Rais Magufuli, Watanzania wangejua hii historia ya Bulyankulu na Mwadui wangelia hata zaidi

Mkuu INASIKITISHA SANA, hii inatokana hii inatokana na wabunge tulionao hasa kutoka CHAMA TAWALA, ambao wamekuwa wakipitisha mambo ya hovyo kwa UWINGI wao BUNGENI...hii inatokea TANZANIA TU...

Mkuu, kama hata sisi tu katika mijadala yetu humu tumetanguliza uvyama hata pasiposrahili, unadhani wabunge wako tofauti na sisi.

Kama ubunge wenyewe tunapeana kama zawadi na wakati mwingine hata kwa kuhonga, ni cha kushangaa? Kama sisi wananchi kumchagua mtu tunaangalia ana nini atatupa nini (fedha) tunawezaje kuwaza miujiza ya mageuzi?

Kama tunadiriki hata kusema tuko tayari hata kumtumia shetani ili tu tuingie ikulu, tuna tofauti gani na hao fisiem?
 
Sidhani kama suala ni ubaya wa CCM au Chadema au chama kingine. Ni mentality ya Watanzania kwa ujumla ambao siku zote hawaweki maslahi ya taifa mbele. CCM wako so consumed na kuendelea kuwa caha tawala, kiasi kwamba chchote Chadema wakishauri wanaona kuwa wakikubali watahatarisha kuendelea kuwapo kwao madarakani. Chadema nao wako so consumed kuingia madarakani kiasi kwamba wamesahau kwamba mara nyingne wao ndio kisababishi cha mgongano na wanasiasa wa chama tawala - wako so focused na kuwakosoa.

Sasa siku tukibadilisha mentality hii ya chama changu na mimi kwanza na taifa baadaye, nadhani tutaenda mbali sana. Nyerere alijitahidi sana kutupa mentality ya uzalendo katika utawala wake wa miaka 23, ambayo ilikuja kupotea katika utawala wa miaka 10 tu ya awamu iliyofuata chini ya Mwinyi. Najiuliza sana kwa nini tulibadilika haraka na ghafla kiasi kile?

Ni sawa mkuu,lakini watanzania wametokea mbali,mpaka kufikia hapa kifikra na kichangamoto,tulikuwa Tupo katika Giza nene,la kutojijua,kuna makosa yakihistoria ambayo yalichangia kuleta siasa mbovu,iliyokosa ukweli kwa kiasi kikubwa na bado,inaendelea kuathiri uhalisia wa namna fulani,ambayo bado inaendelea kulitafuna taifa letu,bila ya kuanza kuwanyoshea vidole,

Hawa na wale,la kwanza kabisa Ni udhaifu wa katiba yetu,ambayo kwa kiasi kikubwa imekosa sheria na mikakati ya kulinda,rasilimali ya Taifa,utawala bora wa sheria,mipaka ya uongozi na maamuzi,kwa upande wa Nyerere na Mwinyi kila mmoja ana mazuri yake na mabaya yake,Nyerere alileta ujamaa ambao pia ulimshinda,alihubiri siasa zaidi,ill kuleta uzalendo,lakini alisahau mishahara ya wananchi wake,na kuliingiza taifa katika njaa,rushwa,na ubadhirifu,hicho ndicho kilikuwa chanzo,na Mwinyi alituokoa kutoka katika mkwamo huu wa hali mbaya kimaisha,ambapo nguvu,sabuni ya kukogea,sukari na vitu muhimu katika maisha ya kila siku ilikuwa tunu,na kuvipata ilibidi ipite rushwa,na yeye akaanzisha biashara huru,ambayo ndiyo iliyoanza kutukwamua katika Hali mbaya tuliyokuwa nayo kabla,ambayo ndio vile vile kwa upande wa pili ,

serikali ya CCM iliendeleza kuchota mikopo ya nje na kuendeleza ufisadi,ilikuwa chanzo cha kuliingiza taifa katika mikopo ya kimataifa,sasa watanzania tusome kwa yaliyopita,kutengeneza taifa kwa yanayokuja mbele,kitaifa na kimataifa.sasa serikali hii ya CCM,iache mitizamo ya nyuma ya kiutawala,iachie haki na sheria zichukue nafasi katika uongozi wa taifa hili,huku wakishirikiana na wapinzani kwa nia safi sana,kuleta maendeleo ya taifa hili,na hilo linatakikana lifanye kazi sasa,Kama kweli tunalipenda taifa letu.
 
Wakae kimya tu wawasikilize wale wenye uwezo wa kuchambua mikataba hiyo. Kwani aliyetaka sifa ya kuwa Wabunge wawe na sifa ya KKK ni nani? Yale yale MACCM ambayo yanajidai bado yanamtafuta mchawi wa Watanzania! Nchi ina miaka 56 bado kuwa mbunge ni kuwa tu KKK!!!!
Machadema kule Tunduma yana Mbunge darasa la 4....
 
Inasikitisha sana na bado anaenda kanisani bila kutuomba msamaha watz!! Heri Mangungo aliyeuza kipande cha ardhi kwa kipande cha nguo kuliko huyu baba alichotufanyia watanzania ili hali akiwa sio tu ni msomi bali pia ana akili timamu "MUNGU ANAMUONA" ....

RIP Mwalimu, haya yalifanyika kama vile watu waliona kifo chako! Inasikitisha sana kwa mtu uliyemwamini kufanya kinyume na matarajio yako! Labda tu nikwambie huko uliko Mwalimu, pamoja na hayo yote aliyotufanyia, bado tunanapenda na kumtunza kwa kodi zetu wanyonge!!!!!!!!
 
Mkapa km ana akili Timamu nahisi [HASHTAG]#Atakufa[/HASHTAG] siku so zake
Nchi imekwama kimaendeleo uku ongezeko la watu likipaa, Rais JPM hana sehemu ambayo atapata pesa zaidi maana ukomo was makusanyo umefika au unaweza kupungua hivyo ili atekeleze miradi mikubwakubwa hana Budi kukopa Nje hilo nalo ndo linalimuumiza zaidi kwani Deni la Taifa limepaa [HASHTAG]#Expontially[/HASHTAG] tokea aingia Madarakan so hana Namna ni kurudi TU kwenye uTanzania na uzalendo ndo tunaona anaanza japo anajua madhira yake lakin hakuna namna nikufanya hivyo ili Km Taifa tutoke....

Ndani ya CCM kuna chembechembe au Makinikia makini km JPM ila umakini wake ungeimarika maradufu na angekua upande salama zaidi km angeruhusu [HASHTAG]#Bunge[/HASHTAG] kua imara zaidi aya yote yangefanyikia Bunge ni na asingelaumiwa na watangulizi wake Ben na JK wala wazungu......

Maoni yangu Bila BUNGE BUNGE BUNGE BUNGE BUNGE BUNGE BUNGE BUNGE BUNGE imala hii vita ya uchumi hawez akaishinda MTU mmoja
 
Tuoeni mapumziko mtatuua jamani aaah,iv kwel huku MKAPA anaruhusu uwanja ukiokua wa ndege pachimbwe madini kwel kbsa huyu mzee.
 
kumbe ndi maana Ben alituita malofa...kweli sisi ni malofa,alituibia na bado tunamsikiliza
 
  • Thanks
Reactions: SDG
tunaitwa nyani kwasababu ya ujinga wetu ngozi ni kipitio tu
Si kweli! Kuna mijitu ambayo ni majangili na wanao ichukia nchi yao wenyewe! Ndiyo maana yanakula tu na kunenepeana afanalek! Muumba wangu Rabuka ingia kazini!
 
Tuoeni mapumziko mtatuua jamani aaah,iv kwel huku MKAPA anaruhusu uwanja ukiokua wa ndege pachimbwe madini kwel kbsa huyu mzee.
Duh! Ni kilio kwa kweli! Ehh MAMA TANZANIA YANGU EHH!
 
Nimeguswa na uchungu alioonyesha Raisi Magufuli juu ya udanganyifu tunaofanyiwa katika sekta ya madini.

Nimejiuliza ikiwa Raisi Magufuli na wananchi kwa ujumla wanailewa kihalisi historia ya mgodi wa Bulhankulu (Bulyanhulu) na nani hasa alikuwa chanzo cha sie kuibiwa?

Labda kwa wale msiojua historia, dhahabu ya mgodi wa Bulyankulu iligunduliwa wakati wa Nyerere miaka ya 1970 na kampuni kutoka Sweden. Wakati wa majadiliano kuhusu uzalishaji, Nyerere alitaka Tanzania iwe na hisa ya 51% na wawekezaji wawe na 49%, kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamond mine. Nyerere alitaka mgodi huu uendeshwe na management ya Watanzania kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamonds. Wawekezaji toka Sweden walikataa wakitaka Tanzania iwe na 49% na wao ndio wawe na 51%. Nyerere alikataa, akawaambia kama hawataki Tanzania iwe na 51% waondoke. Nitamnukuu Nyerere alivyowaambia "dhahabu haiozi, kama hamtaki 49% ondokeni, tutaiacha hiyo dhahabu ardhini hadi tuje tuwe na uwezo wetu wenyewe wa kuichimba".

Sasa baada ya Nyerere kuacha uraisi, makubaliano yaliidhinishwa na Mkapa kutoka ile 49% aliyokataa Nyerere hadi kuwa 5% ya Mkapa, ambayo hata hiyo 5% ilikuja kuondolewa na Kigoda na Tanzania ikawa na 0% (ni wazi Kigoda aliagizwa na Mkapa - kwa hiyo suala la kutowachukulia hatua waliokufa linaweza lisiwe relevant). Ile kampuni ya mwanzo toka Sweden iliyogundua dhahabu Bulyankulu iliposikia Mkapa amekubali 5% ilienda mahakamani kuishitaki serikali na kampuni mpya kutoka Canada ya Bulyankulu Mining, wakisema wao ndio waligundua dhahabu ya Bulyanhulu na walikuwa tayari kuipa Tanzania 49% badala ya 5%. Hadi wakati huo hiyo kampuni ya Sweden ilikuwa na majengo yake pale Bulyankulu, ya ofisi na kulala, na haya ndiyo yaliyotumiwa na hii kampuni ya Canada pale mwanzoni. Serikali ya Mkapa ilisaidiana na kampuni mpya ya Canada ya Bulyankulu Gold mine, nadhani Chenge akiwa Mwanasheria Mkuu, kampuni ya Sweden ikashindwa kesi ambayo kwa kweli ilikuwa ni kushindwa kwa Tanzania kwa kutumia wanasheria wetu wenyewe!

Na si Bulyankulu tu ambayo Mkapa aliibadilisha. Baada ya Nyerere kuondoka madarakani, hata zile 51% tulizokuwa nazo Mwadui Diamonds zilibadilishwa na kuwa 25%. Sasa niwaambie kitu cha AJABU kilichotokea Mwadui Diamonds ndio mtaelewa kwa nini Watanzania tumefanywa wajinga waliwao!

Wakati Mwadui Diamonds ikiwa chini ya Tanzania kwa asilimia 51%, wawekezaji walitenga eneo la mgodi na kulifanya kuwa eneo la uwanja wa ndege, ambao pia ulitumika kama uwanja kwa ajili ya ndege za kibisahara (commercial airlines). Sasa kumbe siku zote walijua kwamba hili eneo la uwanja wa ndege ndilo lililokuwa na almasi kwa wingi sana!!!! Siku tu mkataba na serikali ulipobadilishwa kutoka 51% kuwa 25% hapo mwaka 1997 kama sikosei, walitangaza kwamba ule uwanja wa ndege ndani ya Mwadui Diamonds unafungwa ili uchimbwe almasi. Nasikia kuwa lile eneo lililokuwa uwanja wa ndege lilitoa almasi ambazo mgodi haukuwahi kutoa katika historia yote ya Tanzania kuwa na 51%!

Mkapa alitetea kwamba tutafaidika na kodi za mauzo - na kwa ujanja kampuni zikawa zinatangaza hasara au faida kidogo sana ili wasilipe kodi. Na hili la migodi na kukubali hizi 5% lilikuwa mojawapo ya mambo yaliyofanya uhusiano wa Mkapa na Nyerere uzorote hadi tuseme ufe, pamoja na suala la kuuza NBC na mashirika mengine. Nyerere alimwambia Mkapa "Nina wasiwasi siku moja nitasikia umebinafsisha magereza".
Asante mkuu! Maccm Kamwe hata tone moja kwahili hawajui nakwambia!
 
sawa Mkuu. Ila mie wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba, baada ya miaka kumi ya Magufuli, aina gani ya raisi tutapata kuendeleza hii vita ya kuondoa madudu haya yote?

Nadhani ili kujenga mfumo wa maraisi kuwa na woga wa kuidhinisha madudu, kuna umuhimu sana wa kuondoa kinga ya raisi kushitakiwa. Itafanya maraisi wajao wawe na adabu ya kuiwajibikia nchi hii!
Nakuunga mkono kiongozi, Nafikiri rasimu ya katiba ya warioba ingetufaa kama mchakato wa katiba ungeendelea na kuipitisha kuwa katiba kamili.
 
Ni wakati wa kubadilisha katiba tu.Mwarubaini ni hiyo ndiyo itaua vimemo vya kutoka Magogoni kwenda kwa mawaziri.Je na wabunge wa chama tawala wanajifunza nini?
 
Si kweli! Kuna mijitu ambayo ni majangili na wanao ichukia nchi yao wenyewe! Ndiyo maana yanakula tu na kunenepeana afanalek! Muumba wangu Rabuka ingia kazini!
Ndo ujinga wetu huo sasa hatujali,akili 2..
Yani bara lote la afrika linasifika kwa utajiri lkn watuwake ni maskini we unafikiri ni nini hapo kama si ujinga! Watu wachache wanashinda watu wengi!!!
 
Nimeguswa na uchungu alioonyesha Raisi Magufuli juu ya udanganyifu tunaofanyiwa katika sekta ya madini.

Nimejiuliza ikiwa Raisi Magufuli na wananchi kwa ujumla wanailewa kihalisi historia ya mgodi wa Bulhankulu (Bulyanhulu) na nani hasa alikuwa chanzo cha sie kuibiwa?

Labda kwa wale msiojua historia, dhahabu ya mgodi wa Bulyankulu iligunduliwa wakati wa Nyerere miaka ya 1970 na kampuni kutoka Sweden. Wakati wa majadiliano kuhusu uzalishaji, Nyerere alitaka Tanzania iwe na hisa ya 51% na wawekezaji wawe na 49%, kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamond mine. Nyerere alitaka mgodi huu uendeshwe na management ya Watanzania kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamonds. Wawekezaji toka Sweden walikataa wakitaka Tanzania iwe na 49% na wao ndio wawe na 51%. Nyerere alikataa, akawaambia kama hawataki Tanzania iwe na 51% waondoke. Nitamnukuu Nyerere alivyowaambia "dhahabu haiozi, kama hamtaki 49% ondokeni, tutaiacha hiyo dhahabu ardhini hadi tuje tuwe na uwezo wetu wenyewe wa kuichimba".

Sasa baada ya Nyerere kuacha uraisi, makubaliano yaliidhinishwa na Mkapa kutoka ile 49% aliyokataa Nyerere hadi kuwa 5% ya Mkapa, ambayo hata hiyo 5% ilikuja kuondolewa na Kigoda na Tanzania ikawa na 0% (ni wazi Kigoda aliagizwa na Mkapa - kwa hiyo suala la kutowachukulia hatua waliokufa linaweza lisiwe relevant). Ile kampuni ya mwanzo toka Sweden iliyogundua dhahabu Bulyankulu iliposikia Mkapa amekubali 5% ilienda mahakamani kuishitaki serikali na kampuni mpya kutoka Canada ya Bulyankulu Mining, wakisema wao ndio waligundua dhahabu ya Bulyanhulu na walikuwa tayari kuipa Tanzania 49% badala ya 5%. Hadi wakati huo hiyo kampuni ya Sweden ilikuwa na majengo yake pale Bulyankulu, ya ofisi na kulala, na haya ndiyo yaliyotumiwa na hii kampuni ya Canada pale mwanzoni. Serikali ya Mkapa ilisaidiana na kampuni mpya ya Canada ya Bulyankulu Gold mine, nadhani Chenge akiwa Mwanasheria Mkuu, kampuni ya Sweden ikashindwa kesi ambayo kwa kweli ilikuwa ni kushindwa kwa Tanzania kwa kutumia wanasheria wetu wenyewe!

Na si Bulyankulu tu ambayo Mkapa aliibadilisha. Baada ya Nyerere kuondoka madarakani, hata zile 51% tulizokuwa nazo Mwadui Diamonds zilibadilishwa na kuwa 25%. Sasa niwaambie kitu cha AJABU kilichotokea Mwadui Diamonds ndio mtaelewa kwa nini Watanzania tumefanywa wajinga waliwao!

Wakati Mwadui Diamonds ikiwa chini ya Tanzania kwa asilimia 51%, wawekezaji walitenga eneo la mgodi na kulifanya kuwa eneo la uwanja wa ndege, ambao pia ulitumika kama uwanja kwa ajili ya ndege za kibisahara (commercial airlines). Sasa kumbe siku zote walijua kwamba hili eneo la uwanja wa ndege ndilo lililokuwa na almasi kwa wingi sana!!!! Siku tu mkataba na serikali ulipobadilishwa kutoka 51% kuwa 25% hapo mwaka 1997 kama sikosei, walitangaza kwamba ule uwanja wa ndege ndani ya Mwadui Diamonds unafungwa ili uchimbwe almasi. Nasikia kuwa lile eneo lililokuwa uwanja wa ndege lilitoa almasi ambazo mgodi haukuwahi kutoa katika historia yote ya Tanzania kuwa na 51%!

Mkapa alitetea kwamba tutafaidika na kodi za mauzo - na kwa ujanja kampuni zikawa zinatangaza hasara au faida kidogo sana ili wasilipe kodi. Na hili la migodi na kukubali hizi 5% lilikuwa mojawapo ya mambo yaliyofanya uhusiano wa Mkapa na Nyerere uzorote hadi tuseme ufe, pamoja na suala la kuuza NBC na mashirika mengine. Nyerere alimwambia Mkapa "Nina wasiwasi siku moja nitasikia umebinafsisha magereza".
Pole sana kama hujui hisa za vitabuni hazina uhusiano na gawiwo
 
Acha longo longo. Mbona ulikuwa kimya miaka yote hii!? Peleka mikataba yote ya Nchi bungeni haraka iwezekanavyo ili Wabunge wakaichambue kwa kina.
Bavicha sasa hamna hata pa kushika. Magufuli anachanja mbuga. msalimieni babu yenu Lowassa
 
Back
Top Bottom