MV Mwanza ni wazo la Hayati Magufuli sio Samia

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,195
Reaction score
10,709
Hivi karibuni, tumeshuhudia video mitandaoni kutoka kwa kina Photogenic Mtoto na kikosi chake. Wametupitisha kwenye madaraja ya kifahari ya meli mpya ya MV Mwanza "Hapa Kazi Tu", kuanzia VIP hadi daraja la kawaida.
cccccc-1.jpg

Kusema kweli, meli ni nzuri sana! Ina mvuto wa aina yake, na kwa mbali unaweza kudhani ni hoteli ya nyota tano inayocheza sebene juu ya maji.
images - 2026-01-24T213345.301.jpeg

Katika hali ya kushangaza, video hizo zimejaa sifa kedekede kwa viongozi wa sasa, huku picha kubwa la Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, likipepea kama bendera ya taifa. Sasa, jamani, hebu tuwe waungwana! Hata kama tunapenda "shobo" za kisiasa, kuna mahali penye ukweli wa kihistoria.
26cde720-c06a-11f0-8456-eff94716b162.jpg.webp

Wazo la ujenzi wa MV Mwanza halikuzaliwa juzi kwenye kikao cha baraza la mawaziri aliloliteua Samia. Huu ulikuwa ni mpango mkakati, ndoto, na jasho la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Ni yeye aliyepiga msumari wa kwanza wa ahadi hiyo, akiamini kuwa Warangi, Wakerewe, Wamaasai, Wahehe, Wajita, na Wasukuma wanastahili usafiri wa hadhi ya ndege ndani ya maji.
images - 2026-01-24T212752.718.jpeg

Lakini kama usemavyo mtaani, "Internet never forgets" (Mtandao hausahau). Wakati kina Photogenic Mtoto wakijaribu kupaka rangi mpya kwenye ukuta wa zamani, Watanzania kwenye comments wamegeuka kuwa walimu wa historia.
images - 2026-01-24T212825.245.jpeg

Inafurahisha kuona jinsi wananchi walivyowatandika "makavu" live! "Ebo! Meli ni ya Magufuli, sifa mnampelea Mwigulu? Kwani Mwigulu ndiye aliyeweka msingi wa ujenzi huu?"
images - 2026-01-24T212608.422.jpeg

Wapo wengine wameenda mbali na kusema kuwa hata kama meli imekamilika chini ya Rais Samia (ambaye anastahili sifa kwa kuendeleza miradi), mzizi wa mradi huu una chapa ya chuma ya JPM, na anapaswa kutajwa wazi.
IMG-20220515-WA0116.jpg

Mpeni Kaisari Kilicho cha Kaisari.
Ubunifu wa maudhui usitufanye tuwe viziwi wa historia. Unaweza kupiga picha nzuri, lakini ukishindwa kusema ukweli, picha yako inapoteza kabsa uaminifu. MV Mwanza ni baraka tulizozipata kutokana na maono ya Hayati Magufuli, na ni vyema influencers wetu wakajifunza kutofautisha kati ya "anayekamilisha mradi" na "aliyeasisi ndoto."
images - 2026-01-24T212752.718.jpeg

Vinginevyo, tutaanza kuamini kuwa siku hizi hata mvua ikinyesha, influencers watasema ni jitihada za wizara ya Maji, na si baraka za Mungu.
 
Attachments

  • images - 2026-01-24T212920.501.jpeg
    images - 2026-01-24T212920.501.jpeg
    22.1 KB · Views: 21
Hivi karibuni, tumeshuhudia video mitandaoni kutoka kwa kina Photogenic Mtoto na kikosi chake. Wametupitisha kwenye madaraja ya kifahari ya meli mpya ya MV Mwanza "Hapa Kazi Tu", kuanzia VIP hadi daraja la kawaida.
View attachment 3533983
Kusema kweli, meli ni nzuri sana! Ina mvuto wa aina yake, na kwa mbali unaweza kudhani ni hoteli ya nyota tano inayocheza sebene juu ya maji.
View attachment 3533979
Katika hali ya kushangaza, video hizo zimejaa sifa kedekede kwa viongozi wa sasa, huku picha kubwa la Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, likipepea kama bendera ya taifa. Sasa, jamani, hebu tuwe waungwana! Hata kama tunapenda "shobo" za kisiasa, kuna mahali penye ukweli wa kihistoria.
View attachment 3533987
Wazo la ujenzi wa MV Mwanza halikuzaliwa juzi kwenye kikao cha baraza la mawaziri aliloliteua Samia. Huu ulikuwa ni mpango mkakati, ndoto, na jasho la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Ni yeye aliyepiga msumari wa kwanza wa ahadi hiyo, akiamini kuwa Warangi, Wakerewe, Wamaasai, Wahehe, Wajita, na Wasukuma wanastahili usafiri wa hadhi ya ndege ndani ya maji.
View attachment 3533985
Lakini kama usemavyo mtaani, "Internet never forgets" (Mtandao hausahau). Wakati kina Photogenic Mtoto wakijaribu kupaka rangi mpya kwenye ukuta wa zamani, Watanzania kwenye comments wamegeuka kuwa walimu wa historia.
View attachment 3533986
Inafurahisha kuona jinsi wananchi walivyowatandika "makavu" live! "Ebo! Meli ni ya Magufuli, sifa mnampelea Mwigulu? Kwani Mwigulu ndiye aliyeweka msingi wa ujenzi huu?"
View attachment 3533984
Wapo wengine wameenda mbali na kusema kuwa hata kama meli imekamilika chini ya Rais Samia (ambaye anastahili sifa kwa kuendeleza miradi), mzizi wa mradi huu una chapa ya chuma ya JPM, na anapaswa kutajwa wazi.
View attachment 3533982
Mpeni Kaisari Kilicho cha Kaisari.
Ubunifu wa maudhui usitufanye tuwe viziwi wa historia. Unaweza kupiga picha nzuri, lakini ukishindwa kusema ukweli, picha yako inapoteza kabsa uaminifu. MV Mwanza ni baraka tulizozipata kutokana na maono ya Hayati Magufuli, na ni vyema influencers wetu wakajifunza kutofautisha kati ya "anayekamilisha mradi" na "aliyeasisi ndoto."
View attachment 3533985
Vinginevyo, tutaanza kuamini kuwa siku hizi hata mvua ikinyesha, influencers watasema ni jitihada za wizara ya Maji, na si baraka za Mungu.
Hi ni project nzuri ya JpM ambayo imecost billions of shillings za watanzania, ila ukifanya analysis makini nikama "white elephant project" kwasababu biashara katika ziwa victoria kati ya Kenya Uganda na Tanzani iko low sana kiasi kwamba hata meri ziliopo kwasasa are oparating under capacity,.....kwahiyo hi inaenda kubuni biashara gani mpya ya kuvutia abiria kuitumia? Labda iwe kama kivutio cha watalii
 
Wmetengeneza meli kubwa safari zinafanyika sehemu mbili tu Mwanza a Bukoba, hawakuona haja ya kwenda Musoma na Geita ?
 
Hi ni project nzuri ya JpM ambayo imecost billions of shillings za watanzania, ila ukifanya analysis makini nikama "white elephant project" kwasababu biashara katika ziwa victoria kati ya Kenya Uganda na Tanzani iko low sana kiasi kwamba hata meri ziliopo kwasasa are oparating under capacity,.....kwahiyo hi inaenda kubuni biashara gani mpya ya kuvutia abiria kuitumia? Labda iwe kama kivutio cha watalii
Kuna biashara kubwa sana huko
 
Plus lile lidaraja reeeefu la mabilioni eneo lilelile! Uwekezaji wa mihemko bila planning! Mapovu ruksa...
 
Mkuu Tanzania inakosa strategic national planners, kwa kweli mtu atapandaje meli wakati kuna daraja linafanya kazi 24/7 kuvuka kuenda bkb hadi kampala Rwada kwa mda wamasaa machache.
 
Kanda yote ya ziwa, magharibi, na kaskazini hakuna biashara ya kujustify uwekezaji mkubwa namna hiyo kwa wakati mmoja! Siasa za one man show na urais wa kifalme zinatenda yote haya kwa kuwa tu wamejiwekea ulinzi wa kutokuwajibishwa!
 
Walipenda sifa na kura za wananchi otherwise hela nyingi zimepotea bila faida yoyote ata uwape miaka 20 hiyo pesa haiwezi kurudishwa na hiyo biasha hawakufanya feasibility study ya project.
 
Tunajua ulivyo alejiki na jina la JPM
Naona umekosa point mkuu, hizo pesa nikama zimepotea pale ziwa victoria kuna zaidi ya meri kubwa 4, zinafanya kazi kwa zamu, kwa sabanu mizigo michache inakuaje unaleta meri nyingine kubwa na ya gharama huo ni ujumu wa pesa za wa tanzania
 
Walipenda sifa na kura za wananchi otherwise hela nyingi zimepotea bila faida yoyote ata uwape miaka 20 hiyo pesa haiwezi kurudishwa na hiyo biasha hawakufanya feasibility study ya project.

Muda ni mwalimu mzuri sana, uendeshaji wake utakua wa ghali sana na kwa kuwa hamna wateja wa kutosha liltategemea ruzuku, baada ya muda litakufa tu kifo cha kawaida, inanikumbusha lile likivuko kuukuu walilinunua kwa mihemko vilevile lije kufanya ferrying ya Dar-Bagamoyo, kuficha kashfa wakalificha kwa wanajeshi, nina uhakika lishazikwa tayari au lishauzwa kama chuma chakavu!
 
Hivi karibuni, tumeshuhudia video mitandaoni kutoka kwa kina Photogenic Mtoto na kikosi chake. Wametupitisha kwenye madaraja ya kifahari ya meli mpya ya MV Mwanza "Hapa Kazi Tu", kuanzia VIP hadi daraja la kawaida.
View attachment 3533983
Kusema kweli, meli ni nzuri sana! Ina mvuto wa aina yake, na kwa mbali unaweza kudhani ni hoteli ya nyota tano inayocheza sebene juu ya maji.
View attachment 3533979
Katika hali ya kushangaza, video hizo zimejaa sifa kedekede kwa viongozi wa sasa, huku picha kubwa la Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, likipepea kama bendera ya taifa. Sasa, jamani, hebu tuwe waungwana! Hata kama tunapenda "shobo" za kisiasa, kuna mahali penye ukweli wa kihistoria.
View attachment 3533987
Wazo la ujenzi wa MV Mwanza halikuzaliwa juzi kwenye kikao cha baraza la mawaziri aliloliteua Samia. Huu ulikuwa ni mpango mkakati, ndoto, na jasho la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Ni yeye aliyepiga msumari wa kwanza wa ahadi hiyo, akiamini kuwa Warangi, Wakerewe, Wamaasai, Wahehe, Wajita, na Wasukuma wanastahili usafiri wa hadhi ya ndege ndani ya maji.
View attachment 3533985
Lakini kama usemavyo mtaani, "Internet never forgets" (Mtandao hausahau). Wakati kina Photogenic Mtoto wakijaribu kupaka rangi mpya kwenye ukuta wa zamani, Watanzania kwenye comments wamegeuka kuwa walimu wa historia.
View attachment 3533986
Inafurahisha kuona jinsi wananchi walivyowatandika "makavu" live! "Ebo! Meli ni ya Magufuli, sifa mnampelea Mwigulu? Kwani Mwigulu ndiye aliyeweka msingi wa ujenzi huu?"
View attachment 3533984
Wapo wengine wameenda mbali na kusema kuwa hata kama meli imekamilika chini ya Rais Samia (ambaye anastahili sifa kwa kuendeleza miradi), mzizi wa mradi huu una chapa ya chuma ya JPM, na anapaswa kutajwa wazi.
View attachment 3533982
Mpeni Kaisari Kilicho cha Kaisari.
Ubunifu wa maudhui usitufanye tuwe viziwi wa historia. Unaweza kupiga picha nzuri, lakini ukishindwa kusema ukweli, picha yako inapoteza kabsa uaminifu. MV Mwanza ni baraka tulizozipata kutokana na maono ya Hayati Magufuli, na ni vyema influencers wetu wakajifunza kutofautisha kati ya "anayekamilisha mradi" na "aliyeasisi ndoto."
View attachment 3533985
Vinginevyo, tutaanza kuamini kuwa siku hizi hata mvua ikinyesha, influencers watasema ni jitihada za wizara ya Maji, na si baraka za Mungu.
Kamfufue mungu wako!!
 
Muda ni mwalimu mzuri sana, uendeshaji wake utakua wa ghali sana na kwa kuwa hamna wateja wa kutosha liltetegemea ruzuku, baada ya muda litakufa tu kifo cha kawaida, inanikumbusha lile likivuko kuukuu walilinunua kwa mihemko vilevile lije kufanya ferrying ya Dar-Bagamoyo, kuficha kashfa wakalificha kwa wanajeshi, nina uhakika lishazikwa tayari au lsihauzwa kama chuma chakavu!
Ni kweli walinunua ndege 11 kwa mihemko mpaka leo haijawahi kuingiza faida zaidi ya hasara za billions kila mwaka, hapo hapo waliuua shirika la fastjet ambayo ilikua inasaidia wananchi wa mikoani kusafiri kwa bei nafuu.
 
Back
Top Bottom