Rais Mstaafu Dkt Kikwete Atunukiwa Shahada Nyingine Ya Udaktari wa Falsafa

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,824
WanaJF,

Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametwaa shahada nyingine ya PhD katika masuala ya mahusiano ya kimataifa ya chuo kikuu Huria Tanzania.

Shahada hiyo imetolewa kwake na chuo hicho kupitia kwa chancellor wa chuoni hapo, Dkt Asha Rose Migiro, baada ya chuo hicho kujiridhisha na utendaji kazi wa rais huyo mstaafu katika masuala ya diplomasia na mahusiano ya kimataifa.
 
Ni ajabu na kweli,hizi elimu za kutunukiwa ni bure.Unaweza ukawa kilaza ila team yako ya ushauri ikawa vizuri,matokeo yake ukawa unatunukiwa tu hata kama ni kilaza.
 
Aisee!
Hii nchi kazi sana!
Kwahiyo Migiro analipa fadhila za kubebwa mpaka top five kwenye uteuzi wa mgombea urais CCM kwenye yale majina ya mfukoni?
Basi sawaa mkapa naye aamuru udom impe u profesa!
 
Degree yenye thamani kubwa ni first degree ambayo yeye alizungusha, degree zinazofuata huwa ni mbwembwe tu.
 
Hiyo ndio shahada pekee aliyotakiwa kutunukiwa JK ni mtu wa diplomasia ata kwa kauli zake tu; kama naona uko Msoga sasa hivi joho lake linapigwa pasi na kofia inafutwa vumbi maana katika hafla kama hizi JK huwa anakwenda mwenyewe kupokea tena fully dressed for the part.
 
WanaJF,

Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametwaa shahada nyingine ya PhD katika masuala ya mahusiano ya kimataifa ya chuo kikuu Huria Tanzania.

Shahada hiyo imetolewa kwake na chuo hicho kupitia kwa chancellor wa chuoni hapo, Dkt Asha Rose Migiro, baada ya chuo hicho kujiridhisha na utendaji kazi wa rais huyo mstaafu katika masuala ya diplomasia na mahusiano ya kimataifa.

Zikiwaishia hizo wanazompa,waje wachukuwe ya kwangu nayo wampe.Siku hizi shahada za heshima zimepoteza maana kiasi cha kuwafanya watu makini wenye sifa za kupokea"tuzo"hizo kutokana na michango yao katika jamii,kujiuliza mara mbili kabla ya kupokea tuzo hizo.
 
"Asaha Rose Migiro kumtunuku Kikwete shahada"!!!!!!!!!!! Nchi hii ni ya ABUNUwasi,hakuna lisilowezekana! Kesho mtasikia jamaa katunukiwa shahada na chuo cha SANAA cha Msoga!
 
WanaJF,

Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametwaa shahada nyingine ya PhD katika masuala ya mahusiano ya kimataifa ya chuo kikuu Huria Tanzania.

Shahada hiyo imetolewa kwake na chuo hicho kupitia kwa chancellor wa chuoni hapo, Dkt Asha Rose Migiro, baada ya chuo hicho kujiridhisha na utendaji kazi wa rais huyo mstaafu katika masuala ya diplomasia na mahusiano ya kimataifa.

Bwaha bwaha bwaha bwahaaaaaaa. Na nyingine tena???. Nadhani sasa Title mpya "dr dr dr......"
 
Vyuo vyetu vingi vimepoteza hadhi, hata wahitimu wengi wa vyuo vikuu wanawelewa mdogo,hawajiamini na utendaji wao ni duni usiokuwa na fikra yakinifu...
wanachoweza zaidi ni kufatilia miziki/tamthilia,kuvaa vimini/ vimodo,kunywa pombe,disco na kupigana pini(kukaa ki pea).
Nahisi vinaongozwa kisiasa na kimaslahi ya fedha, vingine vinajidhatiti kidini na kuacha maslahi mapana ya kuwajengea vijana /wahitimu hari ya taaluma,ufanisi,utendaji na kujiongoza.
Hata vikinipa uprofessa sitashtuka maana vinamaprofessa ninaoweza kuwafundisha kazi wanayoifanya.
 
Zikiwaishia hizo wanazompa,waje wachukuwe ya kwangu nayo wampe.Siku hizi shahada za heshima zimepoteza maana kiasi cha kuwafanya watu makini wenye sifa za kupokea"tuzo"hizo kutokana na michango yao katika jamii,kujiuliza mara mbili kabla ya kupokea tuzo hizo.
Ulitaka apewe Lowassa?....Teh teh teh...Hakuna tuzo za ufisadi Bongo wala shahada ya heshima kwa ufisadi...Subirini zikianzishwa kule Monduli atapewa hilo fisadi lenu.
 
hata haoni aibu , Dr Tulia mwenyewe mtoto mdogo kampita mbali kielimu , bado PhD ya kigodoro nayo apewe.......Magufuri usikubali hii elimu ya kupewa pewa hovyo
 
Ulitaka apewe Lowassa?....Teh teh teh...Hakuna tuzo za ufisadi Bongo wala shahada ya heshima kwa ufisadi...Subirini zikianzishwa kule Monduli atapewa hilo fisadi lenu.

muwe na aibu ndo rais mburura anayeongoza kupewa pewa PhD za vigodoro
 
Ulitaka apewe Lowassa?....Teh teh teh...Hakuna tuzo za ufisadi Bongo wala shahada ya heshima kwa ufisadi...Subirini zikianzishwa kule Monduli atapewa hilo fisadi lenu.

Sasa Mh.Lowassa anaingiaje kwenye mazingaombwe haya?Kweli Lowassa ni "kichomi" kila mkigeuka mnapigwa cha mbavu.
 
Back
Top Bottom