Rais Magufuli wewe ni Rais wa wanyonge wapi??

Rais Magufuli wewe ni Rais wa wanyonge wapi??

Wanyonge ndio tumekandamizwa kabisa , maana ajira kasitisha kwa madai ya kutozidi miez 2 lakin mpaka sasa ni miezi 2+

Watoto wa matajir hawawez umia kivile maana kama ni mitaji watapewa na wazazi wao na ndugu zao

Masikin tumebaki tukiumia ukizingatia na bei ya mazao kama huku kwetu ni hatari iko chin mno , mbaazi bei ni mbaya kuliko mwaka Jana , ufuta tuliuza kwa bei ya kutupa, alizeti nayo ni majanga

Ama kweli hii ndio tz ya wanyonge ,acha tuendelee kunyongeka maana tuliipenda wenyewe
 
Mkuu kwanza pokea LIKE kubwa sana...kutoka kwangu...

Tatizo la serikali ya awamu hii hawapendi watu wenye mawazo mbadala kama haya....Wao wanataka kusifiwa tu hata penye hamna.....

Kama viongozi angekubali kupokea ushauri kama huu na wakaufanyia kazi, hakika tungepiga hatia kubwa sana kama taifa.......
Amekua akitoa matamko na hata alikomelea msumari kwenye mfupa kwa kusema kwamba yeye hajaribiwi.
Na ukithubutu kutoa mawazo ambayo yana kinzana na yeye, basi tarajia kuitwa mchochezi au mvunjifu wa sheria.
 
Nilitembelea mikoa ya kusini wiki iliyopita. Cha kushangaza nilikuta wakulima wanauza mbaazi zao kwa sh. 600 kwa kilo, wakati kipindi cha utawala wa JK kilo moja iliuzwa kwa sh. 2000. Hali kadhalika ufuta umenuliliwa kwa sh. 1500 hadi 1200 katika msimu huu wakati kipindi cha utawala wa JK bei kwa kilo ilikuwa sh. 2800 hadi 2400. Inachojali hii serikali ya wanyonge ni kukusanya kodi tu halafu inawatelekeza wakulima kwa wafanyabiashara ili waporwe mazao yao. Hakuna cha serikali ya wanyonge wala nini, hii ni serikali ya kilaghai kama ilivyo serikali ya Zimbabwe. Kila kona wananchi wanalalamikia hali ngumu ya maisha. Yaani sisi wanyonge tunaona 2020 inachelewa ili tutumie haki yetu ya kidemokrasia kuwakataa hawa walaghai.
 
Ulishawahi kuona mnyonge wa wapi anaenda kukopa benki million 10??

Majizi Chadema mtapayuka sana lkn safari mmebanwa kwenye kona .mtanyooka tu

Sisi watoto wetu wanasoma bure
We dada mwasitu na chorus yako majizi chadema huna wimbo mwingine huu tumeuchoka
 
Usijali,Ndege zilizoninuliwa ''cash'' zitakuwa zikihidumia wanyonge.Hapo utajua ni wanyonge wa wapi..
Ndege zinazo tumia injini ya panga boy[emoji15]
Tena kwakuzinunua kwa cash money ni aina nyingine ya uzandiki aiseeee.......
Hakuna nchi yeyote duniani ilio wahi kununua ndege hizi kwa cash money.
NDege zote duniani hununuliwa kwa kulipiwa kidogo kidogo ili ku maintain warranty period, na huku zikiendelea kutumika zinakua zikilipiwa polepole
 
Rais wetu anatupenda sana,katununulia ndege mbili kwa mpigo,ajili ya kusafiria sisi wanyonge
Mnyonge gani anaweza panda ndege!?
Yaani kuna watu hawajawai fika dar toka wazaliwe na wanaishi morogoro si kwa kupenda hawana nauli ya kuja!!
 
Nimesikia rafiki yake Kitwanga kaziponda ndege mpya
Hakaziponda comrade.
Kutwanga hajataka kua mtumwa wa fikra, Kutwanga kausema ukweli.
Ikiwa hata mataifa yalio tupita kwa tambo kubwa kiuchumi wana nunua ndege kwa instalment ili ku maintain warranty period, iweje Tanzania tununue kwa kulipia cash[emoji15]
Hii inatia mashaka kwamba pengine kuna ajenda ya siri nyuma ya malipo kwa cash.
Otherwise.....
Nampongeza Rais kwa kuleta ndege mbili kwa pamoja kwa makusudi na juhudi alizo onyesha kuifufua Air Tanzania
 
Usiamini sana maneno ya wanasiasa akiwa jukwaani..mwingine yupo tayari hata kuvua shati abaki tumbo wazi ili kufanikisha anachokitaka..


Yani kama magufuli alivyokuwa anaomba kura mpaka huruma

Maneno yake: serekari ya makufuri ninserekari ya viwanda.
Msema kweri mpenzi wa Mungu.
Haoo mafisadi nikiingilia ikuru wajiandae uuuhuu

Wakina chenge mpka kesho wanakula ugali mafisadi wapi unadeal nao?

Duh mwenzetu alivyopata kawa kidume hajaribiwi tena, hasikilizi tena wanainchi. Mara fyatueni mara ni utani, mara sigawi chakula mara hakuna siasa.mara kuhamia dodoma. Mwaka unakaribia kukata hamna la maana zaidi ya hasara.

Garama za maisha zinaongezeka.
Hela ngumu kuipata.
Biashara wateja hakuna.
Watalii wanasuasua.
Bandari dar es salaam inakimbiwa adi na wazawa.
Tulikuwa tunakula milo miwilinsaivi ni mmoja.
Ajira umesitisha.
Hosptalini hakuna madawa.
Mishahara huongezi.
Mikopo ya wanafunzi inatolewa kwa mafungu.
Bank hatupati mikopo.
Kutuongezea VAT.
Kuwapa hofu Wafanya kazi wa serikal( mda wowote hawajui utakuja na lipi)

Hii haitoshi bado unataka kutuletea machafuko kwa kuvunja sheria. Swali kwa magufuli lengo lilikupeleka ikulu nikutunyoosha?
Shughulikia ahadi ulizotuahidi uone kama kuna mtu atashawishika kuandamana.

Ushauri usipambane na lowasa na mbowe hao jamaa wanaakili sana ukipambana Nao kichwa kitapata moto utashangaa 2020 hii apa hamna kitu umefanya na utaanguka vibaya.
 
Na wakati huo huyo bibi ulie mtumia 200,000/= ataenda kukatwa 5,000/= na kisha atapokea 195,000/=.
Hapo ni baada ya wewe kukatwa 5,000/= wakati unatuma.
Sasa hapa ndipo wananidanganya kwamba ukituma unalipia na ukipokea unalipia.
Hii inamaanisha kwenye transaction moja unalipa kodi mara mbili.
Huu ni upuuzi kabisa [emoji16] [emoji16] [emoji16]
Angalia wanyonge walipo
1472119593280.jpg
1472119598730.jpg
1472119605850.jpg
1472119612070.jpg
1472119626542.jpg
1472119635572.jpg
 
Nimekuwa nikiumia sana na nchi yangu kwa mambo yanayoendelea !!

Rais Magufuli nipo hapa leo kuongelea mwenendo wa nchi yetu kwenye suala la kiuchumi!!!

Suala lako la kubana matumizi ni zuri lakini unalifanya liwe gumu kwa wananchi wako jinsi unavyochukua hatua!!

Hatua zako hazionekani kuwa za kisayansi kufanya utafiti kuwasaidia wananchi wa kawaida!!!

Riba ya Mabenki
Mh : Riba ya mabenki yetu ipo juu mno kiwango ni 24%-30% kwa mwanachi wa kawaida mfano ukikopa 10,000,000 atatakiwa alipe milioni 13,000,000 sasa hiyo liba ya milioni tatu ndio inawezekana ikawa faida kwenye biashara mtu anayoifanya lakini yote anairudisha kuilipa kama Riba !!

Wewe bado ujaliona hilo lakini Jirani yako Uhuru Kenyatta ameliona hilo kaamua kusaini mswada wa sheria kupunguza Riba ya mabenki kutoka 22%-24% na kuwa 10.5%-14.5 wewe bado hata swala la mabenki hakuna siku nimesikia ukiliongelea!!

Uwezi kujenga uchumi bila kuimulika sector ya mabank Tanzania!!

Sasa hivi kuna vijana wanaitimu Chuo kikuu walitakiwa kukuta Riba imeshushwa ili watumie vyeti vyao vya kuitimu kukopea pesa kwenye mabenki ni kitendo cha kuweka Sera wewe upo kimya !!!

Tatizo la Ajira litaisha vipi kama waitimu wa vyuo vikuu watamaliza vyuo bila kupata mikopo ya kujiajiri na kuajiri wenzao wa Form 4&6?

Tatizo la Ajira tunalitengeneza sisi wenyewe wala hatutakiwi kutafuta mchawi wachawi ni sisi wenyewe!!!

Mbona mswada wa mahakama ya mafisadi uliwaiswa kupelekwa bungeni ingawa hata hatuoni ukifanya kazi ??

Kwanini tusipeleke mswada wa kupunguza Riba tukaacha kuwakamua Watanzania na kuwavutia waitimu wa vyuo vikuu wajiajiri wenyewe?

Kila mwaka tunasikia mabank kama Crdb,Nmb wanatangaza faida ya billions of money, hiyo faida kwanini hata nusu yake isipunguziwe kwenye kushusha Riba ya mabenki ili kuwasadia waitimu wa vyuo vikuu na wawekezaji wa ndani!!

Bado Mimi sijaelewa Mtukufu Rais Magufuli wewe ni Rais wa wanyonge wapi??
Bora useme mkuu maana huenda wakakusikiliza..huyu mr.Mipango nae yupo kimya uadhani haoni.
 
Madawa ya kulevya pia raisi anawatetea wanyonge kwa sababu vijana mtaani ndio waathirika wakubwa km mateja, wezi, ujambazi na ubakaji vinawaathiri wanyonge wengi wao wameingia kwenye hili kupitia madawa ya kulevya.

Raisi anapozuia mtandao wa madawa ya kulevya kwa kumata wafanya biashara hao wakubwa moja kwa moja inakwenda kuleta impact kwa wanyonge, hawataibiwa mali zao, biashara haramu zitapungua, afya, amani na maendeleo yatapatikana kwa wanyonge.
Aliyekuwa anadeal na madawa ya kulevya c keshang'olewa!!!
 
Ulishawahi kuona mnyonge wa wapi anaenda kukopa benki million 10??

Majizi Chadema mtapayuka sana lkn safari mmebanwa kwenye kona .mtanyooka tu

Sisi watoto wetu wanasoma bure
Wanasoma shule ipi watoto wenu nyie wanyonge?
Au zile ambazo walimu wake wanafundisha tu ilimradi siku ipite...hawana Ari ya kufundisha kabsa!!
Yaani zile shule zimezopewa madawati ya harambee ila vitabu hakuna...
Zile shule ziczozingatia ubora wa elimu! Zile ambazo wayoto wanatoka shule wamechakaa...hakuna hata maji safi na salama ya kunywa hapo shuleni!!!
 
Back
Top Bottom