Rais Magufuli: Wanafunzi UDOM waliofeli wakatafute vyuo vya saizi yao

Nakwambia katika nchi za ajabu moja ni hii,kwani utawala uliopita ulikuwa haujui hawa watoto ni faliure??kama kweli mnataka kuondoa taifa la vilaza kwanini wasije na maboresho ambayo hayata athiri mpango ulio kuwepo,sidhani kama watangulizi walikuwa wana niambaya kiasi hicho japo kunamapungufu katika mkakati wao
Hata isue ya makontena bandarini viongozi walikuwepo pia!!;xo usishangae!!
 
Hakika. Anawanyoosha sana. Sijui wale vilaza watasemaje tena


kumbe hatuna serikali mana wabunge wote walitoka nje ina maana wabunge wote vilaza waliungana kutetea vilaza ndo mana meza zinapigwa sana kwa kuwa vilaza kila kitu ni ndiooooooooo
 
Kweli siasa huinua na siasa huangusha,ukipata div2 inaweza isitakiwe kwa kuwa kuna div1.Kanuni ya kujifunza ni UTAYARI,MAZOEZI na UZOESHI ikiwa mhitaji ana uwezo wa kupokea maarifa mapya kwa kuyalinganisha na kuyatofautisha na aliyoyapata ya mwanzo.Hapa UKILAZA hutoweka.
 
Haya ni matokeo ya mtoto wa Rais wetu.

Matokeo ya mtoto *kilaza* wa Rais, alimaliza form 4 2012:

S1071/0102

JESCA JOHN MAGUFULI

Div IV - 30

CIV-D HIST-D GEO-D KISW-F ENGL-C B/MATH-F COMM-F
 
Magufuli aliwahi sema, " Nchi hii ilikuwa imejaa madalali na wapiga dili( aka mission town)
Ndio maana kila mtu now anamlalamikia magufuli cause hela haioni. Wale waliokuwa na tenda za chakula kwenye sherehe za serekali, washona sare cjui za siku ya uhuru etc. Sasa hivi kila mmoja analalamika magufuli ni dikteta. Wengine wanafikia mahali wanasema oh bora mda wa JK.... Like seriously. Mm sio mwanachama wa CCM, ila namuomba mungu aendelee kumlinda huyu mtu. He is not perfect( who is???) ila he is way better than others. Sasa kijana, mzee au mwanafunzi. Anza kujijengea dhana ya life is not a gamble, you have to struggle to win. Bila kufanya kazi kwa bidii na ueledi, utaendelea kusimama juani kupoteza mda wako kusikiliza kelele za mbunge jukwaani akikuhamasisha kuchukia serikali wakati yeye anajenga hoteli ya kisasa kwao..... Am out..
 
Mkuu, ahsante sana kwa hii video. Kuna kipande pia Rais ameongea kuwa kuna wanasiasa walipinga kufukuzwa kwa vilaza kwa sababu na wao ni vilaza. Hapo naona umepapotezea sijui kwa sababu gani
tukianza kuwa categorise watu wetu kama vilaza au si vilaza haifai maana hata wazee wetu kule kijiini tutawita vilaza.
Tafsiri ya kilaza hasa ni ipi?
 
Jaribu kufuatilia tena. Kama umesikia basi umesikia vibaya sana tena sana. Tuliza kichwa
Ndugu yangu nimeifuatilia Hotba ilyowekwa humu. Pale 1.8 hadi 1.26: Raisi kasema: Mie namsifia Purofesa Mkumbo wa ICT (pamoja na kuwa mimi (yaani Mhe Rais) ni wa CCM, Kwa sababu alitoa mwongozo..... Na hapa nimeona vema. Nimeona kamera ilihamia kwa Mkumbo Kitila. Ana miwani na amenyoa upara....Ndiye! Je, huyu siku hizi ni wa ICT....ama Mheshimiwa alikuwa anamaanisha wa ACT..?
 
Duuu!Jamaa hatari anatumbua hadi wanafunzi,bila shaka atafuta matokeo tote ya wanafunz waliomalza miaka10 iliyopta.
 
UFAFANUZI.!

By Malisa GJ

Baada ya timua timua ya wanafunzi walioko vyuoni imeonekana kuna watu wanajadili vitu wasivyovijua vizuri. Watu wengi wanaonekana kuchanganya kati ya wanafunzi waliotimuliwa UDOM na wale waliotimuliwa vyuo vingine kwa kukosa sifa. Ni vizuri wakati wa kujadili tukaelewa tunajadili kundi gani kati ya haya mawili.

#KUNDI_LA_KWANZA ni wale waliopata division one hadi three na wakapata alama "A" au "B" kwenye masomo ya Sayansi (Physics, Maths, Chemistry, Biology). Hawa walidahiliwa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa program maalumu ya miaka mitatu ya kupata diploma ya ualimu wa sekondari.

Utaratibu huu haukuanzishwa na wanafunzi hawa. Ulianzishwa na Rais JK na kupigiwa vigelegele na wafuasi wote wa CCM. Leo JPM anaona ni utaratibu wa hovyo na anawaadhibu wanafunzi kwa kuwafukuza. Cha ajabu wafuasi walewale waliomshangilia JK akianzisha mfumo huu ndio haohao wanaomshangilia JPM akiufuta. Huu ni uzwazwa wa shahaha ya juu kabisa ya uzamivu uliobobea (PhD with gigantic Experiece).

Kwanini tunawahukumu watoto wasio na hatia? Yawezekana tunahitaji marekebisho ktk mfumo wa elimu lakini si kwa style hii. Nadhani kama JPM angekua na busara angesubiri watoto hawa wamalize kisha ndo aufute huu mfumo. Lakini kuufuta sasa hivi wakati ameshawapotezea miaka mitatu ni ukatili. Wanafunzi hawa wangeendelea form five (sifa wanazo) kwa sasa wangekua first year chuo kikuu. Kwahiyo wanafunzi waliotimuliwa UDOM hawajafeli kama inavyoenezwa.

Na kama mfumo huu ulikua haufai kwanini vijana wa CCM mlimshangilia JK alipokua anauanzisha? Si mngemwambia tu wazi kuwa Mzee hii si sawa. But mlipiga makofi kumshangilia halafu leo amekuja mtu mwingine ameufuta mnamshangilia tena?

Hivi vijana wa CCM hamnaga "ujasiri" wa kumkosoa kiongozi awapo madarakani hadi msubiri atoke? Kwa hali hii nina wasiwasi hata JPM akiondoka akija mwingine akarudisha mfumo huu mtamshangilia tena na kuona JPM alifanya ugoro. Kwanini hamna national interest, badala yake mmekuwa wapiga zumari wa Rais aliyeko madarakani hata kama amekosea mnamshangilia tu?

Anyway. Lakini je ni dhambi mtu wa kidato cha nne kwenda chuo kikuu? Je Utaratibu huu ni mpya nchini? Jibu si dhambi. Na utaratibu huu si mpya. Issue sio mtu kuwa chuo kikuu, issue ni anasoma nini huko chuo kikuu. Hivi mhitimu wa kidato cha 4 akienda chuo kikuu akasomea "certificate" tutashangaa? Mbona wapo wengi tu wamejaa huko UDSM, UDOM, SAUT, IFM, CBE, Mzumbe wamesoma "certificate" mwaka mmoja na baadae Diploma na hata "degree" lakini hatuwashangai?

The same applies kwa hawa vijana wa UDOM. Wamemaliza form four wamefaulu vzr wakaenda kusomea Diploma ya ualimu miaka mitatu. Ni sawa na kusema mwaka mmoja wamesoma certificate (foundation course), miaka miwili "diploma". Je hapo kuna ubaya gani?

Eti tunawashangaa na kuwaona wa ajabu. Kabla hatujawashangaa vijana hawa wameendaje chuo kikuu bila kufika form six, tumshangae kwanza Prof.Mark Mwandosya amekuaje Profesa wakati HAIJUI form five wala six.

Mwandosya alipomaliza form four pale Malangali sekondari mwaka 1968, alienda DIT kusoma certificate ya Engineering (FTC) kisha akajiunga na Aston University huko Uingereza kwa BSc. (Engineering). Mbona huyu hatumshangai tunashangaa hawa watoto wa UDOM? Kutokwenda form five sio kitu cha ajabu. Na tuna wataalamu wengi tu hawajapita form five lakini wanafanya vzr sn.

#KUNDI_LA_PILI
Hiki ni kundi la vijana wapatao kama 400+ waliokua wamedahiliwa vyuo vikuu mbalimbali nchini wakitokea form four na wamefeli halafu wanasoma degree wakati hawana "foundation course" yoyote ya certificate wala diploma. Hawa wametimuliwa na mama Ndalichako. Nimeona orodha yao wengi ni watoto wa vigogo. Ajabu walikua wakipewa mikopo 100%. Mmoja wao ni Scholastica Nchimbi aliyekua chuo Kikuu cha St.Joseph akisomea Civil Engineering. Anadaiwa kuwa na division four ya point 29 na hajasoma foundation course popote, lakini alikua chuo kikuu na ana mkopo 100%.

Hawa wa kundi la pili naunga mkono watimuliwe au wahamishiwe level za chini wanazozimudu. Kama wanasoma degree wahamishiwe certificate. Lakini lazima tujiulize waliingiaje? Kama ni watoto wa vigogo it means kuna matumizi mabaya ya madaraka hapa, hivyo viongozi waliohusika ni muhimu wawajibishwe. Pia waliowadahili nao wachukuliwe hatua. Vyuo vilivyowapokea navyo viwajibishwe.

Lakini cha ajabu ni kuwa viongozi wenye tuhuma hizi "hawagusiki". Mmoja wa viongozi ambaye inadaiwa mwanae yupo kundi hili ni RC mmoja ambaye amepewa ubunge juzijuzi. Hivi kiongozi kama huyu aliyeshawishi mwanae ajiunge chuo kikuu wakati ana division four ya 29 anapewaje zawadi ya ubunge kama nyongeza?

Kwa hiyo tunapojenga hoja tujue kuna makundi mawili yanaguswa. Usije kuchanganya vijana wa UDOM (Magenius) na watoto wa kina Mu-longolongo (vilaza) kwa kuwa wote wametimuliwa. Usiwavictimize vijana wa UDOM kwa kuwafananisha na watoto wa mawaziri waliotimuliwa huko St.Joseph na kwingineko. Ni dhambi.!

Malisa G.J
 
Mimi naeleza fact tu wewe ninakupuuza. Unachokifanya ni ushabiki wa kijinga tu. Mfumo wa nchi umeoza we idiot tambua hilo. Jiulize hapo UDOM nani aliwaleta hao wanafunzi? Unajua alichoongea Waziri wa elimu kuhusu wanafunzi hao bungeni? Na anachoongea Rais sasa umewianisha? Tumia akili we mjinga. Mjinga ni sifa yako.
Waliowadahili c ndo walotumbuliwa sasa unauliza nn!!?;acha kashfa wewe!!;hii nchi ilioza!!
 
Ndugu yangu nimeifuatilia Hotba ilyowekwa humu. Pale 1.8 hadi 1.26: Raisi kasema: Mie namsifia Purofesa Mkumbo wa ICT (pamoja na kuwa mimi (yaani Mhe Rais) ni wa CCM, Kwa sababu alitoa mwongozo..... Na hapa nimeona vema. Nimeona kamera ilihamia kwa Mkumbo Kitila. Ana miwani na amenyoa upara....Ndiye! Je, huyu siku hizi ni wa ICT....ama Mheshimiwa alikuwa anamaanisha wa ACT..?
Mkumbo ni huyo huyo. Na si kweli ICT. Kwanza hakuna chama kilichosajiliwa kwa jina hilo. Tulikuwepo hapo kiwanjani. ACT mkuu.
 
wabongo hua tunajua sana kutwist maneno kukidhi haja zetu.. kila nikisikiliza hotuba za magufuli namna anavoelezea mambo na namna anavoelezea EXCEPTIONS kwenye kila misimamo anayokua anaiweka pamoja na kua ana ki lugha cha ukali kidogo binafsi hua namwelewa mno lakin shida inakuja nikisema niingie jf kuchek maoni ya watu.. nabaki tu najiuliza labda hotuba niloangalia ilikua sio yenyewe
 
Back
Top Bottom