Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imemtunuku tunzo ya kuwa mhamasishaji nambari moja wa masuala ya Uwekezaji nchini ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Hasaan Mwinyi kwa mchango wake huo, ulichangia kuinua sekta ya Uwekezaji jambo ambalo limechangia kuongeza idadi ya wawekezaji kwa kipindi kifupi
Tunzo hiyo ambayo iliambatana na utoaji wa tunzo kwa Wawekezaji waliowekeza bila ya kuathiri mazingira, muekezaji wa nje anaefanya vizuri, muekezaji wa ndani, muekezaji katika masuala yanayochangia huduma za jamii, muekezaji mkakati na muekezaji aliechangia kodi kwa kiwango cha juu
Tunzo hizo ambazo ziliambatana na chakula cha usiku zimeandaliwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) zina lengo la kuthamini mchango unaotolewa na wawekezaji nchini ambao unachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi na wanachi wake
Dk. Mwinyi amewahakikishia Wawekezaji hao usalama wa mitaji yao, pamoja na mazingira rafiki ya Uwekezaji ikiwa pamoja na uboreshaji miundombinu, Barbara, umeme na maji
Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Shariff Ali Shariff amesema Sera na Sheria za Uwekezaji zitaendelea kuwa rafiki kwa Wawekezaji anaehitaji kuwekeza nchini, na aliwashukuru Wawekezaji kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika masuala ya kuimarisha Uchumi wa nchi
Aidha Mkurugenzi Mtendaji ZIPA Nd. Saleh Saad Mohamed amesema tunzo hizo ni kuthamini mchango wao, na ZIPA itaendelea kutoa mashirikiano kwa wawekezaji wote ili lengo na madhumuni ya uwepo wa sekta ya Uwekezaji ifanikiwe
Tunzo hizo ziliambatana na Chakula cha usiku kwa wawekezaji ikiwa kutamatisha Tamasha la Uwekezaji Zanzibar 2025 (Zanzibar Investment Summit 2025) na kufungwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi na kuhudhuriwa na Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na watendaji kutoka Taasisi za Umma
chanzo: zipa zanzibar