Rais Mkapa ana ugomvi na Kiswahili chetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Mkapa ana ugomvi na Kiswahili chetu?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Al Zagawi, Mar 17, 2012.

 1. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Wadau,

  Majuzi hapa wakati wa-Japan wanakumbuka wenzao walipoteza hali, mali na nafsi katika tsunami ya mwaka uliopita Mh Rais Mkapa alikuwa ni katika wageni waalikwa ambao walikaribishwa jukwaani na kutoa hotuba. Balozi wa Japan hapa nchini alikuwa ni mwenyeji katika hafla hiyo pamoja na wageni wengine kadhaa.

  Kilichonishangaza ni kuwa Raisi Mkapa alipokaribishwa jukwaani, alitoa hotuba yake kwa ki-ingereza(sijui kama ni english phobia au laa) wakati mwenyeji wa shughuli, balozi wa Japan, alitoa hotuba yake kwa Kiswahili.

  Ni kwa mantiki hiyo nauliza swali hili je, mh sana Ben Mkapa ana nini na kiswahili chetu, hakipendi au ni vipi?

  Nauliza nikiwa na kumbukumbu kuwa wakati fulani akiwa madarakani, alikwenda Addis Ababa kuhudhuria mkutano wa AU. Wakati huo AU ilikuwa imetoka kupitisha azimio la kuruhusu hotuba za wakulu kutolewa kwa kiswahili, mh Mkapa alichagua kutumia kingereza lakini Joachim Chissano akatumia kiswahili kwa muda wa kutosha na baadae ki-reno.

  Hivi kuna aibu gani ya Rais Mmachinga, Mndengereko, Mchaga, n.k. akatumia kiswahili katika kutoa hotuba huko ughaibuni? Hivi pasi na juhudi za makusudi za wakiwemo watawala(usiseme viongozi maana hakuna njia wanayotuongoza kuipita), hiki kiswahili kitakuwa kweli.

  Kuna lugha inaitwa Fursi...inaongewa na taifa moja tu duniani, Iran na bado Ahmadinejad anatamba nayo mpaka UN.

  Hivi, ni kweli kuwa tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele au ni porojo za alinacha kama kawaida yetu.
   
 2. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Mkapa ni Mkapa tu !
   
 3. k

  kiparah JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Hata mi siwezi kutoa hotuba ya maana kwa Kiswahili, maneno yake marefu-marefu!
   
 4. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sema "Rais mstaafu"
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Kiingereza pia ni lugha rasmi Tanzania. Swali linakuja, audience ya hiyo hotuba ilikuwa ipi? Ilikuwa ya Wajapani wengi na watu wa diplomatic corps za nchi mbalimbali walio Tanzania? Kama ni hivyo inawezekana Mkapa aliweka nyuma nationalistic pride kwa kutaka kuipa umuhimu practical issue ya kutaka kueleweka kirahisi zaidi na watu wengi.

  Kama audience ilikuwa ya waTanzania ambao wengi wao hawajui kiingereza then swala la practicality linatoka, inaonekana labda kapendelea Kiingereza tu.

  Tatizo la Mkapa hata akiongea Kiswahili kwa watu wa kawaida ataanza kuwaambia habari za "kuboresha wigo wa hadidu za rejea za asasi za washikadau kwenye mustakabali wa kukarafati miundombinu kama ilivyoainishwa na MKUKUTA", atawapoteza diplomats na Watanzania.

  Balozi wa Japan kutoa hotuba Kiswahili ni moja kati ya njia za kidiplomasia kuonyesha heshima kwa Watanzania.
   
 6. m

  mtafungwa Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kwamba hana ugomvi na lugha ya Kiswahili. Kinachomfanya asitumie Kiswahili katika mikusanyiko ya kimataifa huenda ni fikra kwamba wengi hawawezi kumwelewa. Nasema hivyo kwa sababu yeye ni mzalendo (nasema yeye kama yeye) kwa hiyo hawezi kuwa na nia mbaya na lugha ambayo yeye mwenyewe ameshiriki sana kuipamdisha chati kile kipindi akiwa mhariri wa magazeti ya serikali...
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Nitoe Sifa moja ya Mkapa ninayoijua tangu akiwa waziri wangu pale Mambo ya Nje.

  "mkapa anadharau sana watu wasiojua Kingereza fasaha , Daima huwapuuza watu wanaongea broken English na daima mtu huyo hana nafasi kwa mtazamo wa huyo Mmakonde"
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Kuna m-sure mmoja alikuwa anamsifia sana Mkapa akisema kwamba Mkapa anaongea Kiingereza kizuri kumpita mtu mwingine yeyote serikalini, sijui aliwasikiliza wote?

  Story ya ascent ya Mkapa kutoka Daily News kwenda Mambo ya Nje ilianzia pale Ibrahim Kaduma aliposhindwa kuongea kiingereza na Henry Kissinger wakati wa ziara ya Kissinger Tanzania, bahati nzuri Mkapa alikuwa pembeni ndiye aliyekuja kuokoa jahazi. Inasemekana Kissinger alikuwa anaongea kiingereza cha diplomasia kwa sana (mtu anaweza kukwambia "water closet" huku akimaanisha chooni, unabaki kuuliza "water what?") na Kaduma hakuona ndani. Nyerere akaona bora nimpe shavu tu mwanafunzi wangu Ben.

  Mkapa ana sifa ya ubabe na dharau. Dharau si nzuri. Kama hii habari ya dharau iko limited kwa Foreign Affairs officials, hakuna sababu ya mtu kuwa a foreign affairs official wakati lugha ya kimataifa (ukiondoa Kiswahili) inayotambulika kama lugha rasmi Tanzania, Kiingereza, huifahamu. Mimi ningetegemea hawa officials wajue kwa ufasaha lugha kadhaa za kimataifa, sio Kiingereza tu. Alishakuja Omar Bashir Tanzania, akaleta hizo habari za "mie naongea cha kwetu Kiarabu tu". Foreign affairs bado kidogo aibu wakose interpreter, ndipo akajitokeza Dim (the young Turk is reputed to master six international languages) akaokoa jahazi. Sasa hatutaki kuwa na officials MOFA wasiojua lugha za watu.

  Lakini kutojua Kiingereza hakuna maana mtu hana uwezo sana
   
 9. m

  mwanakaya Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Hahaha na ubinafsishaji wa mashirika kwa nchi wahisani
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Serikalini including Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam? Kama ni hivyo basi kuna wakufunzi nawajua pale (wengi wao ni wastaafu sasa hivi) ambao wanaijua vizuri kabisa lugha ya Kiingereza ambapo nina shaka kama huyo mshua aliwahi kukutana nao.

  Ningetaja majina lakini itakuwa si freshi ila kwa wale wachache wanaojua wanaweza at least ku guess mmoja wao ni nani....

  Ila hiyo ya Mkapa kupenda Kiingereza na kudharau wasiokijua vizuri ni kweli. Mimi nakumbuka wakati yeye ni waziri wa elimu ya juu nilikuwa naenda sana pale wizarani ofisini kwake na baadhi ya wale wadingi waliokuwa chini yake baadhi yao walikuwa wana struggle sana kuwasiliana naye.
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Katika kuendeleza lugha ya Kiswahili, tujitahidi sote kuepuka makosa yanayoonekana kuzoeleka

  Swala =Suala
  Swali= Suali
   
 12. m

  mtafungwa Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa kama anadharau wasiojua vizuri lugha ya kiingereza, naona tabia hii si njema. Nadhani ningemuelewa vizuri saana kama angemdharau msomi asiyejua vizuri kiswahili.
   
 13. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Viongozi wetu wengi bado wana kasumba ya kikoloni na hawajiamini kabisa pale wanapokutana na wazungu. Hii nimeishuhudia ndani na nje ya Tanzania, tena hata kwa huyo Mkapa.
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Wewe utataka kutusemesha cha Unguja wengine tutataka kusema cha Kisangani. Chote Kiswahili.

  Umenikumbusha nilikuwa nagombana sana na ndugu yako asiyependa kuwakirimu watoto wa ami zake(wakija pale nyumba nyeupe Ocean road akijifanya kalala, kisa kulewa ukaizari). Kiswahili chake cha Unguja, ukiandika "Mwalimu" yeye anasema si sahihi, ni "mualim" tena bila ile "u" ya mwisho.

  Nikamwambia rudi kwenu Unguja, kwani unafikiri tuko madrasa hapa.Huku natania nusu tu.
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hahaha huyo ndugu yangu ulikuwa na ajenda ya siri nae tu, ukashindwa kumwambia ukamfukuza. Tungekuwepo tungekuimbia "wafanya kisebu sebu, na kiroho kipo papo"

  Hakuna suala la lahaja kwenye hili. Kama ni makosa ni makosa tu. Kwenye kamusi hakuna "swala" zaidi ya "mnyama mfano wa paa"

  "swala hili" ni makosa kisarufi hata kama ulikuwa unamzungumzia paa kweli
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Mjini Magharibi na Mrima wapi na wapi?

  Ukitaka hivyo hata "Swali" badilisha ufanye "suali" na maadamu tunaongelea hili, hata jina lenyewe la lugha liwe Ki-suahil.

  Mzizi wa swali na swala ni mmoja, habari za "suala" ni kukiarabisha Kiswahili. Na mie kama mtu ninayeamini kiarabu hakina hati pekee ya ugavi wa Kiswahili (au Kisuahil ?) na Kimang'ati nacho kina cha kuchangia, naondokana na hizo habari za kwamba "suala" ni sahihi zaidi ya "swala".

  Nakataa kwamba Kiswahili kinatakiwa kukikumbatia kiarabu kuendelea mbele ili kiwe na maana, na kusema kwamba "swala" si sahihi bali "suala" ni sahihi, ni kukinyima Kiswahili sifa yake kubwa ya kuwa lugha ya kisikio (phonetic language).

  Kama kamusi yako inasema "swala" siyo sawa na "suala" ndiyo sawa hata yenyewe haiko juu ya darubini ya Kiranga. Kamusi zinakosea nazo, au maneno yanabadilika, ndiyo maana unaona matoleo yanabadilika.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Neno "swali" (question) lipo kwenye kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI, toleo la kwanza, 2001.

  Na "swala" ni prayer na gazelle. Suala ni "issue".
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Mitaa ya Mwembetogwa "maswala" ni vipipi vya mateja, kwa hiyo naweza kuwa naongea Kiswahili cha Mwembetogwa vile vile.
   
 19. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,122
  Likes Received: 1,209
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni kasumba, si unaona hata wasanii wa bongo fleva wanaona shida kuimba Kiswahili matokeo yake wanaboronga na kiingereza cha hajabu. Kwa kifupi usishangae Mkapa kujifanya anajua sana kiingereza hii ni tabia yetu watanzania tunapenda sana sifa za kijinga.
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Sio habari ya usahihi zaidi wa "suala" dhidi ya "swala." Ni suala la kuwa "swala" haiwezi kutumika badala ya "suala" hata kidogo. Ni makosa.

  Kiarabu hakina haki pekee, hilo ni kweli, lakini kwenye "suala" badala ya "swala," tayari TUKI imeshaipatia haki hiyo, kwa hiyo wewe Kiranga subiri kwenye neno jengine, kwa hili umenoa
   
Loading...