Wimbo
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 886
- 664
Tuko katika vita na kama ilivyo kawaida ya Watanzania umoja wetu ndiyo nguvu yetu. Umedhihirisha kwamba wewe ni jemedari hodari katika hili.
Ulimwengu mzima unatafuta kujua huyu Magufuli ni wa aina gani? Vitabu vya historia vitaandika habari zako kama mtu shujaa wa karne.
Naamini COVID19 itapita na Tanzania itabaki salama na heshima kubwa. Mungu anayeishi hasemi uongo, alisema niiteni nami nitaitika. Mungu amesikia kilio chetu atajibu nasi tutamtukuza, vile mataifa wanavyotuombea matokeo hasi ndivyo Mungu atakavyo jitukuza katika kutufanikisha katika mema.
Magufuli tunakuamini wala usivunjike moyo kwa kelele zinazopigwa. Weka pamba masikioni songa mbele uuone utukufu a Mungu. Huyo anayekufa sasa anakufa kwa wakati wake na mwisho wa siku maisha yanaendelea.
Wakati wa vita hatutaji majeruhi wala waliokufa vitani, tutafanya hiyo hesabu tukishashinda vita. Wewe tuhimize kuingia kwenye mahandaki tushishambuliwe. Ukiona kuna mtu anafanyia mzaha vita msaidie kuwa kimya tutaombana msamaha mwisho wa safari ya vita.
Wewe uliandaliwa wakati wa sasa, wakati muafaka kwa kusudi maalum. Nawaza kimoyomoyo angelikuwa mwingine ambaye anaweza kusukumwa na kila upepo tungekuwa wapi.
Wewe ni mwanaume, big up tuko nyuma yako. Natamani nikapande Mlima Kilimanjaro niwaambie marais wote wa Afrika, woga wetu ndio umaskini wetu wachukue mfano kwako
Long live Magufuli.