#COVID19 Rais Museveni: Itakuwa ni 'uwendawazimu' kuendesha Uchaguzi wakati wa mlipuko wa virusi vya Corona

RtsHjcq

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,753
5,504
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa itakua ni 'uwendawazimu' kuendesha uchaguzi wakati wa mlipuko wa virusi vya corona.

Ameliambia shirika la habari la Uganda NBS kwamba mipango ya kufanya uchaguzi mapema mwaka 2021 haitakuepo kama virusi vya corona havitadhibitiwa itatakiwa kuangaliwa upya.

Kuna jumla ya visa 122 vya Covid-19 vilivyothibitishwa nchini Uganda.

Mikutano ya umma mkiwemo ya kisiasa imepigwa marufuku kama sehemu ya hatua za kutosogeleana na kukaa nyumbani zilizowekwa nchini humo kwa ajili ya kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona.

Takriban wagombea 24 wametangaza nia yao ya kugombea kiti cha urais na wamewasilisha maombi yao kwa Tume ya Uchaguzi ili kukabiliana na rais Museveni na wameanza mikutano ya kitaifa.

Mikutano hii imeahirishwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Kauli za Bwana Museveni sasa zimeibua swali juu ya ikiwa mchakato mzima wa uchaguzi utaahirishwa au la.

Uchaguzi wa mwaka ujao unatarajiwa kuwa wa mchuano mkubwa hususan kati ya mgombea mwenye umri wa miaka 38 Mwanamuziki na Mbunge Bobi Wine ambaye ameonekana kuwa mpinzani mkuu dhidi ya Bwana Museveni ambaye amekua mamlakani tangu mwaka 1986.

Source: BBC

Shirika la Habari Uganda NBS
 
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema mipango ya kufanya uchaguzi mapema mwaka 2021 haitakuepo kama #CoronaVirus haitadhibitiwa na mipango hiyo itatakiwa kuangaliwa upya
 
Na ukikaribia uchaguzi tutarajie upikwaji takwimu ili ionekane hali ni mbaya kuitisha uchaguzi.
 
Back
Top Bottom