Rais Magufuli wewe ni Rais wa wanyonge wapi??

Rais Magufuli wewe ni Rais wa wanyonge wapi??

Nimekuwa nikiumia sana na nchi yangu kwa mambo yanayoendelea !!

Rais Magufuli nipo hapa leo kuongelea mwenendo wa nchi yetu kwenye suala la kiuchumi!!!

Suala lako la kubana matumizi ni zuri lakini unalifanya liwe gumu kwa wananchi wako jinsi unavyochukua hatua!!

Hatua zako hazionekani kuwa za kisayansi kufanya utafiti kuwasaidia wananchi wa kawaida!!!

Riba ya Mabenki
Mh : Riba ya mabenki yetu ipo juu mno kiwango ni 24%-30% kwa mwanachi wa kawaida mfano ukikopa 10,000,000 atatakiwa alipe milioni 13,000,000 sasa hiyo liba ya milioni tatu ndio inawezekana ikawa faida kwenye biashara mtu anayoifanya lakini yote anairudisha kuilipa kama Riba !!

Wewe bado ujaliona hilo lakini Jirani yako Uhuru Kenyatta ameliona hilo kaamua kusaini mswada wa sheria kupunguza Riba ya mabenki kutoka 22%-24% na kuwa 10.5%-14.5 wewe bado hata swala la mabenki hakuna siku nimesikia ukiliongelea!!

Uwezi kujenga uchumi bila kuimulika sector ya mabank Tanzania!!

Sasa hivi kuna vijana wanaitimu Chuo kikuu walitakiwa kukuta Riba imeshushwa ili watumie vyeti vyao vya kuitimu kukopea pesa kwenye mabenki ni kitendo cha kuweka Sera wewe upo kimya !!!

Tatizo la Ajira litaisha vipi kama waitimu wa vyuo vikuu watamaliza vyuo bila kupata mikopo ya kujiajiri na kuajiri wenzao wa Form 4&6?

Tatizo la Ajira tunalitengeneza sisi wenyewe wala hatutakiwi kutafuta mchawi wachawi ni sisi wenyewe!!!

Mbona mswada wa mahakama ya mafisadi uliwaiswa kupelekwa bungeni ingawa hata hatuoni ukifanya kazi ??

Kwanini tusipeleke mswada wa kupunguza Riba tukaacha kuwakamua Watanzania na kuwavutia waitimu wa vyuo vikuu wajiajiri wenyewe?

Kila mwaka tunasikia mabank kama Crdb,Nmb wanatangaza faida ya billions of money, hiyo faida kwanini hata nusu yake isipunguziwe kwenye kushusha Riba ya mabenki ili kuwasadia waitimu wa vyuo vikuu na wawekezaji wa ndani!!

Bado Mimi sijaelewa Mtukufu Rais Magufuli wewe ni Rais wa wanyonge wapi??
Mkuu kwanza pokea LIKE kubwa sana...kutoka kwangu...

Tatizo la serikali ya awamu hii hawapendi watu wenye mawazo mbadala kama haya....Wao wanataka kusifiwa tu hata penye hamna.....

Kama viongozi angekubali kupokea ushauri kama huu na wakaufanyia kazi, hakika tungepiga hatia kubwa sana kama taifa.......
 
Mkuu kwanza pokea LIKE kubwa sana...kutoka kwangu...

Tatizo la serikali ya awamu hii hawapendi watu wenye mawazo mbadala kama haya....Wao wanataka kusifiwa tu hata penye hamna.....

Kama viongozi angekubali kupokea ushauri kama huu na wakaufanyia kazi, hakika tungepiga hatia kubwa sana kama taifa.......
Kweli nimeamini hawa jamaa wakifa uwa hawaendi mbuguni!!
 
Leo Ukimtumia bibi yako kijijini sh 200,000/ kwenye simu, ajiandae kukatwa sh 5,000/. Huyu ndo maskini ambaye anatakiwa rais kumfikiria
Hata kutoa elfu kumi wanakata hela nyingi yani.
 
Usijali,Ndege zilizoninuliwa ''cash'' zitakuwa zikihidumia wanyonge.Hapo utajua ni wanyonge wa wapi..
 
Usiamini sana maneno ya wanasiasa akiwa jukwaani..mwingine yupo tayari hata kuvua shati abaki tumbo wazi ili kufanikisha anachokitaka..
 
Hakuna raisi wa wanyonge duniani. Hayo huwa wanaongea kwasbb ya kuomba kura. Ni sawa na ww kipind unaomba kazi kwenye shirika fulani. Utajifanya mwema, mcha Mungu na utavaa vizuri.
Ipite miezi 6 baada ya kupata kazi sasa. Nafikiri ushapata jibu
 
Ni kweli kabisa hasa hawa watu benki hawana faida yoyote kwa wananchi zaidi ya kujifaidisha Wao wenyewe kwa kulipana mishahara mikubwa,ukikopa kwao wanakupiga riba kubwa Sana,ukiweka fedha kwao wanasema kuwa fedha yako itaongezwa riba kwa asilimia kadhaa,siku ya kwenda kuangalia unakuta hakuna chochote kilichoongezeka zaidi ya kukatwa fedha ambazo ulikuwa umeweka kwenye Akaunti yako.
 
Ulishawahi kuona mnyonge wa wapi anaenda kukopa benki million 10??

Majizi Chadema mtapayuka sana lkn safari mmebanwa kwenye kona .mtanyooka tu

Sisi watoto wetu wanasoma bure
 
Back
Top Bottom