Pilitoni
JF-Expert Member
- Jul 11, 2011
- 1,190
- 497
Baada ya kuchoka na blaa blaa nyingi za hawa watu wanaojiita wasomi (wenye degrees, masters,PhD na maprofessa) naleta ombi kwako Mh Rais JPM umfikirie bwana Joseph Kasheku Msukuma kwenye nafasi ya uwaziri licha ya Elimu yake ya darasa la saba. Kama mtu aliyekwenda darasani kabisa anashindwa kutambua matatizo yanayoikumba jamii inayomzunguka anakwenda kununua gari la milioni 460 huyo ana msaada gani kwa nchi?
Mwingine alijua kabisa kwamba mwezi January 2021 wanafunzi waliomaliza darasa la saba wataingia kidato cha kwanza na kwa kuwa enrolment kwa sasa ni kubwa tulitegemea wanafunzi wa kidato cha kwanza kuwa wengi madarasa, viti na meza vingehitajika kwa wingi. Ni mwezi huu tu wa December ndio viongozi wetu wameliona hilo na kila mmoja anahangaika tu, hilo suala lilipaswa kuonwa mapema na kushughulikiwa huwa wanafanya nini? Facilities zote wanazo, magari, mishahara mizuri, posho nk wanafanya nini?
Leo utamsikia Jaffo anatamka hivi ilimradi anaongea tu ubunifu sifuri kabisa. Afrika Kusini waliwahi kuongozwa na Jacob Zuma mtu ambaye hakupitia hizi formal education za ma PhD, masters nk zinazotufanya tuwe wapumbavu wa kutokujua matatizo ya wananchi wetu na kuona gari la milioni 460 la mtu mmoja ndio bora sana kuliko maji, vituo vya afya, madawa, madawati na viti, ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na madaktari nk.
Kuna mwaka fulani Rais wa Iran Ahmed Nejad aliwajibu wabunge baada ya waziri wake mmoja kubainika kwamba aliforge cheti chake cha PhD ktk chuo cha Oxford uingereza na wabunge kumtaka waziri huyo ajiuzulu.
Rais aliwaambia alimteua huyo waziri kwa sababu ya utendaji wake mzuri wa kazi na siyo kwa sababu ya hayo makaratasi. Ni ukweli ulio wazi hawa watu tunaojidai nao kuwa wana Elimu zao wameshindwa kabisa kudeliver, Ndalichako kafanya nini Elimu?
Hatujachelewa, tujaribu hawa watu kama akina Msukuma wanaweza kufanya makubwa katika maendeleo kuzidi hawa tulionao.