Rais Museveni kufungua Mkutano wa wafanyabiashara kati ya Tanzania na Uganda

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
Rais Magufuli amemualika Rais Museveni wa Uganda katika ufunguzi wa mkutano mkubwa wa Wafanyabiashara kati ya Uganda na Tanzania ambao utawashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 1000 ambao watapata nafasi ya kujadili namna ya kuongeza biashara mpya baina ya nchi hizi Mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akihamasisha wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza Kwa wingi kushiriki katika kongamano hilo linalotaraji kufanyika Septemba 6,2019 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Bashungwa amesema kongamano hilo litafunguliwa na Rais Yoweri Museven wa Uganda, litahudhuriwa pia na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.

Aidha Waziri Bashungwa ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao wengi wao ndio wamekuwa wakifanya biashara Moja kwa Moja na nchi za jirani hili waweze kupata mtandao mpya wa kibiashara.

Ametaja na kusema muungano wa kimtandao baina ya Tanzania na Uganda utafungua njia mpya ya Biashara hadi Sudan ya kusini ambao wamekuwa wakifanya biashara na Uganda kila uchwao.
 
Ngoja nifuatilie kwa makini uzi huu nione wale wanaofurahia kukamatwa kwa ndege yetu huko SA wanasemaje...utakuta wamekuja na hoja kuwa wafanyabiashara wa Uganda wasusie kuja huku...tehtehtetehtehtehtehteh
 
Kipofu na kiziwi wanapoandaa semina ya safari!!

Uganda wanatuongezea ujuzi was viwanda?! Vya Katerelo ama kachabali?!

Kwa nini sio na Japan,German,China etc?! Huu no ufisadi tu!!
 
Back
Top Bottom