Hamis Mwinjuma ametoa wito kwa waswahili kukitazama Kiswahili kwa jicho la fursa

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ametoa wito kwa waswahili kukitazama Kiswahili kwa jicho la fursa na kuwa wepesi kung'amua kila upenyo kwa lugha hiyo na kuhakikisha inafaidisha kwakua inatambuliwa, inathaminiwa na kuaminiwa Duniani.

Mhe. Mwinjuma ametoa wito huo leo Agosti 9, 2023 jijini Mwanza alipofungua Kongamano la sita la Chama cha Lugha na Fasihi ya Kiswahili Tanzania (CHALUFAKITA).

Amesisitiza kuwa ni wakati wa kila mtumiaji na mtaalamu wa Kiswahili kuweka bidii ya kubuni namna ya kunufaika na Kiswahili. Kwa wale wenye kuandika vitabu vyenye maarifa ya ngazi mbalimbali wafanye hivyo na wenye uwezo wa kubuni na kuandaa kazi mbalimbali za kitamaduni wafanye hivyo pia.

Mhe. Mwinjuma ameongeza kuwa ni muhimu kwa waswahili kuweka bidii katika kujifunza na kutumia mifumo, nyenzo na majukwaa ya kidijiti katika kuandaa, kutangaza na kuuza kazi au mazao ya Kiswahili.
IMG-20230809-WA0027.jpg
 
Back
Top Bottom