GE2025 Rais Mwinyi: Niko Tayari kuheshimu maridhiano na kufanya kazi na upinzani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,608
Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar amesema yuko tayari kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa na kufanya kazi na upande wa upinzani.

Mwinyi ametoa matamshi hayo wakati wa hotuba yake ya kulifungua Baraza la Wawakilishi linaloanza kazi baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Chama kikuu cha upinzani cha ACT Wazalendo kilichoshika nafasi ya pili na ambacho kimedai uchaguzi ulikuwa na dosari bado hakijatoa msimamo juu ya iwapo kitajiunga na serikali ya Umoja wa Kataifa.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilianzishwa visiwani Zanzibar karibu miaka 15 iliyopita ili kumaliza mivutano ya kila wakati wa uchaguzi ambayo athari zake ilikuwa ni pamoja na vifo na uharibifu wa mali.
 
Zanzibar hakuna upinzani miaka hii, awajumuishe wote walioshiriki uchaguzi kwenye hiyo serikali. Kina hamad rashidi na wenzake walambishwe nyadhifa kusiwepo na upinzani wa aina yoyote zanzibar ijulikane hivyo
 
ACT watakubali tu mambo yasiwe mengi, wakikataa ADC wanalamba bingo, sidhani kama watakataa mwito huo kwani kwa sasa hawana mvuto sana kama CUF ya maalimu seif ya wakati ule mpaka kukawa na maridhiano ya kuuna SUK
 
Ha haaa SiASa za Africa.,burudani kweli..yaani unamuibia mwenzio ,then faster unamuomba aje mfanyekazi nyote...na Ijumaa chap Masjid..dah
 
Kajiuliza moto ukiwaka visiwani atatokea njia gani bora awe mpole kdg japo mara nyingi ni sanaa za masisiemu ila zamu hii hawatazichukulia kiurahisi sana kama walivyokua wanamchezea mzee Seif Shariff Hamad
 
Nafasi nne za Ubunge zilizobaki zitatumika kama kete za serikali umoja wa.kitaifa huku kwetu Tanganyika!!

Baadae tutipata serikali rasmi baada ya hii iliyomwaga damu kupoteza uhalali wa.kiroho was kuendelea !!

Mambo ya kimedani !

Nadhani!
 
Wewe unaona 4 positions zinatosha kama kete ya kupoza mambo? Nafasi zenyewe ni kama zinamfunga raisi achague mishangazi ambayo kimsingi itaishia kugonga meza.

Watanganyika wanataka katiba mpya

Haki na usawa

Watu wawajibishwe na kujiwajibisha pale wanapokosea

Ufisadi ukomeshwe n.k

Na sio kuwaza nafasi 4 za uteuzi ndo taka taka Gani hizo?
 
Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar amesema yuko tayari kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa na kufanya kazi na upande wa upinzani.

Mwinyi ametoa matamshi hayo wakati wa hotuba yake ya kulifungua Baraza la Wawakilishi linaloanza kazi baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Chama kikuu cha upinzani cha ACT Wazalendo kilichoshika nafasi ya pili na ambacho kimedai uchaguzi ulikuwa na dosari bado hakijatoa msimamo juu ya iwapo kitajiunga na serikali ya Umoja wa Kataifa.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilianzishwa visiwani Zanzibar karibu miaka 15 iliyopita ili kumaliza mivutano ya kila wakati wa uchaguzi ambayo athari zake ilikuwa ni pamoja na vifo na uharibifu wa mali.

Angaliyatekeleza makubaliano waliyofanya na maalim Seif kwanza ambayo hakutekeleza hata moja, Mwizi mmoja Laanatullahi
 
Wewe unaona 4 positions zinatosha kama kete ya kupoza mambo? Nafasi zenyewe ni kama zinamfunga raisi achague mishangazi ambayo kimsingi itaishia kugonga meza.

Watanganyika wanataka katiba mpya

Haki na usawa

Watu wawajibishwe na kujiwajibisha pale wanapokosea

Ufisadi ukomeshwe n.k

Na sio kuwaza nafasi 4 za uteuzi ndo taka taka Gani hizo?
Ni ngum kunielewa comrade!

Mageuzi yatafanyika kuelekea 2030,mteuzi sio atakaefanya hayo mageuzi!

Kuna nafasi.za kafara zitateuliwa ili kuhalalisha balancing of equations ili mwanamageuzi ashike Dola ambae kwasasa no kivuli.hana meno!!

Umenielewa!!

Kusini kuchele!!
 
Hayo ni matakwa ya katiba yao,awe tayari asiwe tayari
 
Zanzibar hakuna upinzani miaka hii, awajumuishe wote walioshiriki uchaguzi kwenye hiyo serikali. Kina hamad rashidi na wenzake walambishwe nyadhifa kusiwepo na upinzani wa aina yoyote zanzibar ijulikane hivyo
Upinzani wa Zanzibar ulikuwa umejengwa kwenye Maalim (RIP) kupata urais. Mengine yoooote ni maneno tu na sasa hivi wanagawana vyeo tu.
 
Alikudanganya Nani ?
Hakunidanganya mtu yeyote ila nimefanya mchanganuo mimi mwenyewe. Mfano uchaguzi huu wa 2025 upinzani wameshindwa vibaya sana sana (inaonekana CCM wameiba kuliko chaguzi zote) ila wamekuwa kimya wakisubiri ving'ora na teuzi.
 
Back
Top Bottom