na kugeuka kuwa ni utamaduni wetu kwamba Rais tunaemchagua akishaapishwa anageuka kuwa Bosi wa kila mtanzania jambo ambalo si sahihi.

Kwa mujibu wa Katiba yetu Rais anakuwa ni mtumishi namba moja wa nchi hii anayechaguliwa ili kuisimamia serikali (Siyo wananchi) kwa lengo la kuleta maendeleo kwa taifa kwa ujumla!

Rais anaweza kuogopwa na wale walioajiriwa kwenye serikali na taasisi zake pamoja na taasisi zingine za Umma, lakini haiyumkini Rais akaogopwa na Raia waliomchagua ambao kimsingi ndiyo mabosi wake. Na ndiyo maana wananchi wa kawaida hawahitajiki kusema hela wanazozipata wamezitumiaje wakati serikali inapaswa kutoa taarifa fedha wanazozipata kwa njia mbali mbali wanazitumiaje kwa kuwa wao pamoja na Rais ni watumishi wa Umma na wala siyo Umma ni watumishi wa waliio serikalini Rais akiwemo!

Hiyo ni dhanna potofu.

Kama unadhani mwananchi siyo serikali basi uelewe kuwa serikali bila wananchi hakuna.

Kwanza ni nini maana ya "bosi", kuna kila uwezekano hauelewi maana ya "bosi" ni nini jinsi ulivyoandika.
 
Hii inawezekana tu, katika nchi zile ambazo kuna Demokrasia ya kweli.

"A government afraid of its citizens is a Democracy. Citizens afraid of government is tyranny!" Thomas Jefferson

Hii inawezekana tu, pale kwenye uwajibikaji wa kweli upo. Nchi nyingi za kiafrika zinafanya kinyume kidogo na ulichokiosema katika uzi wako, kuna tofauti kubwa kati wa msimami na mtawala!

Hakuna popote kuna kitu kinaitwa demokrasia ya ukweli hapa duniani, acheni kujidanganya na kudanganywa. Democracy simply means power & interests, only that.
 
Mi nashangaa kila sekunde anasema mimi ndo Rais, mimi ndo Rais... Sijui ana mtishia nani!!
 
Mkuu kwani akisema "mimi ndio Raisi" anakukwaza nini??
Au unadhani kuna mtu anatishwa??
Wewe unadhani kwann kuna watu wana dhani wanatishwa kwa maneno hayo??
 
Hiyo ni dhanna potofu.

Kama unadhani mwananchi siyo serikali basi uelewe kuwa serikali bila wananchi hakuna.

Kwanza ni nini maana ya "bosi", kuna kila uwezekano hauelewi maana ya "bosi" ni nini jinsi ulivyoandika.
Si kila mwananchi ni serikali ingawa serikali inatarajiwa itokane (Si lazima iwe hivyo) na wananchi. Neno "bosi" ambalo tumelitohoa toka kwenye lugha ya Kiingereza kwenye Mkutadha wa hoja hii limetumika kuonesha nani anamsimamia nani!!

Tangu Mwaka 1964 hadi 1980 Zanzibar ilikuwa inatawaliwa na Serikali ya mapinduzi Zanzibar, iliyotokana na Mapinduzi ya mwaka 1964, kila Mzanzibari alikuwa ni Serikali? Kuchamba kwingi dada yangu...
 
Back
Top Bottom