Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,273
- 21,455
Nimeguswa na uchungu alioonyesha Raisi Magufuli juu ya udanganyifu tunaofanyiwa katika sekta ya madini.
Nimejiuliza ikiwa Raisi Magufuli na wananchi kwa ujumla wanailewa kihalisi historia ya mgodi wa Bulyankulu (Bulyanhulu) na nani hasa alikuwa chanzo cha sie kuibiwa?
Labda kwa wale msiojua historia, dhahabu ya mgodi wa Bulyankulu iligunduliwa wakati wa Nyerere miaka ya 1970 na kampuni kutoka Sweden. Wakati wa majadiliano kuhusu uzalishaji, Nyerere alitaka Tanzania iwe na hisa ya 51% na wawekezaji wawe na 49%, kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamond mine. Nyerere alitaka mgodi huu uendeshwe na management ya Watanzania kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamonds. Wawekezaji toka Sweden walikataa wakitaka Tanzania iwe na 49% na wao ndio wawe na 51%. Nyerere alikataa, akawaambia kama hawataki Tanzania iwe na 51% waondoke. Nitamnukuu Nyerere alivyowaambia "dhahabu haiozi, kama hamtaki 49% ondokeni, tutaiacha hiyo dhahabu ardhini hadi tuje tuwe na uwezo wetu wenyewe wa kuichimba".
Sasa baada ya Nyerere kuacha uraisi, makubaliano yaliidhinishwa na Mkapa kutoka ile 49% aliyokataa Nyerere hadi kuwa 5% ya Mkapa, ambayo hata hiyo 5% ilikuja kuondolewa na Kigoda na Tanzania ikawa na 0% (ni wazi Kigoda aliagizwa na Mkapa - kwa hiyo suala la kutowachukulia hatua waliokufa linaweza lisiwe relevant). Ile kampuni ya mwanzo toka Sweden iliyogundua dhahabu Bulyankulu iliposikia Mkapa amekubali 5% ilienda mahakamani kuishitaki serikali na kampuni mpya kutoka Canada ya Bulyankulu Mining, wakisema wao ndio waligundua dhahabu ya Bulyanhulu na walikuwa tayari kuipa Tanzania 49% badala ya 5%. Hadi wakati huo hiyo kampuni ya Sweden ilikuwa na majengo yake pale Bulyankulu, ya ofisi na kulala, na haya ndiyo yaliyotumiwa na hii kampuni ya Canada pale mwanzoni. Serikali ya Mkapa ilisaidiana na kampuni mpya ya Canada ya Bulyankulu Gold mine, nadhani Chenge akiwa Mwanasheria Mkuu, kampuni ya Sweden ikashindwa kesi ambayo kwa kweli ilikuwa ni kushindwa kwa Tanzania kwa kutumia wanasheria wetu wenyewe!
Na si Bulyankulu tu ambayo Mkapa aliibadilisha. Baada ya Nyerere kuondoka madarakani, hata zile 51% tulizokuwa nazo Mwadui Diamonds zilibadilishwa na kuwa 25%. Sasa niwaambie kitu cha AJABU kilichotokea Mwadui Diamonds ndio mtaelewa kwa nini Watanzania tumefanywa wajinga waliwao!
Wakati Mwadui Diamonds ikiwa chini ya Tanzania kwa asilimia 51%, wawekezaji walitenga eneo la mgodi na kulifanya kuwa eneo la uwanja wa ndege, ambao pia ulitumika kama uwanja kwa ajili ya ndege za kibisahara (commercial airlines). Sasa kumbe siku zote walijua kwamba hili eneo la uwanja wa ndege ndilo lililokuwa na almasi kwa wingi sana!!!! Siku tu mkataba na serikali ulipobadilishwa kutoka 51% kuwa 25% hapo mwaka 1997 kama sikosei, walitangaza kwamba ule uwanja wa ndege ndani ya Mwadui Diamonds unafungwa ili uchimbwe almasi. Nasikia kuwa lile eneo lililokuwa uwanja wa ndege lilitoa almasi ambazo mgodi haukuwahi kutoa katika historia yote ya Tanzania kuwa na 51%!
Mkapa alitetea kwamba tutafaidika na kodi za mauzo - na kwa ujanja kampuni zikawa zinatangaza hasara au faida kidogo sana ili wasilipe kodi. Na hili la migodi na kukubali hizi 5% lilikuwa mojawapo ya mambo yaliyofanya uhusiano wa Mkapa na Nyerere uzorote hadi tuseme ufe, pamoja na suala la kuuza NBC na mashirika mengine. Nyerere alimwambia Mkapa "Nina wasiwasi siku moja nitasikia umebinafsisha magereza".