Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,670
- 22,261
Kuna wazee wastaafu ambao wameondolewa kwenye orodha ya wanaolipwa pensheni ya kila mwezi wakidhaniwa tayari wamefariki! Maafisa wa NSSF wanadai wamewaondoa ili pensheni zao zisichukuliwe na wajanja wao wakiwa tayari wamefariki!
Dhana hii inatokana na wazee hao kutohakikiwa, NSSF iliwajibika kuwapelekea taarifa kama wafanyavyo kwenye malipo lakini haikufanya hivyo kwa sababu wazijuazo wao.
Wengi wa wazee hawa malipo yao yapo kwenye wastani wa shs.250,000/=, Baada ya kujitokeza kwenye ofisi za NSSF wakiwa hao, wameambiwa watalipwa mwisho wa mwezi wa pili!
Wakati wazee hawa hawana ajira nyingine. Mwezi huu tumekuwa tukiwasikia walioko kwenye ajira wakilalamika haki ya kifedha kuwa ngumu kutokana na majukumu ya mwisho na mwanzo wa mwaka, sasa hawa wenye kipato kinacholingana na hela ya matumizi ya mwanafunzi wa sekondari ataishije mpaka mwisho wa mwezi wa pili!
Nilipowahoji NSSF kuhusu taarifa ya kujihakiki walisema ziko kwenye baadhi ya magazeti, japo hawakuweza kusema ni vipi mzee anayelipwa shs.250,000/= anaweza kununua magazeti yote kila siku ili akutane na tangazo la uhakiki wakati NSSF wanazo namba za simu za wazee hao! Ni wazi NSSF wamelichukulia swala la malipo haya ya wastaafu kuwa ni dogo sana na halina maana.
Waheshimiwa, kuna wazee walikuwa wana nauli ya kuwafikisha NSSF makao makuu wakijua watalipwa huko, lakini walijikuta hawana nauli ya kurudi makwao hivyo ikabidi wasaidiwe.
Ni tumaini langu viongozi wa juu mtaona umuhimu wa kulipwa mafao yao ya mwezi wa kwanza kwani chanzo cha tatizo ni NSSF kutojipanga.