Rais nakuomba umteue Joseph Kasheku Msukuma awe Waziri

KWA maoni yangu nadhani musukuma anafaa na Ana uwezo mkubwa wa kuwa waziri. Pale wizarani Kuna makatibu wakuu ambao ni watendaji wakuu wa hizo wizara na pia Kuna wataalam wa wizara pia. Yule musukuma pamoja na la saba yake Ana confidence, na Ana uwezo wa kujenga na kusimamia hoja. Wapo wasomi wengi na wameshindwa kudeliver tulivyotarajia.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Haya Profesa, katika hizo methods zako tatu za justification ya Msukuma kuwa Waziri ili nae aokotwe jalalani, yeye una muweka kwenye category gani?
Najua neno jalala ndilo linakutaabishaka sababu umekariri maana moja. Maana nyingine ni eneo, mahali au sehemu yenye wingi ama utajiri wa almost kila kitu. Ndiyo maana jalala ulilozoea huwa na rutuba tele. Jalala usilolijua pia lina rutuba maridhawa ya maarifa, utajiri, elimu na maadili.
 
Utawala huu kweli ni wa hovyo yaani hata uwaziri umekua cheo cha hovyo hovyo,watu wamesahau ndo cheo kinachosimamia sera zote za maendeleo kwa nchi yetu.
 
Abaki kuwa Mbunge ili aendelee kulijenga taifa kwa uhuru zaidi; akiwa waziri mishughuliko inamwelemea.
Huyu akiwa WAZIRI inabidi naibu na katibu mkuu Wa hiyo wizara wafanye kazi ya ziada.
Acheni kudharau elimu.sio kwamba hao mawaziri waliopo sasa hivi wameshindwa kazi hapana,tatizo ni mfumo Wa utawala Wa chama cha ccm.
 
Elimu ya ngumbaru siku hizi inapigiwa chapuo? basi mpeni na babu yangu uwaziri maana yuko front-line kuhimiza maendeleo pale kijijini na juzi tu hapa aliitisha kampeni ya kuwakamata wachawi wote wanaosumbua pale kijijini.
 
Elimu ya ngumbaru siku hizi inapigiwa chapuo? basi mpeni na babu yangu uwaziri maana yuko front-line kuhimiza maendeleo pale kijijini na juzi tu hapa aliitisha kampeni ya kuwakamata wachawi wote wanaosumbua pale kijijini.
Anafaa sana huyo
 
Baada ya kuchoka na blaa blaa nyingi za hawa watu wanaojiita wasomi (wenye degrees, masters,PhD na maprofessa) naleta ombi kwako Mh Rais JPM umfikirie bwana Joseph Kasheku Msukuma kwenye nafasi ya uwaziri licha ya Elimu yake ya darasa la saba. Kama mtu aliyekwenda darasani kabisa anashindwa kutambua matatizo yanayoikumba jamii inayomzunguka anakwenda kununua gari la milioni 460 huyo ana msaada gani kwa nchi?

Mwingine alijua kabisa kwamba mwezi January 2021 wanafunzi waliomaliza darasa la saba wataingia kidato cha kwanza na kwa kuwa enrolment kwa sasa ni kubwa tulitegemea wanafunzi wa kidato cha kwanza kuwa wengi madarasa, viti na meza vingehitajika kwa wingi. Ni mwezi huu tu wa December ndio viongozi wetu wameliona hilo na kila mmoja anahangaika tu, hilo suala lilipaswa kuonwa mapema na kushughulikiwa huwa wanafanya nini? Facilities zote wanazo, magari, mishahara mizuri, posho nk wanafanya nini?

Leo utamsikia Jaffo anatamka hivi ilimradi anaongea tu ubunifu sifuri kabisa. Afrika Kusini waliwahi kuongozwa na Jacob Zuma mtu ambaye hakupitia hizi formal education za ma PhD, masters nk zinazotufanya tuwe wapumbavu wa kutokujua matatizo ya wananchi wetu na kuona gari la milioni 460 la mtu mmoja ndio bora sana kuliko maji, vituo vya afya, madawa, madawati na viti, ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na madaktari nk.

Kuna mwaka fulani Rais wa Iran Ahmed Nejad aliwajibu wabunge baada ya waziri wake mmoja kubainika kwamba aliforge cheti chake cha PhD ktk chuo cha Oxford uingereza na wabunge kumtaka waziri huyo ajiuzulu.

Rais aliwaambia alimteua huyo waziri kwa sababu ya utendaji wake mzuri wa kazi na siyo kwa sababu ya hayo makaratasi. Ni ukweli ulio wazi hawa watu tunaojidai nao kuwa wana Elimu zao wameshindwa kabisa kudeliver, Ndalichako kafanya nini Elimu?

Hatujachelewa, tujaribu hawa watu kama akina Msukuma wanaweza kufanya makubwa katika maendeleo kuzidi hawa tulionao.
Kwa ni shule hazimhusu raisi ni waziri tu? Kwa ni raising hawezi kufanya chochote? Mbona huwa anabadili mafumizi ya pesa na kupeleka ktk Barbara kwani hawezi kuzipeleka zijenge madarasa.
 
Back
Top Bottom