Rais Magufuli, Watanzania wangejua hii historia ya Bulyankulu na Mwadui wangelia hata zaidi

Nimeguswa na uchungu alioonyesha Raisi Magufuli juu ya udanganyifu tunaofanyiwa katika sekta ya madini.

Nimejiuliza ikiwa Raisi Magufuli na wananchi kwa ujumla wanailewa kihalisi historia ya mgodi wa Bulhankulu (Bulyanhulu) na nani hasa alikuwa chanzo cha sie kuibiwa?

Labda kwa wale msiojua historia, dhahabu ya mgodi wa Bulyankulu iligunduliwa wakati wa Nyerere miaka ya 1970 na kampuni kutoka Sweden. Wakati wa majadiliano kuhusu uzalishaji, Nyerere alitaka Tanzania iwe na hisa ya 51% na wawekezaji wawe na 49%, kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamond mine. Nyerere alitaka mgodi huu uendeshwe na management ya Watanzania kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamonds. Wawekezaji toka Sweden walikataa wakitaka Tanzania iwe na 49% na wao ndio wawe na 51%. Nyerere alikataa, akawaambia kama hawataki Tanzania iwe na 51% waondoke. Nitamnukuu Nyerere alivyowaambia "dhahabu haiozi, kama hamtaki 49% ondokeni, tutaiacha hiyo dhahabu ardhini hadi tuje tuwe na uwezo wetu wenyewe wa kuichimba".

Sasa baada ya Nyerere kuacha uraisi, makubaliano yaliidhinishwa na Mkapa kutoka ile 49% aliyokataa Nyerere hadi kuwa 5% ya Mkapa, ambayo hata hiyo 5% ilikuja kuondolewa na Kigoda na Tanzania ikawa na 0% (ni wazi Kigoda aliagizwa na Mkapa - kwa hiyo suala la kutowachukulia hatua waliokufa linaweza lisiwe relevant). Ile kampuni ya mwanzo toka Sweden iliyogundua dhahabu Bulyankulu iliposikia Mkapa amekubali 5% ilienda mahakamani kuishitaki serikali na kampuni mpya kutoka Canada ya Bulyankulu Mining, wakisema wao ndio waligundua dhahabu ya Bulyanhulu na walikuwa tayari kuipa Tanzania 49% badala ya 5%. Hadi wakati huo hiyo kampuni ya Sweden ilikuwa na majengo yake pale Bulyankulu, ya ofisi na kulala, na haya ndiyo yaliyotumiwa na hii kampuni ya Canada pale mwanzoni. Serikali ya Mkapa ilisaidiana na kampuni mpya ya Canada ya Bulyankulu Gold mine, nadhani Chenge akiwa Mwanasheria Mkuu, kampuni ya Sweden ikashindwa kesi ambayo kwa kweli ilikuwa ni kushindwa kwa Tanzania kwa kutumia wanasheria wetu wenyewe!

Na si Bulyankulu tu ambayo Mkapa aliibadilisha. Baada ya Nyerere kuondoka madarakani, hata zile 51% tulizokuwa nazo Mwadui Diamonds zilibadilishwa na kuwa 25%. Sasa niwaambie kitu cha AJABU kilichotokea Mwadui Diamonds ndio mtaelewa kwa nini Watanzania tumefanywa wajinga waliwao!

Wakati Mwadui Diamonds ikiwa chini ya Tanzania kwa asilimia 51%, wawekezaji walitenga eneo la mgodi na kulifanya kuwa eneo la uwanja wa ndege, ambao pia ulitumika kama uwanja kwa ajili ya ndege za kibisahara (commercial airlines). Sasa kumbe siku zote walijua kwamba hili eneo la uwanja wa ndege ndilo lililokuwa na almasi kwa wingi sana!!!! Siku tu mkataba na serikali ulipobadilishwa kutoka 51% kuwa 25% hapo mwaka 1997 kama sikosei, walitangaza kwamba ule uwanja wa ndege ndani ya Mwadui Diamonds unafungwa ili uchimbwe almasi. Nasikia kuwa lile eneo lililokuwa uwanja wa ndege lilitoa almasi ambazo mgodi haukuwahi kutoa katika historia yote ya Tanzania kuwa na 51%!

Mkapa alitetea kwamba tutafaidika na kodi za mauzo - na kwa ujanja kampuni zikawa zinatangaza hasara au faida kidogo sana ili wasilipe kodi. Na hili la migodi na kukubali hizi 5% lilikuwa mojawapo ya mambo yaliyofanya uhusiano wa Mkapa na Nyerere uzorote hadi tuseme ufe, pamoja na suala la kuuza NBC na mashirika mengine. Nyerere alimwambia Mkapa "Nina wasiwasi siku moja nitasikia umebinafsisha magereza".
IMG_m0l78m.jpg
IMG_20170612_132504.jpg
 
sawa Mkuu. Ila mie wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba, baada ya miaka kumi ya Magufuli, aina gani ya raisi tutapata kuendeleza hii vita ya kuondoa madudu haya yote?

Nadhani ili kujenga mfumo wa maraisi kuwa na woga wa kuidhinisha madudu, kuna umuhimu sana wa kuondoa kinga ya raisi kushitakiwa. Itafanya maraisi wajao wawe na adabu ya kuiwajibikia nchi hii!

Tunahitaji KATIBA haya mnayang'au yakalale pale Keko kwanza.Ati unapigana vita First Lady aliyepita umemteua kuwa Mbunge.Duh unategemea tutengue Mikataba mh!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu BAK, unaheshimika humu JF. Toa comments kulingana na reputation yako. Kwa mfano hili la 5% Tundu Lissu alilipigia sana kelele kwa Mkapa. Nakumbuka sana juu ya hilo. Na nadhani kuna wakati wabunge walikuja juu sana juu ya kubinafsishwa kwa NBC - Mkapa akawatishia, na kwa jinsi wabunge wa CCM wanavyolelewa, wanafyata mkia wakati wakijua kabisa walikuwa na support ya Nyerere kukataa kubinafsishwa kwa NBC.

Nimezidi kuichukia CCM na watawala wake wote.Yaani I wish I could be IGP
 
  • Thanks
Reactions: BAK
0%??
Na mtu akachukua kalamu akatia sahihi, msomi PhD na analipwa mamilioni. Imbeciles
Huwezi kusema hamna rushwa hapo.
 
Ndo ujinga wetu huo sasa hatujali,akili 2..
Yani bara lote la afrika linasifika kwa utajiri lkn watuwake ni maskini we unafikiri ni nini hapo kama si ujinga! Watu wachache wanashinda watu wengi!!!
Badala ya kulalamika na kuendelea kujilaani anza wewe kubadilika maana mabadiliko huanza inside out, start with the man in the mirror kuliko ku point fingers! START!
 
Mmmmh hatari kabisa ndugu zangu. Ebu tumuunge mkono Rais kwa suala hilo. Mkapa bwana!!!! Hakuyaona yote hayo?????
 
Nimeguswa na uchungu alioonyesha Raisi Magufuli juu ya udanganyifu tunaofanyiwa katika sekta ya madini.

Nimejiuliza ikiwa Raisi Magufuli na wananchi kwa ujumla wanailewa kihalisi historia ya mgodi wa Bulhankulu (Bulyanhulu) na nani hasa alikuwa chanzo cha sie kuibiwa?

Labda kwa wale msiojua historia, dhahabu ya mgodi wa Bulyankulu iligunduliwa wakati wa Nyerere miaka ya 1970 na kampuni kutoka Sweden. Wakati wa majadiliano kuhusu uzalishaji, Nyerere alitaka Tanzania iwe na hisa ya 51% na wawekezaji wawe na 49%, kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamond mine. Nyerere alitaka mgodi huu uendeshwe na management ya Watanzania kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamonds. Wawekezaji toka Sweden walikataa wakitaka Tanzania iwe na 49% na wao ndio wawe na 51%. Nyerere alikataa, akawaambia kama hawataki Tanzania iwe na 51% waondoke. Nitamnukuu Nyerere alivyowaambia "dhahabu haiozi, kama hamtaki 49% ondokeni, tutaiacha hiyo dhahabu ardhini hadi tuje tuwe na uwezo wetu wenyewe wa kuichimba".

Sasa baada ya Nyerere kuacha uraisi, makubaliano yaliidhinishwa na Mkapa kutoka ile 49% aliyokataa Nyerere hadi kuwa 5% ya Mkapa, ambayo hata hiyo 5% ilikuja kuondolewa na Kigoda na Tanzania ikawa na 0% (ni wazi Kigoda aliagizwa na Mkapa - kwa hiyo suala la kutowachukulia hatua waliokufa linaweza lisiwe relevant). Ile kampuni ya mwanzo toka Sweden iliyogundua dhahabu Bulyankulu iliposikia Mkapa amekubali 5% ilienda mahakamani kuishitaki serikali na kampuni mpya kutoka Canada ya Bulyankulu Mining, wakisema wao ndio waligundua dhahabu ya Bulyanhulu na walikuwa tayari kuipa Tanzania 49% badala ya 5%. Hadi wakati huo hiyo kampuni ya Sweden ilikuwa na majengo yake pale Bulyankulu, ya ofisi na kulala, na haya ndiyo yaliyotumiwa na hii kampuni ya Canada pale mwanzoni. Serikali ya Mkapa ilisaidiana na kampuni mpya ya Canada ya Bulyankulu Gold mine, nadhani Chenge akiwa Mwanasheria Mkuu, kampuni ya Sweden ikashindwa kesi ambayo kwa kweli ilikuwa ni kushindwa kwa Tanzania kwa kutumia wanasheria wetu wenyewe!

Na si Bulyankulu tu ambayo Mkapa aliibadilisha. Baada ya Nyerere kuondoka madarakani, hata zile 51% tulizokuwa nazo Mwadui Diamonds zilibadilishwa na kuwa 25%. Sasa niwaambie kitu cha AJABU kilichotokea Mwadui Diamonds ndio mtaelewa kwa nini Watanzania tumefanywa wajinga waliwao!

Wakati Mwadui Diamonds ikiwa chini ya Tanzania kwa asilimia 51%, wawekezaji walitenga eneo la mgodi na kulifanya kuwa eneo la uwanja wa ndege, ambao pia ulitumika kama uwanja kwa ajili ya ndege za kibisahara (commercial airlines). Sasa kumbe siku zote walijua kwamba hili eneo la uwanja wa ndege ndilo lililokuwa na almasi kwa wingi sana!!!! Siku tu mkataba na serikali ulipobadilishwa kutoka 51% kuwa 25% hapo mwaka 1997 kama sikosei, walitangaza kwamba ule uwanja wa ndege ndani ya Mwadui Diamonds unafungwa ili uchimbwe almasi. Nasikia kuwa lile eneo lililokuwa uwanja wa ndege lilitoa almasi ambazo mgodi haukuwahi kutoa katika historia yote ya Tanzania kuwa na 51%!

Mkapa alitetea kwamba tutafaidika na kodi za mauzo - na kwa ujanja kampuni zikawa zinatangaza hasara au faida kidogo sana ili wasilipe kodi. Na hili la migodi na kukubali hizi 5% lilikuwa mojawapo ya mambo yaliyofanya uhusiano wa Mkapa na Nyerere uzorote hadi tuseme ufe, pamoja na suala la kuuza NBC na mashirika mengine. Nyerere alimwambia Mkapa "Nina wasiwasi siku moja nitasikia umebinafsisha magereza".

Tuliposema Marehemu Julius Kambarage Nyerere aliuwawa kuna watu walitubeza sana wakasema sisi ni Mafala! Hoja ya kupeleka mswada Bungeni tufute Immunity ya Rais kushtakiwa kwa Makosa aliyofanya akiwa Madarakani ni zaidi ya Katiba mpya hata JPM hatadhubutu kutawala kwa impunity kwani atajua fika akimaliza muda wa kuwa Rais atapelekwa Mahakamani ! Ila pia kuwepo na sheria ya Rais kuwa impeached for whatever he does kabla hajamaliza muda wake that is anavunja katiba and we shall be home and dry! The same will apply to all! Haiwezekani mtu anakwiba fedha halafu baada ya kuondolewa madarakani au kuachana na serikali anakuwa bonge la Investor kama Nazir Karamagi na Kampuni ya TICTS inayotoa mizigo bandarini na Jakaya Mrisho Kikwete akawaongezea Muda for 20years halafu anajifanya sijui yeye ni Mkulima/ Mfugaji pamoja na kuanzisha a very luxurious Foundation kama ile ya Marais wezi wa Marekani and even Bill Gate! Hizo fedha za foundation si ni zile hongo na mapato kutoka Symbion, Barrick, IPTL and the likes halafu you people are crying foul kwamba wana Kinga! Shame on Tanzanians! Magufuli go Baba utaweka Bonge la Legacy ! Fanya Uamuzi mgumu! Kila mtu atabeba Mzigo wake mwenyewe! Tufanye maandamano for one week tumuunge mkono JPM baada ya kuwatoa upepo hao miungu tutamgeuka as usual. Ukiwa kwenye shimo hata Chizi akikusaidia kubali utamsema ni Chizi akishakuokoa!
 
Nimezidi kuichukia CCM na watawala wake wote.Yaani I wish I could be IGP

Hahaha! Mkuu, tuliza moyo. CCM au Cahdema kama vyama (systems) havina tatizo. Tatizo lililopo ni aina ya Watanzania kama society. Tumekuwa watu wenye mentality za ajabu sana. Tunatakiwa tuwe na mindset ya Tanzania kwanza na mengine yataenda sawa.
 
Ni sawa mkuu,lakini watanzania wametokea mbali,mpaka kufikia hapa kifikra na kichangamoto,tulikuwa Tupo katika Giza nene,la kutojijua,kuna makosa yakihistoria ambayo yalichangia kuleta siasa mbovu,iliyokosa ukweli kwa kiasi kikubwa na bado,inaendelea kuathiri uhalisia wa namna fulani,ambayo bado inaendelea kulitafuna taifa letu,bila ya kuanza kuwanyoshea vidole,

Hawa na wale,la kwanza kabisa Ni udhaifu wa katiba yetu,ambayo kwa kiasi kikubwa imekosa sheria na mikakati ya kulinda,rasilimali ya Taifa,utawala bora wa sheria,mipaka ya uongozi na maamuzi,kwa upande wa Nyerere na Mwinyi kila mmoja ana mazuri yake na mabaya yake,Nyerere alileta ujamaa ambao pia ulimshinda,alihubiri siasa zaidi,ill kuleta uzalendo,lakini alisahau mishahara ya wananchi wake,na kuliingiza taifa katika njaa,rushwa,na ubadhirifu,hicho ndicho kilikuwa chanzo,na Mwinyi alituokoa kutoka katika mkwamo huu wa hali mbaya kimaisha,ambapo nguvu,sabuni ya kukogea,sukari na vitu muhimu katika maisha ya kila siku ilikuwa tunu,na kuvipata ilibidi ipite rushwa,na yeye akaanzisha biashara huru,ambayo ndiyo iliyoanza kutukwamua katika Hali mbaya tuliyokuwa nayo kabla,ambayo ndio vile vile kwa upande wa pili ,

serikali ya CCM iliendeleza kuchota mikopo ya nje na kuendeleza ufisadi,ilikuwa chanzo cha kuliingiza taifa katika mikopo ya kimataifa,sasa watanzania tusome kwa yaliyopita,kutengeneza taifa kwa yanayokuja mbele,kitaifa na kimataifa.sasa serikali hii ya CCM,iache mitizamo ya nyuma ya kiutawala,iachie haki na sheria zichukue nafasi katika uongozi wa taifa hili,huku wakishirikiana na wapinzani kwa nia safi sana,kuleta maendeleo ya taifa hili,na hilo linatakikana lifanye kazi sasa,Kama kweli tunalipenda taifa letu.

Mkuu, ni lini tutaacha kusingizia ujinga wa kiuongozi uliokuja baada ya Nyerere na matokeo yake kuwa umetokana na sera za Nyerere? Tunataka tumfanye Nyerere kuwa ndio chanzo cha matatizo yetu na IPPL, ACASIA, Escrow, Richmond, EPL nk? IN fact, tunaposoma historia ya Nyerere kwa jinsi alivyoweka msimamo kama hili suala la mgodi wa Bulyankulu, tunapaswa tumshukuru sana, kwamba angalau aliacha nchi yetu ikiwa na rasilimali zetu intact hazijafididiwa.

Kurekebisha sera za Nyerere ili tufanye haraka kimaendeleo lilikuwa suala dogo sana, na ni kweli Mwinyi alianza vizuri. Lakini hatuwezi kusahau ubaya uliokuja na mabadiliko ya sera yaliyoletwa na Mwinyi - ufisadi na kutosimamia serikali vizuri katika utendaji. Sasa hilo tumlaumu Nyerere na sera zake? Au umesahau kwamba wakati wa Mwinyi serikali iliwekwa mfukoni na watu wachache, na hasa watu wa asili ya kiasia na wafanya biashara wakubwa, na hakuna lolote serikali ilifanya? Leo hii kule South Afrika Zuma analaumiwa kwa kosa lile lile alilofanya Mwinyi - kuachia serikali itekwe na wafanya biashara wa kihindi kina Gupta. Kwa hiyo Wa South Afrika wamlaumu Mandela?
 
Nimeguswa na uchungu alioonyesha Raisi Magufuli juu ya udanganyifu tunaofanyiwa katika sekta ya madini.

Nimejiuliza ikiwa Raisi Magufuli na wananchi kwa ujumla wanailewa kihalisi historia ya mgodi wa Bulyankulu (Bulyanhulu) na nani hasa alikuwa chanzo cha sie kuibiwa?

Labda kwa wale msiojua historia, dhahabu ya mgodi wa Bulyankulu iligunduliwa wakati wa Nyerere miaka ya 1970 na kampuni kutoka Sweden. Wakati wa majadiliano kuhusu uzalishaji, Nyerere alitaka Tanzania iwe na hisa ya 51% na wawekezaji wawe na 49%, kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamond mine. Nyerere alitaka mgodi huu uendeshwe na management ya Watanzania kama ilivyokuwa kwa Mwadui Diamonds. Wawekezaji toka Sweden walikataa wakitaka Tanzania iwe na 49% na wao ndio wawe na 51%. Nyerere alikataa, akawaambia kama hawataki Tanzania iwe na 51% waondoke. Nitamnukuu Nyerere alivyowaambia "dhahabu haiozi, kama hamtaki 49% ondokeni, tutaiacha hiyo dhahabu ardhini hadi tuje tuwe na uwezo wetu wenyewe wa kuichimba".

Sasa baada ya Nyerere kuacha uraisi, makubaliano yaliidhinishwa na Mkapa kutoka ile 49% aliyokataa Nyerere hadi kuwa 5% ya Mkapa, ambayo hata hiyo 5% ilikuja kuondolewa na Kigoda na Tanzania ikawa na 0% (ni wazi Kigoda aliagizwa na Mkapa - kwa hiyo suala la kutowachukulia hatua waliokufa linaweza lisiwe relevant). Ile kampuni ya mwanzo toka Sweden iliyogundua dhahabu Bulyankulu iliposikia Mkapa amekubali 5% ilienda mahakamani kuishitaki serikali na kampuni mpya kutoka Canada ya Bulyankulu Mining, wakisema wao ndio waligundua dhahabu ya Bulyanhulu na walikuwa tayari kuipa Tanzania 49% badala ya 5%. Hadi wakati huo hiyo kampuni ya Sweden ilikuwa na majengo yake pale Bulyankulu, ya ofisi na kulala, na haya ndiyo yaliyotumiwa na hii kampuni ya Canada pale mwanzoni. Serikali ya Mkapa ilisaidiana na kampuni mpya ya Canada ya Bulyankulu Gold mine, nadhani Chenge akiwa Mwanasheria Mkuu, kampuni ya Sweden ikashindwa kesi ambayo kwa kweli ilikuwa ni kushindwa kwa Tanzania kwa kutumia wanasheria wetu wenyewe!

Na si Bulyankulu tu ambayo Mkapa aliibadilisha. Baada ya Nyerere kuondoka madarakani, hata zile 51% tulizokuwa nazo Mwadui Diamonds zilibadilishwa na kuwa 25%. Sasa niwaambie kitu cha AJABU kilichotokea Mwadui Diamonds ndio mtaelewa kwa nini Watanzania tumefanywa wajinga waliwao!

Wakati Mwadui Diamonds ikiwa chini ya Tanzania kwa asilimia 51%, wawekezaji walitenga eneo la mgodi na kulifanya kuwa eneo la uwanja wa ndege, ambao pia ulitumika kama uwanja kwa ajili ya ndege za kibisahara (commercial airlines). Sasa kumbe siku zote walijua kwamba hili eneo la uwanja wa ndege ndilo lililokuwa na almasi kwa wingi sana!!!! Siku tu mkataba na serikali ulipobadilishwa kutoka 51% kuwa 25% hapo mwaka 1997 kama sikosei, walitangaza kwamba ule uwanja wa ndege ndani ya Mwadui Diamonds unafungwa ili uchimbwe almasi. Nasikia kuwa lile eneo lililokuwa uwanja wa ndege lilitoa almasi ambazo mgodi haukuwahi kutoa katika historia yote ya Tanzania kuwa na 51%!

Mkapa alitetea kwamba tutafaidika na kodi za mauzo - na kwa ujanja kampuni zikawa zinatangaza hasara au faida kidogo sana ili wasilipe kodi. Na hili la migodi na kukubali hizi 5% lilikuwa mojawapo ya mambo yaliyofanya uhusiano wa Mkapa na Nyerere uzorote hadi tuseme ufe, pamoja na suala la kuuza NBC na mashirika mengine. Nyerere alimwambia Mkapa "Nina wasiwasi siku moja nitasikia umebinafsisha magereza".
masikini mzee wetu nyerere. RIP
 
Mkuu, ni lini tutaacha kusingizia ujinga wa kiuongozi uliokuja baada ya Nyerere na matokeo yake kuwa umetokana na sera za Nyerere? Tunataka tumfanye Nyerere kuwa ndio chanzo cha matatizo yetu na IPPL, ACASIA, Escrow, Richmond, EPL nk? IN fact, tunaposoma historia ya Nyerere kwa jinsi alivyoweka msimamo kama hili suala la mgodi wa Bulyankulu, tunapaswa tumshukuru sana, kwamba angalau aliacha nchi yetu ikiwa na rasilimali zetu intact hazijafididiwa.

Kurekebisha sera za Nyerere ili tufanye haraka kimaendeleo lilikuwa suala dogo sana, na ni kweli Mwinyi alianza vizuri. Lakini hatuwezi kusahau ubaya uliokuja na mabadiliko ya sera yaliyoletwa na Mwinyi - ufisadi na kutosimamia serikali vizuri katika utendaji. Sasa hilo tumlaumu Nyerere na sera zake? Au umesahau kwamba wakati wa Mwinyi serikali iliwekwa mfukoni na watu wachache, na hasa watu wa asili ya kiasia na wafanya biashara wakubwa, na hakuna lolote serikali ilifanya? Leo hii kule South Afrika Zuma analaumiwa kwa kosa lile lile alilofanya Mwinyi - kuachia serikali itekwe na wafanya biashara wa kihindi kina Gupta. Kwa hiyo Wa South Afrika wamlaumu Mandela?
Mkuu Nyerere,Mwinyi na wengine Ni binaadamu Kama Mimi na wewe tuna mazuri yetu na mabaya yetu,Sasa kwa Nyerere Ana makosa mengi amekuja nayo na ameyawacha na yalisabiabisha madhara kwa taifa leta vile vile,Moja wapo Ni rushwa,ubadhirifu Ni,wakati wa Nyerere,nchi Iliingia katika Hali ngumu kimaisha,kwa ajili ya maamuzi yake peke yake,alikua kwa jina linguine,tukwimwita mzee haambiliki au kifimbo,ukumbuke wakati wa utawala wa Chama kimoja,kuna mengi ya matokeo baada ya uhuru,ambayo ni mazuri na mabaya,ukisema sana kutoa makosa serikali,unamalizikia korokoroni,Mwinyi kwa upande wake hakuipata nchi tokea uhuru,isipokua alikabidhiwa nchi,ikiwa katika Hali mbaya imechoka,na alichukuliwa kutoka Zanzibar pale,alipouinua uchumi kule Zanzibar,kwa kuanzisha biashara huru,kwa upande wangu Mwinyi ndie mkombozi wa taifa hili,yeye ndiye aliyeuvunja,siasa mbaya za uchumi,alizoziacha Nyerere,ambazo yeye mwenyewe
,alirizika na hilo.
Suala la Zuma,halina mahusiano kabisa na Mwinyi,Mwinyi alikuwa mzalendo wa kweli,Zuma kaikuta South Africa nchi inayojitegemea,tofauti na Mwinyi.Suala la kulaumu halipo,isipokuwa tunapambanua historia ya uhalisia,hakuna anaelaumiwa,Heshima ya Nelson Mandela ziko juu kabisa,mfano harakati zake za kupigania uhuru zipo juu,katika nchi iliyokuwa na ubaguzi wa rangi,hasa wazungu weupe wachache,wakiwabagua waafrika walio wengi,uzalendo na ujasiri wake ulipelekea kuwekwa mahabusu Miata 27 ,kwa upande wa Tanganyika historia ya uwazi kabisa ya kupiginia uhuru,iliyokuwa na watu kama Abduwahid sykes,Julius Nyerere,Mtemvu na kadhalika,ilififirishwa na ndio ikaenziwa hii ambayo,inalinda maslahi ya CCM,sasa nadhani kwa upande wako,kutokana kwa ulivyosomeshwa shule,ambao una hisia ya kwamba Ni dhambi kubwa,kumsema Nyerere makosa yake,watanzania tuungane tujenge nchi yetu,tuache siasa tulete maendeleo,Serikali iliyokuwepo iwe na nia njema,kwa wananchi wote,bill kujali itikadi gani,tuweke uzalendo wa kuilinda na kuleta mandeleo,utekelezaji wa katiba nzuri ndio msingi wa maendeleleo.
Mungu ibariki Tanzania
 
Mkuu hii ni mpya. Napenda Lumumba wote waisome ili wajue adui namba moja wa Tanzania si wawekezaki ila CCM kwa ujumla wao.
 
Back
Top Bottom