Rais Magufuli wewe ni Rais wa wanyonge wapi??

Rais Magufuli wewe ni Rais wa wanyonge wapi??

Nimekuwa nikiumia sana na nchi yangu kwa mambo yanayoendelea !!

Rais Magufuli nipo hapa leo kuongelea mwenendo wa nchi yetu kwenye suala la kiuchumi!!!

Suala lako la kubana matumizi ni zuri lakini unalifanya liwe gumu kwa wananchi wako jinsi unavyochukua hatua!!

Hatua zako hazionekani kuwa za kisayansi kufanya utafiti kuwasaidia wananchi wa kawaida!!!

Riba ya Mabenki
Mh : Riba ya mabenki yetu ipo juu mno kiwango ni 24%-30% kwa mwanachi wa kawaida mfano ukikopa 10,000,000 atatakiwa alipe milioni 13,000,000 sasa hiyo liba ya milioni tatu ndio inawezekana ikawa faida kwenye biashara mtu anayoifanya lakini yote anairudisha kuilipa kama Riba !!

Wewe bado ujaliona hilo lakini Jirani yako Uhuru Kenyatta ameliona hilo kaamua kusaini mswada wa sheria kupunguza Riba ya mabenki kutoka 22%-24% na kuwa 10.5%-14.5 wewe bado hata swala la mabenki hakuna siku nimesikia ukiliongelea!!

Uwezi kujenga uchumi bila kuimulika sector ya mabank Tanzania!!

Sasa hivi kuna vijana wanaitimu Chuo kikuu walitakiwa kukuta Riba imeshushwa ili watumie vyeti vyao vya kuitimu kukopea pesa kwenye mabenki ni kitendo cha kuweka Sera wewe upo kimya !!!

Tatizo la Ajira litaisha vipi kama waitimu wa vyuo vikuu watamaliza vyuo bila kupata mikopo ya kujiajiri na kuajiri wenzao wa Form 4&6?

Tatizo la Ajira tunalitengeneza sisi wenyewe wala hatutakiwi kutafuta mchawi wachawi ni sisi wenyewe!!!

Mbona mswada wa mahakama ya mafisadi uliwaiswa kupelekwa bungeni ingawa hata hatuoni ukifanya kazi ??

Kwanini tusipeleke mswada wa kupunguza Riba tukaacha kuwakamua Watanzania na kuwavutia waitimu wa vyuo vikuu wajiajiri wenyewe?

Kila mwaka tunasikia mabank kama Crdb,Nmb wanatangaza faida ya billions of money, hiyo faida kwanini hata nusu yake isipunguziwe kwenye kushusha Riba ya mabenki ili kuwasadia waitimu wa vyuo vikuu na wawekezaji wa ndani!!

Bado Mimi sijaelewa Mtukufu Rais Magufuli wewe ni Rais wa wanyonge wapi??
Hiyo lugha ya wanyonge inasemwa kwa ajili ya kuwafanya wanyonge wabweteke Ili wanyongwe vizuri.
 
Ulishawahi kuona mnyonge wa wapi anaenda kukopa benki million 10??

Majizi Chadema mtapayuka sana lkn safari mmebanwa kwenye kona .mtanyooka tu

Sisi watoto wetu wanasoma bure
Wewe ndio ujui lolote kaa kimya no sense upuuzi ?
Nani kakwambia Mimi ni chadema yaani mtu akiongea tofauti na tumbo lako linavyowaza wewe unakuja kasi kumuita chadema ?

Wewe ni k.laza wa Lumumba wala aunisumbui .?
Milioni 10 nimetoa kama mfano hata wewe ukikopa laki3 liba ni ileile wala haibadiliki!!
Baada ya kupambana nahoja unaleta mambo ya vyama ??
Hivi huyo mtoto wako anayesoma bure wakati anaenda shule bila kunywa chai kwa sababu una sukari unategemea ataenda wapi zaidi ya kumaliza shule na kwenda kuosha office za Lumumba?

Think using brain sio tumbo!!!
 
Umeangalia upande mmoja wa riba. (Hakimu mzuri mtenda haki hufanya maamuzi kwa kuangalia pande zote 2)

Riba, VAT kwa miamala ya simu na bank, mfumuko wa bei za bidhaa na kushuka sana kwa bei ya mavuno shambani.
(Hivi ni vinamuumiza mtu wa hali ya chini vinahitaji marekebisho)..

Usimamizi wa kodi stahiki kwa makampuni na wafanyabiashara wakubwa, uongozi wa serikali thabiti km kwenye halmashauri kwa wakubwa na wadogo, kuzuiwa kwa mitandao ya madawa ya kulevya kwa kukamatwa wahusika wakubwa, kupungua kwa mianya ya rushwa na kubana matumizi kwa baadhi ya shughuli km safari za nje( haya ni baadhi yanamuumiza mwenye kipato cha juu tofauti na alivyozoea awamu zilizopita)

Elimu bure kwa waliokuwa hawana fedha kusomesha watoto wao, usimamizi, uwajibikaji na ufuatiliaji kwa madaktari na walimu, umakini ktk hospitali, ununuzi wa vitanda na huduma kwa wagonjwa na wajawazito, kuondolewa kwa ushuru na tozo ndogo ndogo kwa wafanyabiashara wadogo wa mbogamboga na mama ntilie (haya ni baadhi ya kutetea wanyonge)

Riba ikiwa kubwa hata mwenye kipato cha juu pia kina muumiza na kinamuathiri pamoja na serikali yenyewe.
 
Sawa lakini kuna kuwa na mambo ya msingi ambayo yanakuwa wazi kabisa lakini uoni akiyaongelea!!!

Mimi mfano swala la kuzuia madawa ya kulevya aliniusu moja kwa moja maana sitakaa nitumie !!!
Naongelea jambo linalowagusa watu walio wengi!!
 
Subi ri mambo yatakuwa sawa. Bado anapanga vema serikali yake. Tumpe muda
 
Subi ri mambo yatakuwa sawa. Bado anapanga vema serikali yake. Tumpe muda
Muda gani mwaka unaisha ?
Sawa lakini kuna kuwa na mambo ya msingi ambayo yanakuwa wazi kabisa lakini uoni akiyaongelea!!!

Mimi mfano swala la kuzuia madawa ya kulevya aliniusu moja kwa moja maana sitakaa nitumie !!!
Naongelea jambo linalowagusa watu walio wengi!!
 
Sawa lakini kuna kuwa na mambo ya msingi ambayo yanakuwa wazi kabisa lakini uoni akiyaongelea!!!

Mimi mfano swala la kuzuia madawa ya kulevya aliniusu moja kwa moja maana sitakaa nitumie !!!
Naongelea jambo linalowagusa watu walio wengi!!
Madawa ya kulevya pia raisi anawatetea wanyonge kwa sababu vijana mtaani ndio waathirika wakubwa km mateja, wezi, ujambazi na ubakaji vinawaathiri wanyonge wengi wao wameingia kwenye hili kupitia madawa ya kulevya.

Raisi anapozuia mtandao wa madawa ya kulevya kwa kumata wafanya biashara hao wakubwa moja kwa moja inakwenda kuleta impact kwa wanyonge, hawataibiwa mali zao, biashara haramu zitapungua, afya, amani na maendeleo yatapatikana kwa wanyonge.
 
Leo Ukimtumia bibi yako kijijini sh 200,000/ kwenye simu, ajiandae kukatwa sh 5,000/. Huyu ndo maskini ambaye anatakiwa rais kumfikiria
Na wakati huo huyo bibi ulie mtumia 200,000/= ataenda kukatwa 5,000/= na kisha atapokea 195,000/=.
Hapo ni baada ya wewe kukatwa 5,000/= wakati unatuma.
Sasa hapa ndipo wananidanganya kwamba ukituma unalipia na ukipokea unalipia.
Hii inamaanisha kwenye transaction moja unalipa kodi mara mbili.
Huu ni upuuzi kabisa [emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
Wewe ndio ujui lolote kaa kimya no sense upuuzi ?
Nani kakwambia Mimi ni chadema yaani mtu akiongea tofauti na tumbo lako linavyowaza wewe unakuja kasi kumuita chadema ?

Wewe ni k.laza wa Lumumba wala aunisumbui .?
Milioni 10 nimetoa kama mfano hata wewe ukikopa laki3 liba ni ileile wala haibadiliki!!
Baada ya kupambana nahoja unaleta mambo ya vyama ??
Hivi huyo mtoto wako anayesoma bure wakati anaenda shule bila kunywa chai kwa sababu una sukari unategemea ataenda wapi zaidi ya kumaliza shule na kwenda kuosha office za Lumumba?

Think using brain sio tumbo!!!
Ukibishana na huyo utakuwa unaumiza kichwa chako tu
 
1472113017959.jpg
 
Back
Top Bottom