VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Charles Kitwanga ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi. Wananchi wa Misungwi,wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana,hawakuwa wanaikataa CCM. Jimbo hilo lilikuwa la CCM tu.WanaMisungwi hawakuwa wanamtaka Charles Kitwanga. Wanamjua kuliko unavyomjua.
Kitwanga anajulikana kwa kujiamini kuliko kiasi kitakiwacho;kujisifusifu;kuchukulia mambo kiwepesiwepesi na kadhalika. Mambo ya ulabu pia walikuwa wanajua kuhusu huyo aliyekuwa mgombea wa Ubunge wa CCM. Kitwanga hakuwa anatosha kuwa Mbunge. WanaMisungwi walishakata shauri kumkataa.
Uchaguzini,mwaka jana,WanaMisungwi walikuwa wanakuhitaji sana. Walikuwa wanakuamini kwa kauli zako na matendo yako. Ulipofika jimboni mwao,ukawaomba wanaMisungwi wamchague Kitwanga kwakuwa unamfahamu,unamjua,rafikiyo,unampenda na umesoma naye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
WanaMisungwi wakakuamini. Wakamchagua Kitwanga. Katika kuonesha kuwa Kitwanga anafaa,unampenda,rafikiyo,unamfahamu na umesoma naye,ukamteua Waziri wa Mambo ya Ndani. WanaMisungwi wakashangilia na wengine kulia. Hawakuamini kilichotokea. Wakasubiri matokeo. Mbunge wao jana katenguliwa Uwaziri wake kwa ulevi. Tena Bungeni akiwajibika. Kitwanga halisi anayejulikana na wanaMisungwi akajitokeza.
Amini nakuambia,wanaMisungwi hawana pa kuficha nyuso zao kwa aibu:Mbunge wao mlevi hadi muda wa kuwajibika!? Watabaki kukulilia hadi 2020 kwakuwa uliwaaminisha tofauti. Utakwenda tena kumnadi Kitwanga mwaka 2020?
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam