Rais Magufuli yashamshinda?

Rais Magufuli yashamshinda?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,148
Reaction score
137,142
Hivi ni mimi tu au na wengine mpo mnaoona kama vile mambo yashamshinda huyu Magufuli?

Kuna hali fulani hivi naiona ambapo jamaa ni kama anaamka tu kila asubuhi na kutoa maamuzi ya kukurupuka kurupuka.
Yaani yeye ni amri tu....fanya hivi....fukuza huyu....twende kule...nk.

Yapo baadhi ambayo ni mazuri ambapo mtu unaona kabisa hapa nia ni nzuri lakini kuna mengine yenye ukakasi sana hadi kunifanya nianze kuhoji hekima na busara za huyo bwana!

---
Mimi ni mmoja wa watu wanaoamini kuwa rais wetu huyu, mheshimiwa mtukufu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli si kiongozi mzuri hata kidogo, hususan katika ngazi ya urais.

Hilo nimekuwa nikilisema kwa muda mrefu sasa. Nakumbuka hata ile siku alipoteuliwa kuipeperusha bendera ya CCM nilisema hivyo humu humu JF.

Kwa kiasi fulani namkubali kwenye usimamizi lakini si kwenye uongozi. Hana kabisa haiba ya kiuongozi. Pia hana sifa za kuweza kuwa kiongozi mzuri.

Ni mtu mwenye jazba. Ana jeuri. Mwenye kuongea bila kufikiria athari za maneno yake[nyakati zingine]. Wengine wanasema eti kuwa hashauriki. Kwa ufupi ni mengi sana yanasemwa juu yake kiasi kwamba mengine ni vigumu kwa watu wa mbali kama sisi kujua kama ni ya kweli au la. Hivyo kwa sisi wa mbali tunaenda na yale tuyaonayo na tuyasikiayo toka kwake yeye mwenyewe.

Sasa kwa jinsi vile mambo yanavyoenda sasa hivi kuna kila dalili huenda nchi imeshamshinda kuiongoza. Hivyo ndivyo niuonavyo mwelekeo.

Hata ndani ya chama chake ukiangalia vizuri utaona nyuso nyingi tu za manung'uniko toka kwa wakereketwa. Wengi wao siku hizi wanashindwa hata kumtetea. Wapo kimyaaaa utadhani wagonjwa. CCM hawana furaha kabisa.

Naamini asipojiangalia na kujifanyia tathmini basi hiyo kazi itamshinda kabla hata hajafikia nusu ya muhula wa hii miaka mitano.

Niliwahi kuandika kuhusu 'a police state'. Jikumbushe....

https://www.jamiiforums.com/threads/a-police-state.1105346/#post-17414170
 
Hivi ni mimi tu au na wengine mpo mnaoona kama vile mambo yashamshinda huyu Magufuli?

Kuna hali fulani hivi naiona ambapo jamaa ni kama anaamka tu kila asubuhi na kutoa maamuzi ya kukurupuka kurupuka.

Yaani yeye ni amri tu....fanya hivi....fukuza huyu....twende kule...nk.

Yapo baadhi ambayo ni mazuri ambapo mtu unaona kabisa hapa nia ni nzuri lakini mengine yana ukakasi kidogo.
Mkuu sasa hivi wananchi hatujui kesho ataropoka nini, sasa nimeelewa ni kwa nini mzee kitwanga na mama Kilango malecela wapo kimya
 
CHADEMA ingekuwa imara kama zamani huyu easily angeondoka 2020
Lkn kwa upinzani huu wa hovyo hovyo wa kutowasikiliza wanachama na kujiona viongozi kama Mungu watu
Wapinzani wanawatumia wanachama wao kwenye maadamano tu
Kwenye teuzi wanapuuzi kauli za wanachama wa kawaida
Wao na CCM hamna tofauti
Magufuli atashinda 2020 hata kukiwa na TUME HURU
Mark my words
 
Na kwanza tuliosema huyu ni One term president inawezekana hata asikamilishe One Term

Ofcourse sio lazima akae madarakani miaka 5.

Laiti kama tungekuwa na chaguzi huru na haki
laiti kama tungekuwa na tume huru ya uchaguzi....
na vingekuwepo hivyo vyote hata yeye asinge endesha mambo hivi
angekumbuka wapiga kura wanamsubiri 2020...

right now hata tufanyaje....atabaki Rais hadi 2025 unless itokee 'intervention'
 
Ukipita mitaani watu washachoka na story zake...
biashara haziendi.....mood iliyopo ni kusubiri labda mambo yatanyooka soon...
sasa sijui yasiponyooka itakuaje....

Halafu mbona mji bado ni mchafu mchafu tu....

20160608_174630.jpg
 

Attachments

  • 20160608_174630.jpg
    20160608_174630.jpg
    338 KB · Views: 172
Back
Top Bottom