Rais Mstaafu Mwinyi: Watanzania Wamevimbiwa Raha

Rais Mstaafu Mwinyi: Watanzania Wamevimbiwa Raha

Inatakiwa ujue kiswahili fasaha ili ujue anachosema mzee mwinyi Hivi mbona watu wa humu hamna adabu kumsema mzee wa watu aliyeifanyia makubwa nchi yetu? Basi kuweni na shukrani japo mara moja.

yule mzee kajisahau, ccm walivo wavivu wa kufikiri hawataki hata kuhoji kauli za viongozi wao
 
mwinyi kama yeye ni kidume aende kwao zanzibar akatamke haya maneno kwenye wana uamsho. mbona ajificha huku bara watampiga makofi tena

Mkuu, Mwinyi kwao sio ZNZ. Ni wa Mrima huyo.
 
mwinyi hajawahi kuifanyia nchi hii chochote zaidi ya kuuza mali asili zetu akishirikiana na mama siti
 
Hicho kizee kinatakiwa kiulizwe kinapata % ngapi za mgao kutoka iptl... Kwa hiyo yeye hataki watu waongee?
 
huyu mzee mwinyi nampenda sana...maana enzi zake aliiba lakini pia aliwapa watu maisha ya afadhali..ndo maana watu hawakua wanalalamikia utawala wake kila mtu alikua anafaidika...kwa hiyo alikula na wananchi wake..alivokuja mkapa akaona donge kula na wananchi akaamua ale mwenyewe wakati wananchi wanakufa na njaa...
 
Mzee anazeeka vibaya sana huyu. Ndio maana hata vijana wanampiga makofi hadharani tena mchana kweupeeeeee.

rais wa kwanza duniani kupigwa makofi hadharani.

Pole sana mzee rukhsa
.
 
Mzee Mwinyi a.k.a Mzee Ruksa VIDEO LIVE! anauliza Watanganyika na Wazanzibari wanaosema ''SISI HATUUTAKI MUUNGANO' wamepata wapi ruksa toka kwa Watanganyika na Wazanzibari kuwasemea wote kwa ujumla?



Video kwa hisani ya Tangibovu wa Youtube.
 
Last edited by a moderator:
Rais Mstaafu anaamini watanzania wana raha sana, kwamba raha waliyonayo watanzania ni nyingi kupita kiasi, anasema sasa ni kama wamevimbia ndio maana wanaongeaongea sana.

Source: TBC Habari.

MyTake:
Hawa viongozi wakiwa wanapita barabarani wanasafishiwa njia, hawajui adha ya mfumuko wa bei wala ukosefu wa ajira maana yake nini, Mwinyi kajisahau.

kuna nchi watu walikua na njaa sana, kulikua hakuna mke wa mfalme alipoulizwa kuhusu njaa za watu, kwa mshangao akasema sasa kama hawana mkate si wale keki? naomba Mh Rais mstaafu ndicho kitu anafanya, kajisahau sana!

Raha? Raha gani? yeye si ndo anayekula raha! yeye sio rais lakini bado anasafishiwa njia wakati sie wengine tuko kwa foleni ili yeye apite (by the way nachukia sana hii system ya kusimamishwa foleni masaa hili hawa jamaa wapite na wanalofanya halionekani zaidi ya ufisadi, dharau na kutucheka, etc) sasa huyu jamaa kwa kweli kajisahau mpaka anatudharau!!
 
Mwalimu Nyerere hakukosea aliposema anashauriwa na mkewe namna ya kuongoza taifa!! pia mwalimu alisema rais wetu ni dhaifu tumvumilie amalize muda wake rejea kitabu cha mwalimu!!
 
Kama sikosei alisema wanaosema sisi hatuutaki muungano nani kawatuma wamuongelee kila mtu? Wasiotaka muungano wamevimbiwa raha...
 
Nadhani Mzee Mwinyi alisema maneno hayo wakati wa zile vurugu za wana-Uamsho kule Zanzibar wiwki iliyopita. Kama ndivyo namuonea huruma huyu mzee Ruksa. Yeye na viongozi wenzake kutoka Zanzibar ndio wanachochea watu wafanye fujo za kuua Muungano amini usiamini. Lakini pia sio siri wanaofaidi huo Muungano ni wao hao Wazanzibar. Nimepata bahati ya kufanya kazi kwa muda huko miaka ya nyuma kwa Taarifa tu kwa wana JF; Simenti yatoka Bara, Mbao kwa wingi kutoka bara, Chakula chatoka bara; Mimi mwenyewe nilikuwa napeleka kiti moto wawili kila nikipanda ndege ya kukodi niliyokuwa natumia twice a week kutoka mkoa mmoja wa pwani bara kwenda Zenji na huko inanyang'anyiwa mno na wateja ni kibao kuliko huku Bara na of course the price was too good; Bia of course zatoka Ilala ndio maana walipofanya vurugu wakawa wanakimbilia kunywa bia wakati wanavunja mabaa. Viongozi zanzibar ndio chanzo cha kutaka kuvunja Muungano wetu jamani uliodumu kwa hii miaka yote. Watu wa kawaida hawana tatizo na huu Muungano. Leo ingekuwa Rais ni Mkristo Uamsho wangekuwa na agenda ambayo ndugu zangu wa bara mngeshindwa kuitetea. leo hii Raisi na Makamu Muislaam. Huku bara hakuna anayelalamika ila angekuwa Mkristo na Makamo Zanzibar wangepiga kelele na usingeshangaa hata mtu kama Shamuhuna angekuwemo kwenye hizo kelele. Mbona sisi wa bara tumenyamaza? Sasa huu Muungano nawahakikishia utafia mikononi mwa JK na hasa alipozuia kujadili Muungano siku alipoapisha Tume ya Katiba. Binafsi siungi mkono kuvunja Muungano lakini hawa wenzetu wa Zanzibar waking'ang'ania jamani tuwaache wende zao kwani mtu akiomba talaka mpe atafute kidume kingine chakutosheleza labda wewe shakuwa kaputi mzee.
 
Back
Top Bottom